Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Wanamajlis,
Itakapofika 12 Oktoba itakuwa miaka miaka 50 toka Abdulwahid Sykes kufariki.
Huu ni wakati mzuri kufanya tathmini ya historia ya uhuru wa Tanganyika kwa lau
kwa ufupi kumkumbuka yeye na wazalendo wenzake wake kwa waume waliokuwa
pamoja na yeye miaka ile ya 1950 wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika.
Aisha ‘’Daisy’’ Sykes Buruku ni binti ya Abdulwahid Sykes mmoja kati ya watu 17 waliounda chama cha TANU kilichopigania uhuru wa Tanganyika.
Daisy kama anavyofahamika zaidi kwa jina hili, ni msichana wa kwanza Mwafrika kusoma Shule ya Wasichana ya Aga Khan mwanzoni mwa miaka ya 1950 na msichana wa pili kuingia Chuo Kikuu Cha Afrika ya Mashariki, Dar es Salaam
mwishoni mwa miaka ya 1960.
Daisy amefahamiana na wazalendo wengi mmoja wapo akiwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na machifu mashuhuri kama Mangi Mkuu Thomas Marealle, Mwami Theresa Ntare waliokuwa wakifika nyumbani kwa
baba yake wakati wa harakatiza kupigania uhuru wa Tanganyika.
Katika kuadhimisha miaka 50 ya kifo cha baba yake, Daisy ameandika makala kukumbuka siku zile zilizojenga haiba ya baba yake na ya wazalendo walioshiriki katika kupigania uhuru wa Tanganyika.
Makala haya itawekwa hapa JF kuadhimisha kumbukumbu ya kifo cha baba yake tarehe 12 Oktoba, 1968.
Kwa miaka mingi Daisy amekuwa akiishi na kufanya kazi nje ya Tanzania.