Miaka 30 ijayo kabila la kichaga kutoweka kabisa Kilimanjaro

rosemarie

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2011
Posts
6,887
Reaction score
3,420
Ishara zote zinaonyesho miaka 30 ijayo kabila maarufu la kichaga litafutika kabisa mkoani Kilimanjaro.

Sababu kuu ni kama zifuatazo:
  • Wachaga wengi wanaoa na kuolewa na makabila tofauti,wengi walio oa kabila tofauti wakifa wake zao ambao ni kabila tofauti wanarithi Mali za mume zao pamoja na shamba LA urithi alilopewa Mme wake.
  • Watoto wengi Wachaga miaka ya sasa hivi wanazaliwa mijini na mikoani na wanakua na tatizo la kutokujua mila na desturi za kichaga sababu hiyo inafanya wawe waswahili.
  • Wanawake wana olewa uchagani wanaleta ndugu zao pindi wenye mji wanapokufa kama kawaida mnajua wanaume wanatangulia kufa. Mfano mzuri ni Jirani yetu mwanamke wa kipare aliolewa kwenye ukoo wetu wa Lema baada ya mume wake kufa na wakwe zake alileta ndugu zake wengine wakaoa na kuolewa huku machame.
  • Wachaga halisi waliorithi Mali na mashamba kutoka kwa wazee wetu hawakuthubutu kuuza ile ardhi kutokana na historian jinsi wazee wetu walivyoteseka kupata ardhi miaka ya 1700 mpaka 1900 mwanzoni.
  • Wanaozaliwa nje ya Kilimanjaro na kurudi uchagani bila kujua historian na wale wanawake wanaoolewa uchagani wanauza na watauza ardhi kwani historian inafutika Wachaga wanajenga mbali na Kilimanjaro na wengine wanafia huko na kuzikwa huko.
  • Ukiwa uchagani sasa hivi kila ukikutana na watu kumi basi watano ni wageni
Ama kweli kila lenye mwanzo halikosi kuwa na mwisho. Binafsi nasikia uchungu sana nikitafakari mambo haya,hakuna jinsi dunia inabadilika na hakuna wa kuzuia.

Wito kwa wachaga acheni Mara moja kuwadharau wazaramo kwa kuuza mashamba na kuikimbia Dar yaleyale yanakuja kwenu na nashauri mvumilie hakuna jinsi tena ndugu zangu.
 
Ishara zote zinaonyesho miaka 30 ijayo kabila maarufu LA kichaga litafutika kabisa mkoani Kilimanjaro
Sababu kuu ni kama zifuatazo:
Wachaga wengi wanaoa na kuolewa na makabila tofauti,wengi walio oa kabila tofauti wakifa wake zao ambao ni kabila tofauti wanarithi Mali za mume zao pamoja na shamba LA urithi alilopewa Mme wake.
Watoto wengi Wachaga miaka ya sasa hivi wanazaliwa mijini na mikoani na wanakua na tatizo LA kutokujua mila na desturi za kichaga sababu hiyo inafanya wawe waswahili
Wanawake wana olewa uchagani wanaleta ndugu zao pindi wenye mji wanapokufa kama kawaida mnajua wanaume wanatangulia kufa,
Mfano mzuri ni Jirani yetu mwanamke wa kipare aliolewa kwenye ukoo wetu wa Lema baada ya mume wake kufa na wakwe zake alileta ndugu zake wengine wakaoa na kuolewa huku machame.
Wachaga halisi waliorithi Mali na mashamba kutoka kwa wazee wetu hawakuthubutu kuuza ile ardhi kutokana na historian jinsi wazee wetu walivyoteseka kupata ardhi miaka ya 1700 mpaka 1900 mwanzoni
Wanaozaliwa nje ya Kilimanjaro na kurudi uchagani bila kujua historian na wale wanawake wanao olewa uchagani wanauza na watauza ardhi kwani historian inafutika
Wachaga wanajenga mbali na Kilimanjaro na wengine wanafia huko na kuzikwa huko
Ukiwa uchagani sasa hivi kila ukikutana na watu kumi basi watano ni wageni
Ama kweli kila lenye mwanzo halikosi kuwa na mwisho
Binafsi nasikia uchungu sana nikitafakari mambo haya,hakuna jinsi dunia inabadilika na hakuna wa kuzuia.

