Miaka 30 ijayo kabila la kichaga kutoweka kabisa Kilimanjaro

Basi ata wachina watatoweka china maana wamesambaa duniani kote...

My take..rudi kalale uote tena hyo ndoto yako then uje na uzi unaosema
WACHAGGA TUNAKARIBIA KUITAWALA DUNIA.
 
Aki Wachagga wanaandamwa. Hakuna siku nitaingia JF nisikute thread inayowahusu wao. Ila guess what! Hawa watu wanakitu cha ziada. Mti wenye matunda ndiyo upigwa mawe
Umenena haki
 
Wote ni watanzania, na sio wachaga tu hiyo hali inawakumba makabila yote leo hii mmasai anasuka wanawake nywele salooni huko mjini.
 
Kweli uchagani kumezidi sehemu kama rombo wamejaa wasambaa na wanuaturu wanalisha mifugo na wanaoa ukouko na kuzaliana tofauti na mikoa mingne ni nadra sana kukuta makabila tofauti na wazawa vijijini
 
Fact.
 
Inauma sana
mwenyewe natafakari nabaki naumia mno
Iruwa mndumi lukabannye mbe lulasasange fo mbe maana
nyindo da baba kwifo namna fo
 
Dunia ya utandawazi hii,lengo la watandawazi ni kuvunja ukabila,udini,ukanda,na rangi ili kufanya watu wote kuwa na mira inayofanana.wachaga watahama na wageni watahamia,mbona wachaga wamejaa huku mlimba kwani huku ni marangu??
 
Mambo ya kabila niujinga mtu wote ni watanzania waswahili wabantu
 
Ni kweli kuna mabadiliko makubwa ktk jamii ya wachaga licha sikubaliani na hoja na maono ya mleta mada.

Kwanza kila desturi na tamaduni za jamii yoyote huwa zinabadilika, wapende au wasipende.
Ni jukumu la watu wa jamii yao kuhakikisha mabadiliko yanaleta matokeo chanya na siyo hasi.

Pia tamaduni na desturi tulizozikuta ktk jamii zetu ni namna wazee waliotangulia walivyoamua ku define maisha yao au walivyokubali mazingira yatengeneze desturi na tamaduni zao.

Ni jukumu letu kama kizazi kipya kutengeneza tamaduni na desturi zetu badala ya kukumbatia desturi za wazee wetu.
Swala la culture ni pana, tusichukue situations za wazee wetu na kuita culture yetu, hapana ni culture ya wazee wetu. Watu wengine wanaokota mabakuli ya mbao ya wazee wetu na kuita culture yetu, hapana ni culture ya wazee wao, tuna jukumu la ku create yakwetu.

Ktk kipindi hiki cha mageuzi makubwa duniani, jamii ya wachaga ina jukumu la kujipanga na kutafakari weakness yao na strength yao na kutumia strength yao kufunika weakness yao
 
Suala la mtu back kupewa ardhi ya urithi uchagani sijawai ona labda huko kwenu.
 
Ni wachaga tu wanaotoka nje ya mkoa wao? hayo mambo yapo kwa makabila karibu yote, hata wamasai sasahivi wameacha kuchunga wamekuwa walinzi na wauza dawa za kienyeji mijini
Sisi tunasifika kwa hilo tu mkuu?LOOH!
 
Kama ndo hivyo basi ni kwa kabila zote
 
Reactions: BAK
Aki Wachagga wanaandamwa. Hakuna siku nitaingia JF nisikute thread inayowahusu wao. Ila guess what! Hawa watu wanakitu cha ziada. Mti wenye matunda ndiyo upigwa mawe
Ni uzao wa Abrahamu
 
Hakuna na hakujawahi kuwa na kitu kama ,,Kabila la Wachaga" Dunia hii bali kilichopo ni makundi mbali mbali ya watu yaliounganishwa na Mzungu na kubatizwa jina Wachaga lkn kabla ya Mzungu kuja hao unaowaita Wachaga hawakujiita hivyo!
Ila walijiita nani? Unajua asili ya wachaga na wametokea wapi?
 
Hii ishu inaathiri makabila yote.. lakin kabila la wachaga ni kubwa.. kuna wamarangu.. machame ..kibosho.. huru, oldmoshi..

Hiyo dhana kuwa kabila la wachaga litapotea.. ni ndoto nyevu...
Haitokaa itokee ng'o.

Long live chagga.... long live kilimanjaro..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…