Miaka 5 ya CCM #Pambana Na Hali Yako

Umefika wakati ambapo badala ya CCM kuwaghilibu na kuwanunua vichwa vilivyopo ndani ya vyama vya upinzani ili kuziba pengo lililopo ndani yake la watu walio makini, werevu na wenye uelewa wa hali ya juu ktk fani mbalimbali.

Na pia imefika wakati, ambapo badala ya CCM kuwaundia kila aina ya zengwe watu wenye akili kubwa waliopo ndani ya vyama vya upinzani, ili wakose ufanisi ktk kuwatumikia Watanzania. Nashauri waje na hoja ya kuunda serikali ya ymoja wa kitaifa nchini, ili waweze kutumia vipaji hivi kwa uhuru.

Kongole zako Mh. Zitto kwa hoja murua kabisa za kiuchumi ktk kuzichambua vyema bajeti za serikali za 2016/17 kuelekea 2020/21 na kuyaweka hadharani mapungufu yake. Tena ukizingatia uwasilishaji wa bajeti ya mwaka huu ilikuwa ni sehemu kama ya ibada kwa kuonyesha sifa na kuabudu kwa yeye yule aketiye ktk kiti cha enzi hapa nchini.
 
Ningependekeza wanafunzi waanze kufundishwa IT kuanzia shule ya msingi. Shule ipate computer hata tano, iwe na WiFi, kuwe na mwalimu mwenye taaluma hiyo.

Dunia ya sasa ni kidigital mtoto anamaliza darasa la saba hajui hata kujaza fomu kwa kidigital.

Watoto wafundishwe Machine Learning.
 
Ni ndefu lakini nimesoma mpaka mwisho kwa sababu ina mvuto fulani na kwa hiyo kila hatua ya kusoma kwangu, nafsi ilinianbia endelea mbele zaidi, mwisho nikamaliza.....

Ni mpango mzuri sana. Na ni ukweli kuwa CCM wamechoka, hawana kitu kipya cha kuifanyia Tanzania kwa sasa. Wako hapo kujilinda, wanaogopa kuachia madaraka, wanaogopa kuliwa vichwa vyao kwa sababu ya dhambi na maovu yao waliyowatendea watanzania.....

Wanaelewa fika kuwa, "MSHAHARA WA DHAMBI/MAOVU NI MAUTI". Wanaiogopa mauti yao waliyoiumba/tengeneza wenyewe....!!

Ni kwamba wanajua kabisa kuwa wameshindwa, hawapendwi, hawakubaliki na hawatakiwi kuiongoza Tanzania kwa lolote....

Lakini bahati mbaya ni kuwa wamejiandaa kutokabidhi nchi kwa mtawala mpya, wako tayari kumwaga damu ili mradi wabaki madarakani....

The best way hawa ni kukabiliana nao kwa njia hiyo hiyo wanayoitaka, kuwachapa makofi tu mpaka washike adabu na wakimbie wenyewe....

Hii inawezekana, tumechoka kuongozwa na nguvu za kuzimu.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…