Miaka 51 ya uhuru na elimu bora nchini Tanzania

Miaka 51 ya uhuru na elimu bora nchini Tanzania

Baba mtata

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2012
Posts
280
Reaction score
40
Heshima wakuu!!
Katika kuadhimisha miaka 51 ya uhuru kuna mafanikio gani na changamoto gani katika kuiendeleza elimu bora nchini Tanzania?
Nawasilisha
 
Kama tunataka kufikia nchi za far east zilikofikia, na hata nchi kama Turkey ambayo ingawa kuna mdodoro wa uchumi nchi za ulaya, yenyewe uchumi unaendelea kukua kwa kasi, lazima tuwekeze kwenye elimu bora.Elimu yetu bado ni ya mashaka mashaka...tuanze kuitazama upya elimu kuanzia chini mpaka ya juu kabisa.
 
Ni aibu miaka yote hii 51 kati ya watu 100, 57 hawajui kusoma na kuandika,

Leo waalimu wa digrii ya elimu mshahara wake ni sawa na mtu certificate ya uuguzi, je? Kiwango cha elimu kitapanda vip? Acha watoto waburutwe tu walimu wanafundisha private schools vizuri wenye kujali mchango wao! Na gvt wanalishwa matango poli.

Mpende akupendaye asiyekupenda achana nae!
 
Heshima wakuu!!
Katika kuadhimisha miaka 51 ya uhuru kuna mafanikio gani na changamoto gani katika kuiendeleza elimu bora nchini Tanzania?
Nawasilisha
dah mafanikio katika elimu??? kusema kweli mimi ninawapongeza sana kwa pepa ya form six mwaka huu japo ilivuja ila ilikua kwenyestandard....sasa ukija kwengine ni uozo mtupu!! matokeo ya darasa la saba,mitihani kuvuja,board ya mikopo na matatizo yake mengi tu,tcu ndo uozo kabisa,mtihani wa kuchagua majibu katika somo la hisabati(std 7) ni aibu.....GENERALLY NOTHING NEW!
 
Ni kwel kwamba kama mtoto anaweza kuhtimu Darasa la saba na kuingia sekondar akiwa hajui kusoma wala kuandika, mfumo wa elimu unahtaji tathimimi kubwa. Kikubwa ninacho kiona tofauti na maslah Dun ya waalimu, nchi haina Dira! Hatuna farsafa kama taifa. Hatuna itikadi ya nchi. Miaka hyo 51 tunasherekea Taifa lililokwisha chakachuliwa. Tunaongelea Tanganyika? Iko wapi? Rais wa hyo jamhur ya tanganyika n nan? Ok kwa kukosa Dira kama taifa inapelekea pia kukosa Farsafa ya Elimu.
 
yapo maswali ya kujiuliza ili kuiona tz mpya yenye elimu itakayolipeleka Taifa la tz mahala pema zaidi
  • Je elimu yetu ni kwa ajili ya ya kufaulu mtihani ama kumtayarisha mtanzania bora ili ajitumikie na kulitumikia taifa?
  • je elimu yetu ina uwiano katika utolewaji na ubora ili kutengeneza Taifa moja la Tanzania?
  • Je uwekezaji ktk elimu ni kwa ajili ya mustakabali mwema wa Taifa ama matumbo binafsi ya watu?
tafakari nami!
 
Back
Top Bottom