Ni jambo la kushangaza sana ndg zangu. Kuna shule moja inaiwa Juma kisiwani, ni shule ya msingi iliyopo kata ya Katunguru Wilaya ya Sengerema Mkoa wa Mwanza. Shule hii licha ya kuwa na uhaba wa walimu pia haija wahi kuwa na mwalimu hata mmoja wa kike tangu ianzishwe 1974. Sijui wadau wa elimu wanalijua hilo au la! Kwa kuwa ajira mpya za walimu hazijatoka ni bora wadau wa elimu mko, wilaya na kata wakaliangalia hili kwa jicho pevu ili wapatikane walimu wa kike wa kupelekwa shule hii.