Miaka 4 ya Kwanza: Rais Magufuli - Kipimo Mara Mbili cha Ujasiri na Uthubutu

Hakuna kosa kubwa lililofanyika ile 2015 kama lile la kumsukumiza mtu ambaye hakuwa amejiandaa. Wote walioshiriki kwenye ule uharamia, watapata malipo yao hapa hapa duniani.
 
Kama kusifia vitu basi tulipaswa sana kuwasifia wazungu.
 
Ni vigumu kwa mtu yeyote anaeweka mbele utawala bora na haki kumuelewa Magufuli. Huwezi ukatenganisha maendeleo na utawala bora wenye sheria za haki. Magufuli haoni umuhimu wa haya mambo na wengi walio chini yake wako hivyo hivyo.
Enzi ya Nyerere ni tofauti kabisa na hii ya Magufuli, chini ya Nyerere alifuta vyama vingi akatupeleka hivyo hivyo cha ajabu Magufuli anajifanya ni mwana demokrasia lakini matendo yake sivyo kabisa-na dunia imebadilika hawezi kuturudisha huko kwa Nyerere.
Huwa anapenda kusema hiki hakitafanyika chini ya utawala wangu labda wakija wengine, sioni kama ana vision ya beyond Magufuli hasa kwenye utawala bora. Na kwa msimamo wako juu ya utawala bora akitokea "mkorofi" kama wasemao wao nchi hii inaweza kwenda kubaya. Haonyeshi kabisa kuwavumilia wapinzani wake hata kidogo. Amesha kutana na makundi tofauti lakini si wapinzani wake. Kwangu mimi afadhali apunzike tu 2020 tuendelee na wengine.
 
Pamoja mapambio yako yote mwanakijiji, bado magufuli atabaki kuwa Dictator wa kwanza kuongoza nchi ya wastaarabu kwa mkono wa chuma!
Aidha atakuwa wa kwanza kuua na kupoteza watu, kushambulia wapiga kura wake kwa risasi mchana kweupe. kufanya manunuzi bila bunge kuridhia pamoja na kufanya ufisadi wa kutisha ndani ya miaka minne ya utawala wake. 1.5t Atakumbukwa zaidi kwa kuwaacha watanzania wakiwa masikini wa kutupwa.
Mwanakijiji endelea tu kujipendekeza ipo siku utaukwaa utendaji wa kijiji.
 
Kwa wengine ukilitaja jina lake wanajisikia fahari na hisia ya uzalendo ambayo haijaonekana ncihni labda tangu Baba wa Taifa alipokuwa akizunguka nchini wakati wa harakati za uhuru miaka ya 1950.
You're into something right here.
 
Kutetea Magufuli kumewafanya vijana wengi wapoteze kabisa heshima kidogo walizokuwa nazo , kwa sasa si rahisi kuona madhara yake ila ngoja huyu jamaa aondoke madarakani , wengi watakimbia kwa aibu.

Huyu mtu hateteeki .
 
Pamoja mapambio yako yote mwanakijiji, bado magufuli atabaki kuwa Dictator wa kwanza kuongoza nchi ya wastaarabu kwa mkono wa chuma!
Aidha atakuwa wa kwanza kuua na kupoteza watu, kushambulia wapiga kura wake kwa risasi mchana kweupe. kufanya manunuzi bila bunge kuridhia pamoja na kufanya ufisadi wa kutisha ndani ya miaka minne ya utawala wake. 1.5t Atakumbukwa zaidi kwa kuwaacha watanzania wakiwa masikini wa kutupwa.
Mwanakijiji endelea tu kujipendekeza ipo siku utaukwaa utendaji wa kijiji.
 
Asante
 
Nimekuelewa
 
umesomeka boss
 
nyie mnataka democracy ila hamtaki wengine watumie democracy waliyo nayo
 
Kutetea Magufuli kumewafanya vijana wengi wapoteze kabisa heshima kidogo walizokuwa nazo , kwa sasa si rahisi kuona madhara yake ila ngoja huyu jamaa aondoke madarakani , wengi watakimbia kwa aibu.

Huyu mtu hateteeki .
maadam anaye kushushia heshima hakulishi aisumbui
 
kwa mtizamo wako wewe
 
siyo kila kiongozi lazima awe Kama nyerere
Na nyerere alikuwa na mapungufu msimfanye mtakatifu
 
Jibu la hapa ni takataka tu umeandika yaani rubish

ukiangalia vile alivyojiimarisha kuijenga ccm kuliko nchi halafu ndo uniambie huyo ndo raisi bora ni takataka umeandika

Kila kitu kipo hovyo sana ndani ya nchi hii
wengine tunaona kila kitu kipo na kinaenda SAWA tu
 
Kwenye makala hii sioni substance hasa unamsifu Jiwe kwa lipi zaidi ya wingi wa vibwagizo wazungu wanaita "rhetoric"

Makala nzima imejaa adjectives badala ya verbs, hii ni ishara ya kuimba mapambio na propaganda badala ya kuonyesha utendaji halisi wa Jiwe!

Weka vitu halisi kuwa Jiwe mathalani kafanya A, B, C na kutokana na hayo ndiyo maana nasema X, Y, Z. Fanya hivyo ili tuweze kuchambua kuwa je kuna uhusiano wowote wa msingi kati ya sifa unazomwaga na outcome ya matendo hayo ya Jiwe?

lakini wewe ukizungumza habari, za Sijui Jiwe kuwa eti ni kama Mwalimu, unakuwa unajaribu kubeba nyota nzuri ya mwalimu kumpachika Jiwe ambaye kwa haiba, charisma, Intellectual prowess, Political Shrewdness, Utu, Leadership skills hafikii hata theluthi moja ya uwezo mwalimu.

