Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Mbarali kupitia Jumuiya ya umoja wa wanawake Tanzania UWT, imefanya maadhimisho ya miaka 48 ya chama Cha mapinduzi kwa kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na serikali wilayani humo, ikiwemo miradi ya maji, Afya na Umwagiliaji.
Katika maadhimisho hayo mbunge wa jimbo la Mbarali Mhe. Bahati Ndingo, amesema serikali ya awamu ya sita inayoundwa na chama cha mapinduzi ikiongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, inatekeleza miradi mbali ili kusaidia wananchi ikiwemo miradi ya maji pamoja kujenga skimu za umwagiliaji ili kuinua kilimo kinachofanywa na wananchi wa wilaya hiyo cha mpunga.
Soma Pia:
Pamoja na kutembelea miradi hiyo ya maendeleo mbunge Mhe. Bahati Ndingo pamona viongozi wa UWT wilaya ya Mbarali wametoa mahitaji kwa wanafunzi 27 wenye mahitaji kwenye shule ya msingi Igomelo, zoezi lililoenda sambamba na kukabidhi Mitungi ya gesi kwa mamantilie 100 kwa lengo la kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt, Samia Suluhu Hassan kuhamasisha matumizi ya nishati Safi kupikia na kulinda mazingira.