Miaka 45 Baadaye. Wako wapi hawa?

Mwanakijiji ninavyosoma post zako unaonekana uko informed kwa mengi, siamini kwamba humfahamu Bhoke Munanka.

Si unamjua tena Mwanakijiji kawaida yake kuplay mind games. Huyu Bhoke Munanka ni mtu ambaye amekuwa hasikiki kabisa kwenye siasa siku za karibuni yaani hata watoto wake (kama anao) siwasikii kabisa ila hakuna malalamishi kuwa Nyerere ndiye amemfuta kwenye historia ya Tanzania (labda kwa sababu wote ni wa musoma).

Kuna uwezekano mkubwa kabisa wa kusahau, kutojua, au kutotaja jina la kiongozi au mmoja wa wapigania uhuru na sidhani kama ni vyema kila hili linapotokea watu walalamike au kufikiria mchezo au nia mbaya ya anayehusika.
 

Mkuu Mwanakijiji,

Heshima kwako! Nilikuwa najaribu kumsihi Gamba la Nyoka kuwa kwa mtazamo wake wa kutaka tuangalia kinachowafanya tuwaite waasisi kwa kuwachambua, basi hatutafikia lengo lako la kuwaorodhesha na kujua wako wapi sasa. Maana kila mtu anaweza kushindwa ku qualify kutokana na kutokukubalika mchango wake na wengine...pengine kwa kutokujua mchango alioutoa mhusika au kwa tofauti ya kiitikadi. Ndiyo maana nikauliza maana hasa ya neno hili la muasisis.

Lakini pengine ni vema tukaendelea kuwaorodhesha kuliko kurudishwa nyuma na watu wanaotaka credibility za waasisi kuitwa hivyo.
 

Wakuu,
Wikipedia sio mahali pa kwenda kutafuta data. Data wanazotoa huku inabidi usome mara mbili mbili na kuziangalia kwa makini. Msomi yeyote hawazi kutumia wikipedia kama source kuandika historia. Kutoa mfano mmoja, watch dog moja ilikuja gundua kwamba jamaa wa CIA walikuwa wanaandika uongo kuhusu Iran/Ahmadinajan kwenye wikipedia.
 
Kwa maoni yangu binafsi. Miaka 45 ni ya uhuru wa Tanganyika. Na kinachoneka hapa ni siasa za waliodai madaraka kutoka kwa wadhamini waliowekwa na umoja wa mataifa.

Tanganyika kama legal entity ilianzishwa baada ya ujerumani ku-saini The Treaty of Versailles (1919). Katika mkataba huu, ujerumani ilipoteza makoloni yake na mwingireza akabadilisha jina kutoka ujerumani ya afrika mashariki kuwa Tanganyika.

Kwa mtaji huo hakuna mwasisi wa Tanganyika, kwa sababu taifa lilikuwepo kabla ya wanaoitwa waasisi kuzaliwa.

Kama vile Nelson Mandela hawezi kuitwa mwasisi wa Afrika kusini, Nyerere na wenzake hawawezi kuitwa waasisi wa Tanganyika. Walichoasisi wao ni TANU.
 
KUMBU KUMBU HAFIFU........WENGI kama sio wote SIWAJUI...ok! sio vizuri11 Tuna hitaji kuwa fahamu...Tujenge shule za misingi Kwa Majina yao...
 
Bin Maryam,

uko sahihi. baada ya kuondoka Mjerumani, Tanganyika ilikuwa chini ya League of Nations. Tanganyika haikuwa koloni. Muingereza alikuwa mdhamana tu.

Inawezekana kabisa kwamba "UHURU" lisiwe neno sahihi kuelezea kilichopatikana December 9, 1961.

Mwanakijiji,

Bhoke Munanka aliwahi kuwa waziri wa mambo ya ndani ktk serikali ya Tanganyika ua Tanzania.
 
Niliwahi kusikia mambo fulani kuhusu Bhoke Mnanka, sasa Bi Maryam unaweza kunisaidia kunipa machache kuhusu huyu Bhoke Mnanka inaelekea unamfahamu vizuri tafadhali nipe data zake.

There is no BI MARYAM in this forum.
 
Mwanakijiji,
upo serious kuhubu Munanka au?

Wafuatao ndio baadhi ya wanadiplomasia wa kwanza nje ya nchi. Wao walikuwa UN:

Michael Lukumbuzya, Sebastian Chale, C.Y. Mgonja, na Erasto Mang'enya. Ninaona hawa walifanya kazi nzuri.

Chief Lukumbuzya alikuwa mmoja wa wakwanza kama sijakusea. Alipelekwa New Zealand kufanya training halafu ndio akapelekwa UN.
 
Aiseee watu wa zamani kwenye jukwaa la celeblities mlikuwa mnajadili hadi siasa?

Kina Kiba na wenzake hawakuwa maceleb?
kama ndo hivo basi mods hawakuwepo
 
Aiseee watu wa zamani kwenye jukwaa la celeblities mlikuwa mnajadili hadi siasa?

Kina Kiba na wenzake hawakuwa maceleb?
kama ndo hivo basi mods hawakuwepo
Mida hiyo mastar wa sasa wapo shule za msingi wengine mida hiyo wanajikojolea bado...dah
 
Mida hiyo mastar wa sasa wapo shule za msingi wengine mida hiyo wanajikojolea bado...dah
hapana mzee baba, mbona wakina dully misifa, prof jay, nk walikuwepo? labda mods hawakuwa active km sasa
 
Feild Masrshal ES wazee wa Sauti ya Umeme You Know Hahaha I'm Super humble.
 

Mtu sahihi unayemtaka wewe alikuwa wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…