Kama ni Uzalendo hatujawahi kupata Rais asiye mzalendo nchi hii, Uraisi ni zaidi ya uzalendo. Uraisi ni utawala bora, kutumia kidogo tulichonacho kwa ajili ya mambo ya msingi zaidi na kwa nidhamu kubwa.

1.Mtu anayetumia pesa za umma bila kuidhinishwa na bunge
2.Mtu anayeharibu uchaguzi serikali za mitaa
3.Mtu anayenunua wapinzani na kuwatia ndani wengine kinyume cha sheria
4.Mtu anayejiweka Live yeye huku akitunyima kuona bunge Live
5.Mtu anachukua korosho za wakulima kwa mtutu wa bunduki
6.Mtu anayevunja nyumba za wananchi wakati kuna zuio la mahakama
7.Mtu anayewaambia wananchi waliopatwa na tetemeko kuwa Serikali haitotoa msaada kwa sababu siyo yenyewe iliyoleta tetemeko
8.Mtu anayewaambia watoto waliopata mimba hatowasomesha kwa sababu yeye hasomeshi wazazi
9.Mtu anayevunja katiba kuzuia shughuli halali za kisiasa wakati yeye chama chake kinafanya siasa
10. Mpaka sasa Taifa halijui yuko wapi Ben Saanane, Azory Gwanda, Kanguye, waliompiga Lissu risasi bado wapo wamejaa tele wanakula bata!

Unawezaje kusema mtu wa namna hiyo ni kiongozi mzuri hata kwenda mbali kumvisha baadhi ya sifa za mwalimu?. Mwalimu alikuwa mkali lakini alikuwa fair sana, Mwalimu maamuzi yake alijenga hoja na kushawishi umma na hata kwenda mbali kushawishi wateule wake mwenyewe wakubaliane naye! , Jiwe anatumia style ya amri za "mimi nimesema", bila kujali alichosema ndiyo best option, au bila kujali kuwa yuko within kanuni na sheria zilizopo za kuendesha mambo!

Mwalimu alijenga mifumo na taasisi, Jiwe anajijenga mwenyewe!. Hakuna taasisi za maana Jiwe anazotengeneza zaidi ya kuzipoka mamlaka zile alizozikuta, au kuzivuruga kwa amri amri badala ya kuziacha zifanye kazi kwa mujibu wa kanuni zake chukulia mfano maagizo yake kwa CAG mpya kuwa lazima atii mamlaka zilizomteua kwenye utendaji wake wa kazi kinyume cha katiba inayotaka CAG asifuate maagizo ya mtu wala idara yoyote kwenye kutekeleza majukumu yake!

Halafu katika yote hayo mambo ya ajabuajabu unatoka hapo unatwambia Jiwe ni kama Mwalimu, Sijui hii analogy unaipata wapi, hivi unamjua mwalimu wewe au unamsikia?.

Mzee unatafuta teuzi kwa nguvu?
Weka basi namba na email yako kabisa wakuone, maana kurudia yaleyale kila wakati lakini kwa lugha nyingine ni dalili za propaganda mfu!
 
Pia na yeye ipo siku atasema 1.5trillion alikula yeye na familia yake hizo tunazo jua lakini kuna kuna za nyuma ya pazia. Ukubwa wa katiba kwa rais ndio matatizo ya nchi yetu.

Tubadilike kwenye hoja ili tuweze kusaidia nchi.
Nadandia kwako, kwa sababu "bandiko refu" sina muda nalo.

Kiongozi mwenye uthubutu ni yule anayefanya mambo yake ya uongozi kwa kufuata taratibu zilizowekwa katika kuiongoza nchi. Anapokiuka na kuweka 'taratibu' anazoziamini yeye binafsi, kiongozi huyo hata kama angekuwa anafanya yote katika uongozi wake kwa nia njema, ni lazima atakuwa amepotoka.

Kiongozi, hata kama angekuwa mzuri kiasi gani, hawezi kunyang'anya "HAKI" za wananchi anaowaongoza; haki hiyo ikiwa ni pamoja na kujichagulia viongozi wao kwa hiari zao wenyewe, bila ya kuingilia taratibu zilizowekwa.

Kiongozi mzuri hawezi kuwa yeye ndiye anayejua kila kitu kizuri kinachohitajiwa kwa maendeleo ya nchi, na kuwafanya wananchi wake kama mifugo yake isiyokuwa na utashi wowote juu ya maisha yao.

Ujenzi wa 'Mavitu' mazuri, hauwezi kuwa mbadala kwa wananchi kujiamulia mwelekeo wa maendeleo ya nchi yao.

Tunayoyaona sasa hivi sio uongozi.
 
Wewe umemaliza kila kitu.
Sakata hili la uchaguzi wa serikali za mitaa na uonevu na kutokujali haki ya mwananchi kujipatia viongozi anaowataka bila kuwekewa figisu lilikuwa linatosha kumuonyesha mtu yeyote mwenye akili kuwa tuna tatizo kubwa katika uongozi wa nchi hii. Halafu unashangaa mtu anaandika limakala reefu kusifiasifia.

Ndiyo maana Afrika tunachelewa kuendelea kwa sababu wakati mwingine tunafikiri kwa mahaba na kishabiki na tunaamua kikabila huku tukisukumwa na udini na njaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…