Miaka 45 Baadaye. Wako wapi hawa?


Habari hii nilivyoisoma mimi kwa tafsiri yangu inaonyesha mambo mengi sana, baadhi tu machache tu yakiwa kama ifuatavyo:

1. Inaonyesha KAMA Kambona hakuwa muwazi sana kwa wenzake, alikuwa anajaribu kuwa-double cross. Akiwa nao anawakubalia, halafu akifika mbele ya hadhira ya kamati husika, anaamua kuwageuka

2. Alikuwa jasiri na kwamba alikuwa tayari kwa lolote

3. Mgomo wa wanaJeshi yeye akiwa kama Waziri wa Ulinzi, lazima alikuwa na taarifa za awali, ambazo alimficha Mwalimu. Huwezi ukawa waziri wa Ulinzi halafu jeshi liko mbioni kugoma, halafu wewe ukawa huna taarifa, ni uongo na haiwezekani.

4. Kitendo cha kuwatuliza wanajeshi kinaonyesha moja kwa moja kuwa anaweza kuwa alikuwa anahusika ila aliamua kutumia saikolojia ya the obvious will not be taken as the truth, the obvious will not seem the obvious!

5. Kilichokuja kuwafanya watofautiane na Mwalimu ni huo mgomo wa wanajeshi, mwalimu atakuwa alipata taarifa kamili baadaye, baada ya mgomo huo.

6. Kuhusu issue ya vijiji vya Ujamaa, Kambona hakuwa sahihi kwa sababu huwezi ukafanya Pilot Study kwa "ku-experiment na maisha HALISI ya watu", ungekuwa ni upumbavu wa hali ya juu sana. Actualy mimi naweza kusema kitu cha namna hii ni blasphemy kwa maisha ya mwanadamu na hivyo, kwa Mungu pia. Ndiyo maana madaktari wanaojifunza upasuaji huwa wanatumia vyura na panya na si Binadamu mzima, na sijui lakini ila nadhani wanapofikia hatua ya juu, pengine huwa wanatumia sanamu za binadamu ( a model of a human being), na pengine maiti, kwa kibali maalumu cha mamlaka husika ya Nchi

7. Mimi nimezaliwa na kukulia kijijini, kabla ya vijiji vya ujamaa kuanzishwa, na hivyo nayajua maisha kabla ya vijiji vya ujamaa. Watu walivyokuwa wanaishi maporini, mapori zaidi ya wanavyoishi sasa hivi wamasai huko Ngrongoro. Huu ndiyo ukweli kwa sababu kipindi hicho walikuwa aroud million 8 tu. It was a terrible kind of living ambayo haikuhitaji mtu msomi yeyote kuhitaji Pilot Study kwa ajili ya kuwanasua watu kutoka kwenye maisha ya namna hiyo, ASSUMING PILOT STUDY INGEKUWA A VIABLE WAY OF DOING IT!

8. Kambona inaonyesha kama alikuwa hayajui kabisa hata chembe, maisha ya watu waliokuwa wanaishi maisha ya kijijini kabla ya vijiji vya ujamaa, ambayo mwalimu alikuwa anataka awanasue

9.Kambona alikuwa anafanya insurbodination, kitendo cha kuwakatalia wenzake mbele ya hadhira ya kamati husika. Angekuwa na nia njema wangeweza kuwa wanazi-resolve differences zao huko halafu wanakuja kwenye kamati wakiwa na kitu kimoja. Na hii kitu ndiyo inanifanya nizidi kuamini kuwa taarifa za mgomo alikuwa anazijua

10. Kambona alikuwa sahihi kwenye jambo moja tu, la mfumo wa vyama vingi, ila inaonyesha KAMA, makubaliano yao huko nyuma kabla ya army MUTINY, ilikuwa ni kwamba wataendesha mfumo wa vyama vingi. Baada ya Jeshi kugoma, KAWAWA na Nyerere wakawa wameamua kuchukua msimamo tofauti, kwa sababu waligundua kuwa yeye alikuwa na maslahi yake binafsi, wakaamua kumziba. Kwa hiyo in a way, yeye ndiyo alisababisha mfumo wa vyama vingi usiwepo.

Ni mengi sana naweza kuchambua kutoka kwenye habari hii, sema tu muda hautoshi. Kambona mimi sikuwahi kumfahamu, zaidi ya kumuimba kwenye nyimbo za mchaka mchaka.

Mimi ushauri wangu siku zote naomba watu tuwe tunakuwa wakweli kutoka ROHONI, na ikiwezekana kabisa, pasiwepo na tofauti kati ya maneno yetu na dhamira tulizonazo rohoni. Siyo mtu unasimamia advocacy ya ukweli na uwazi halafu rohoni una kitu kingine tofauti kabisa na yale ambayo huwa unatamka siku zote.Ukifanya hivi, watu siyo wajinga watakuona tu halafu utashindwa hata namna ya kujitetea, utabaki kuandika kwenye magazeti!

Naomba niwe mkweli kabisa kutoka rohoni kwangu kwamba kwa kiasi fulani huyu mtu ameniumixza sana!
 
Army mutiny was the main cause of disagreement between these two leaders. Assuming it's true that Kambona didn't have any clue, then it's obvious that he wasn't fit for the post, Neither was he for any other post in the Government. Huwezi ukawa Waziri wa Ulinzi, Jeshi linafikia hatua linafanya mgomo huna taarifa, na wakati huo huo unaelewana nalo kiasi cha kwenda kulituliza.
 
Tungempata Bernard Membe au Lowassa 2015, sasa hivi wangekuwa na lawama kibao, halafu wale ambao tungekuwa hatukuwachagua, tuseme JPM akiwa mmoja wao, ndiyo wangekuwa sukari. Hii ni tabia ya kujikataa, kitu kibaya sana katika maisha, na nindahani ni kibaya kuliko vyote. Kwamba wewe vyote unavyokuwa navyo ni vibaya tu kwako, hakuna kizuri, halafu vilivyoko kwa wengine ndiyo vizuri! Watu waliojikataa huwa hawasababishi kitu chochote kilicho positive, na ukimkuta ana kitu positive, ujue amekwapua kutoka kwa mtu mwingine ambaye yuko positive. Aidha kwa ushirikina au kwa mabavu ya kutumia mamlaka aliyo nayo. Hawa ndiyo wanaoutusababisha wakati mwingine tunaanza kulalamika wakati mwingine hata kwenye sehemu zisizo sahihi, kwamba wanalazimisha kula hata mishahara ya watu wengine mpaka mtu anaamua kuwaachia
 
Una muchallenge mtu kwa kumvamia na kutaka kumuumiza halafu unategemea akusikilize?. Hata uwe na credible idea za namna gani siwezi kuzikubali tena, ukishaharibu trust. You pose as a friend outside while a great enemy inside, what a hell?. Kama Nchi iko mikononi mwangu, siwezi tena kukuona unafurukuta na watu wangu, piga ua!
 
Hata huko nyuma kumbe niliwahi kuchangia kwenye thread hii! Ndiyo ninauona mchango wangu hapa sasa hivi, una miaka zaidi ya 12 humu. Jaribuni kuulinganisha na michango yangu ya leo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…