SautiYaMnyonge
JF-Expert Member
- May 13, 2018
- 439
- 742
Marehemu Ndugu Edward Moringe Sokoine alizaliwa tarehe 01.08.1938.
Alifariki tarehe 12 Aprili 1984 katika ajali ya gari iliyotokea katika eneo la Wami-Dakawa wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro, wakati akitoka Bungeni Dodoma kurejea jijini Dar es Salaam. Gari lake liligonga uso kwa uso na gari jingine lililokuwa likitokea Morogoro Mjini. Katika ajali hiyo, Sokoine pekee ndiye aliyepoteza maisha!
Sokoine aliwahi kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania aliyeiongoza katika kipindi kigumu sana ya kiuchumi na kuwa mwiba mkali kwa wahujumu uchumi (alitumikia nafasi ya uwaziri mkuu mara mbili 1977-1980 na 1983-1984).
Hizi ni baadhi ya nukuu za kauli zake:-
1. “Ole wake kiongozi mzembe na asiye na nidhamu nitakayemkuta: Kiongozi wa siasa hana usalama wa aina yoyote. Usalama wake ni kudra ya Mungu na Wananchi peke yake. Viongozi wazembe na wabadhirifu wahesabu siku zao. Labda tusiwajue. Hawa hatuna sababu ya kuwapa imani, kuwa tutawalinda kama vitendo vyao viovu” - 26 Machi 1983
2. “Vijana leo wengi wana mali zaidi kuliko wazee waliofanya kazi miaka thelathini hadi arobaini. Lakini wanaitaka Serikali ndiyo iwaulize mali hiyo wameipata wapi. Hivi kwa nini mzazi asimuulize mwanae, 'mali hii umeipata wapi?” - 23 Oktoba 1983
3. “Wajibu wa kila Mtanzania, kila familia na kila anayekula ni kujilisha mwenyewe. Si wajibu wa Taifa kumlisha mtu. Unaweza ukasaidiwa unapopatikana na janga. Lakini kama hakuna janga ni wajibu wa kila mtu aweze kujitosheleza kwa chakula na atoe ziada kwa Taifa” - 4 Oktoba 1983
Alikuwa kiongozi aliyejawa utaifa na uzalendo kwa nchi yake na watu wake. Tuendelee kumuombea apumzike kwa amani na kumuenzi kwa vitendo.
GALILA WABANH'U
Naibu Katibu Mkuu UVCCM Tanzania Bara na Mjumbe wa Halmashauri Kuu, CCM Taifa.
Sent using Jamii Forums mobile app