Wito kwa wachaga acheni Mara moja kuwadharau wazaramo kwa kuuza mashamba na kuikimbia Dar,yaleyale yanakuja kwenu na nashauri mvumilie hakuna jinsi tena ndugu zangu

Hakuna na hakujawahi kuwa na kitu kama ,,Kabila la Wachaga" Dunia hii bali kilichopo ni makundi mbali mbali ya watu yaliounganishwa na Mzungu na kubatizwa jina Wachaga lkn kabla ya Mzungu kuja hao unaowaita Wachaga hawakujiita hivyo!
 
mbona hata ulaya wageni watakua wengi kuliko wenyeji wa asili yaani wazungu. hilo tatizo mbona si kwa wachaga tu ila ni kwa kabila zote au watu wote. inaelekea mtoa mada ana mind sana ukabila. angeangalia tu angeona tatizo hilo liko kwa watani zake wapare na jirani zao wamasai ambao wao tayari wamehama kwao na kusambaa nchi nzima. ni maendeleo huwezi kuzuia kwa mkono. hivi sasa juhudi zianzishwe kuhifadhi lugha za kienyeji. mijini watu waanzishe madarasa kuwafunza watoto lugha za kabila zao kwa vile asilimia kidogo sana ndio wanajua.
 
Mleta thread.. I think umevimbiwa.... Ungetuwekea na mfano wa tangia dunia ianze kuwepo ni makabila mangapi yalisha toweka?

Ungekuja kwa kusema baada ya miaka 20 ijayo Tanzania itakuwa ina robo tatu ya wazaliwa wakichina.. huku raia wazaliwa wakiwa ni robo... hapo ungesomeka....
 
Ishara zote zinaonyesho miaka 30 ijayo kabila maarufu LA kichaga litafutika kabisa mkoani Kilimanjaro
Sababu kuu ni kama zifuatazo:
Wachaga wengi wanaoa na kuolewa na makabila tofauti,wengi walio oa kabila tofauti wakifa wake zao ambao ni kabila tofauti wanarithi Mali za mume zao pamoja na shamba LA urithi alilopewa Mme wake.
Watoto wengi Wachaga miaka ya sasa hivi wanazaliwa mijini na mikoani na wanakua na tatizo LA kutokujua mila na desturi za kichaga sababu hiyo inafanya wawe waswahili
Wanawake wana olewa uchagani wanaleta ndugu zao pindi wenye mji wanapokufa kama kawaida mnajua wanaume wanatangulia kufa,
Mfano mzuri ni Jirani yetu mwanamke wa kipare aliolewa kwenye ukoo wetu wa Lema baada ya mume wake kufa na wakwe zake alileta ndugu zake wengine wakaoa na kuolewa huku machame.
Wachaga halisi waliorithi Mali na mashamba kutoka kwa wazee wetu hawakuthubutu kuuza ile ardhi kutokana na historian jinsi wazee wetu walivyoteseka kupata ardhi miaka ya 1700 mpaka 1900 mwanzoni
Wanaozaliwa nje ya Kilimanjaro na kurudi uchagani bila kujua historian na wale wanawake wanao olewa uchagani wanauza na watauza ardhi kwani historian inafutika
Wachaga wanajenga mbali na Kilimanjaro na wengine wanafia huko na kuzikwa huko
Ukiwa uchagani sasa hivi kila ukikutana na watu kumi basi watano ni wageni
Ama kweli kila lenye mwanzo halikosi kuwa na mwisho
Binafsi nasikia uchungu sana nikitafakari mambo haya,hakuna jinsi dunia inabadilika na hakuna wa kuzuia.

Wito kwa wachaga acheni Mara moja kuwadharau wazaramo kwa kuuza mashamba na kuikimbia Dar,yaleyale yanakuja kwenu na nashauri mvumilie hakuna jinsi tena ndugu zangu
Wachaga maana yake nini? Wewe fafanua ni nani unamzungumzia hapo,
Mmarangu, mkibosho, muuru, mmachame, mrombo, au muoldmoshi?

Ukija kilimanjaro uwe specific, sisi sio watu wa kujumlishwa pamoja.
Yapo mambo tunayojivunia tunapotambuliwa kwa majina yetu halisi.
 
