Ni jambo la kushangaza sana ndg zangu. Kuna shule moja inaiwa Juma kisiwani, ni shule ya msingi iliyopo kata ya Katunguru Wilaya ya Sengerema Mkoa wa Mwanza. Shule hii licha ya kuwa na uhaba wa walimu pia haija wahi kuwa na mwalimu hata mmoja wa kike tangu ianzishwe 1974. Sijui wadau wa elimu wanalijua hilo au la! Kwa kuwa ajira mpya za walimu hazijatoka ni bora wadau wa elimu mko, wilaya na kata wakaliangalia hili kwa jicho pevu ili wapatikane walimu wa kike wa kupelekwa shule hii.
Naifahamu vizuri sana hiyo shule, kuna shule moja sijui inaitwaje iko pale sengerema mjini karibu na bank ya NMB ina walimu wengi kama utitili more than 50. Serikali haiko makini kwenye mgawanyo wa walimu kati za shule za mjini na zile za pembezoni
Ipo shule pale mjini inaitwa Pambaru s/m ina walimu kila aina na kila jinsia. Kwa kweli serikali haizitendei haki baadhi ya shule. Shule yenye walimu saba haiwezi kulingana na yenye 50 hata ki ufanisi wa ufundishaji.
Naifahamu vizuri sana hiyo shule, kuna shule moja sijui inaitwaje iko pale sengerema mjini karibu na bank ya NMB ina walimu wengi kama utitili more than 50. Serikali haiko makini kwenye mgawanyo wa walimu kati za shule za mjini na zile za pembezoni
Kuna shule moja, bahati mbaya sikumbuki jina, iko maeneo ya mpakani mwa Dodoma na Kiteto, ilikuwa na waalimu 2 tu, kwa madarasa ya kwanza mpaka la saba.....Hakuna mwanafunzi aliyewahi kufaulu kwenda sekondari, toka ianzishwe mwaka 1972 (though haishangazi sana kutegemea na idadi ya hao walimu)....kama ametoka mwanafunzi basi ni ndani ya miaka 5 iliyopita....