Miaka 20 ijayo, majina ya Asili Tanzania yatakuwa yamefutika kabisa

Fikra finyu sana hz.. Hata hayo majina ya waarabu na wazungu bado nayo yana udini mwingi...!! Majina haya ya afrika kwanza yalikuwa yanasaidia mtu kujua ametokea wapi ili hata ukipata tatzo watu wanajua wapi watapata ndugu zako.

Sasa hv unaweza ukatoka dar mwanza utaenda dar na ww ni msukuma na usijue ndugu yako wala usipate mtu wa kukusaidia kwasbb kila mtu ana jina la slave master wake. Alafu kingine inabidi ujifunzr historia ktk mlengo wa waafrika pia na sio huo mlengo wa wazungu unakuaminisha eti waafrika wanaukabila ukabila uliletwa na wakoloni kwania kuintroduce pinciple ya divide and rule...mfno ni watusi na wahutu mfaransa ndio aliyeanzisha ukabila kwa kuwafanya kabila moja kuwapa hadhi na jingine kulishusha
 
tuntufye au tuntu kama tumuitavyo yupo mtaani kwangu huwa nawaza wazazi wake walikuwa wanawaza nini sijui,ingawa ana jina jingine la mjini.

kuna mabaharia nimekutana nao waliitwa ndundu,kirundu,chililo,mponda dodo,cholo
yaani majina hayana hata ladha,kama wale jamaa wahadzabe wale mtu anaitwa khunkhu.
 
Mbona mimi bado natumia na nitaendelea kutumia jina la Kuku wa zabanga papa fololo, Kipeme biss ya mboka?
 
Ndo hivo tena wengi wameshapumbazwa
 
Chagua haya ya kienyeji: Shida, taabu, mateso, majuto, simanzi, chausiku, kisirani, kivuruge,n.k
 
Hayawatesi,,,,mnajitesa wenyewe kwa kukimbilia mambo ya wengine na kuacha ya kwenu
 
Leo 95% ya watoto wanaozaliwa majini ni James, John, Abdalah, Mohamed, Abdrazak, Jayden, Johnson, Beatus, Julius, julieth, Jayna, Jasmine, Chris, nk nk.kwenye intervi
Leo tumetoka kwenye kuinterview watu kwenye kada fulani nimeshituka interviewee mmoja wa kike anaitwa Loveson
 
Mkuu hivi wazazi wako wangekupa jina la kisoda au kichuguu, ungefurahi?

Majina mengine ya kiafrika yana maana ya uchuro mtupu.
 
Sasa majina kama mateso, tabu kweli umwit mwanao, Mi wa kwanza kukataa majina ya mababu nilivopata ka akili kidogo
 
Mambo ya walimwengu waachie wenyewe...

Unaona hata magome ya miti hatuvai tena tunapiga pamba nyepesi...
 
Sisi wahaya tupo proud na majina yetu ya asili ujinga ni kutojua tu maana majina yote duniani yana fanana maana utofouti ni utamkwaji katika lugha Love Pendo glad furaha
 
Kazi kubwa ya kwanza aliyofanya mzungu ni kuhakikisha mtu mweusi anaikataa asili na ustaarabu wake na kufuata wa kigeni.......

Kitu ambacho hatujui ni kuwa hayo majina ya wazungu ndio majina yao ya asili........

Huu ni ulimbukeni na ulemavu wa akili aliotuachia wakoloni........
 
Mkuu hivi wazazi wako wangekupa jina la kisoda au kichuguu, ungefurahi?

Majina mengine ya kiafrika yana maana ya uchuro mtupu.
Kuna wazungu wanaitwa Wood, Stone, Drinkwater etc, mbona nayo uchuro tu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…