w0rM
Member
- May 3, 2011
- 81
- 192
Juni 9, mwaka 1979 Kamanda aliyeongoza Vita vya Uganda dhidi ya Iddi Amin alitamka kuikamata Ngome ya mwisho ya adui. Haikupita muda Amiti Jeshi Mkuu, Julius Kambarage Nyerere akatangazia Taifa na Dunia kuwa ngome ya mwisho ya adui imeanguka.
Ikiwa ni miaka 45 sasa tangu ushindi wa Vita hii. Je, tunawakumbuka na kuwaenzi vipi Mashujaa wetu wa Vita hii? Wapo walio hai hadi sasa!
Wenzetu Mataifa yaliyoendelea yanawaheshimu sana Mashujaa na Veterans wao. Mwezi huu Uingereza, Marekani, Canada na Ufaransa wanasherekea miaka 80 ya Wanajeshi wao waliopigana Kijasiri pale ufukwe wa Normandy (Ufaransa) wakitokea English Channel. Jumla ya Askari 150,000 walivuka na kuwakomesha Wajerumani na Waitaliano.
Mwaka 1978 - 1979 Tanzania kupitia kwa Jeshi la Wananchi (JWTZ) iliingia katika vita yake ya kwanza kutetea mipaka yake dhidi ya majeshi ya Idd Amin. Ushiriki wa JWTZ katika mapambano hayo ulikuwa wa Kiukombozi zaidi.
Tarehe 25/7 kila mwaka ni siku ya Mashujaa ambapo hufanyika kumbukizi kwa gwaride na vitu vingine. Imekuwa hivyo tangu tupate uhuru. Mstari wa mbele wanapitishwa waliopigana vita Kuu ya pili. Je, kwanini Mashujaa (Wanajeshi) waliopigana katika Vita vya Uganda na kuleta ushindi hawajawahi kutajwa katika sherehe hizo?
Hawa Wanajeshi waliopo hai na waliofariki tunawathamini na kuwaenzi kwa namna gani?
Soma:
- Historia ya Vita ya Kagera 1978-1979
- Waziri Dkt. Stergomena Tax: Maveterani waliopigana vita ya kagera wameshalipwa, hakuna anayedai
- DOKEZO - Rais Samia, Watumishi Wastaafu wa Jeshi tunaomba utusaidie kupata stahiki zetu, tunateseka
- Vilio vya Wastaafu wa majeshi vitatuliwe haraka, kinachoendelea ipo siku kitatengeneza ‘matunda yasiyofaa’
- Waziri Tax: Hakuna malimbikizo kwa wastaafu wanaohusiana na JWTZ