.. hivi sasa juhudi zianzishwe kuhifadhi lugha za kienyeji. mijini watu waanzishe madarasa kuwafunza watoto lugha za kabila zao kwa vile asilimia kidogo sana ndio wanajua.
Naunga mkono wazo hili. Kuna hatari miaka ijayo lugha za asili zitatoweka na kubaki Kiswahili tu. Napendekeza kwenye Maktaba yetu ya taifa kianzishwe kitengo cha hifadhi ya lugha na waweke audio/video recordings za lugha mbali mbali na jinsi ya kujifunza lugha hizo na tamaduni zake. Vile vile serikali iruhusu uanzishwaji wa radio za kilugha mfano kichaga, kinyaturu, kingoni etc
 
Ni wachaga tu wanaotoka nje ya mkoa wao? hayo mambo yapo kwa makabila karibu yote, hata wamasai sasahivi wameacha kuchunga wamekuwa walinzi na wauza dawa za kienyeji mijini
Huyu hofu yake ni kuwa wale wazee wa zamani wanaojua kupika mbege nzuri wanaanza kutokweka kwamaana vijana wa kisasa hawataki kujifunza kupika hiyo kitu wakijifanya wasomi na kunywa kilimanjaro na tusker baridi, kwa hiyo yeye kama mdau mkuu wa mbege jambo hili linampa wakati mgumu sana.
 
Mkuu umeandika as if uchagani ni so special kama israel au kama vile sio Tanzania. Sasa mlitaka mkae wenyewe Moshi? Kiruuuuuuuu
 
Huyu hofu yake ni kuwa wale wazee wa zamani wanaojua kupika mbege nzuri wanaanza kutokweka kwamaana vijana wa kisasa hawataki kujifunza kupika hiyo kitu wakijifanya wasomi na kunywa kilimanjaro na tusker baridi, kwa hiyo yeye kama mdau mkuu wa mbege jambo hili linampa wakati mgumu sana.
Kweli mkuu
 
Ishara zote zinaonyesho miaka 30 ijayo kabila maarufu la kichaga litafutika kabisa mkoani Kilimanjaro.

Sababu kuu ni kama zifuatazo:
  • Wachaga wengi wanaoa na kuolewa na makabila tofauti,wengi walio oa kabila tofauti wakifa wake zao ambao ni kabila tofauti wanarithi Mali za mume zao pamoja na shamba LA urithi alilopewa Mme wake.
  • Watoto wengi Wachaga miaka ya sasa hivi wanazaliwa mijini na mikoani na wanakua na tatizo la kutokujua mila na desturi za kichaga sababu hiyo inafanya wawe waswahili.
  • Wanawake wana olewa uchagani wanaleta ndugu zao pindi wenye mji wanapokufa kama kawaida mnajua wanaume wanatangulia kufa. Mfano mzuri ni Jirani yetu mwanamke wa kipare aliolewa kwenye ukoo wetu wa Lema baada ya mume wake kufa na wakwe zake alileta ndugu zake wengine wakaoa na kuolewa huku machame.
  • Wachaga halisi waliorithi Mali na mashamba kutoka kwa wazee wetu hawakuthubutu kuuza ile ardhi kutokana na historian jinsi wazee wetu walivyoteseka kupata ardhi miaka ya 1700 mpaka 1900 mwanzoni.
  • Wanaozaliwa nje ya Kilimanjaro na kurudi uchagani bila kujua historian na wale wanawake wanaoolewa uchagani wanauza na watauza ardhi kwani historian inafutika Wachaga wanajenga mbali na Kilimanjaro na wengine wanafia huko na kuzikwa huko.
  • Ukiwa uchagani sasa hivi kila ukikutana na watu kumi basi watano ni wageni
Ama kweli kila lenye mwanzo halikosi kuwa na mwisho. Binafsi nasikia uchungu sana nikitafakari mambo haya,hakuna jinsi dunia inabadilika na hakuna wa kuzuia.

Wito kwa wachaga acheni Mara moja kuwadharau wazaramo kwa kuuza mashamba na kuikimbia Dar yaleyale yanakuja kwenu na nashauri mvumilie hakuna jinsi tena ndugu zangu.
Wachaga mnawaza ardhi, kuoa na kuolewa tu. Sema mmeakalia uchoyo tu, kilimanjaro yote hamuuzi ardhi yenu kama sio mchaga, mbona huko kwetu twawauzia? Acheni ukabila ndio maana hampewi nchi watu wa kaskazini
 
Back
Top Bottom