Miaka 58 ya Uhuru wa Tanganyika: Uhuru una maana gani leo?

Tufupishe maneno umoja wakitaifa chini yake umepotea sasa watu tunaangaliana kwa ukabila na udini.
 
Kama umezaliwa Tanzania na hujawahi ishi Sehemu za majanga kama Somalia, ni rahisi kuandika haya anaandika Mhe Zitto. Mnao dhani hatuko huru kawaulizeni Libya nini kinawapata Baada ya kutamani Vurugu.
heri ya siku ya uhuru
Jifunze kuwa na ufaham ina mana huwoni yanayo tokea? Nahumjuwi mwanzilishi wa haya
 
Hahaha bwana Zitto mjanja sana kwenye uandishi wake

Amekwepa maswali Mengi ambayo nilitaka nimtandike

Ila siuna ona Rais Magufuli anavyochapa kazi?

Tumpongeze Rais kwa kutumia vizuri raslimali za Nchi yetu kujenga uchumi
 
Uhuru umegeuka laana ya CCM kulazimisha kutawala milele hii nchi.
 
Huyu kijana amebaki kuwa mbunge wa Twitter
Amewatelekeza kabisa Wananchi wa kigoma

Wanakigoma wanajuta
 
Zitto huaminiki wewe. Uliwageuka wenzio kipindi cha JK Kwa ajili ya tumbo lako. Leo nchi imenyooshwa halafu unakuja na porojo za kijinga.
Upepo umebadilika dogo utakufa njaa subiri 2020 unyang'anywe na Ubunge ndio utajua unafiki sio mzuri.
JPM alikushtukia mapema.
 
Reactions: PNC
Hahaha bwana Zitto mjanja sana kwenye uandishi wake

Amekwepa maswali Mengi ambayo nilitaka nimtandike

Ila siuna ona Rais Magufuli anavyochapa kazi?

Tumpongeze Rais kwa kutumia vizuri raslimali za Nchi yetu kujenga uchumi
Tunatofautiana katika uelewa, nani kasema Magufuli hafanyi kazi? Nani kasema ni goigoi? Hakuna aliyesema hivyo. Lakini kama nchi, INA katiba,sheria,kanuni na tamaduni zake na zipo ili zifuatwe. Jee anazifuata? Kama hafuati HATUFAI hata kidogo.
Utawala wa sheria haufwatwi, demokrasia inasiginwa na mihimili mingine katumia mabavu kuikandamiza hivyo check and balance hakuna. Kwa nini tukubali? Maendeleo kama ya Libya ya kupata lakini nchi inakandamizwa na MTU mmoja na hakuna Uhuru hatuyataki maana mwisho wake ni vita na mateso.
Mbona nchi kama Botswana maendeleo yanaonekana huku katiba na sheria zinaheshimiwa? One man show hatutaki kabisa maana haina hatma nzuri kwa nchi na hata kwa watawala wenyewe na reference zipo nyingi tuu.
Ni rais wetu tayari tutampenda na kumuunga mkono mpaka amalize kipindi chake kama ata heshimu Katiba na sheria, atajali mawazo kinzani, ataheshimu utu wa watu kwenye nchi yao, atakiheshimu kiti tulicho mpa akalie (maana sio chake ndio maana alikiomba kwa kupiga hadi pushup) na aache ukatili dhidi ya RAIA wenye nchi yao.
 
sisi watanzania tunaelewa maana ya uhuru lakini wewe kila kukicha unajipendekeza kwa mabeberu ili wakusaidie kupata urais, tunajua njaa yako ya Ikulu lakini kumbuka Ikulu ni mahali patakatifu wezi kama nyie mtapasikia tuu
 
Kama umezaliwa Tanzania na hujawahi ishi Sehemu za majanga kama Somalia, ni rahisi kuandika haya anaandika Mhe Zitto. Mnao dhani hatuko huru kawaulizeni Libya nini kinawapata Baada ya kutamani Vurugu.
heri ya siku ya uhuru
Nakiona kitambi cha wadhifa
 
Tukipata watanzania kama wewe nchi itazidi kuwa maskini na dhaifu, nakuona km umekuja kudai demokrasia ya mikutano sisi tunawaza maendeleo na sasa nchi inajengwa

History inaoesha tangu mfumo wa vyama vingi ndio uchumi ulianza kuyumba


USSR

Wakati Nyerere anatoka madarakanu huku wananchi wakiwa wanavaa viraka, nchi ilikuwa ya vyama vingi? Kama huna hoja piga kimya dogo.
 
Kama umezaliwa Tanzania na hujawahi ishi Sehemu za majanga kama Somalia, ni rahisi kuandika haya anaandika Mhe Zitto. Mnao dhani hatuko huru kawaulizeni Libya nini kinawapata Baada ya kutamani Vurugu.
heri ya siku ya uhuru

Tofautisha kuwa huru na kuwa kwenye vita. Kutokuwa na mapigano sio tafsiri ya kuwa huru. Kwani Somalia na Libya sio nchi huru? Jifunze maana ya kuwa huru kisha uje uchangie.
 
Tukipata watanzania kama wewe nchi itazidi kuwa maskini na dhaifu, nakuona km umekuja kudai demokrasia ya mikutano sisi tunawaza maendeleo na sasa nchi inajengwa

History inaoesha tangu mfumo wa vyama vingi ndio uchumi ulianza kuyumba


USSR

Kumbe! Kwa hiyo tunarejeshwa kwenye chama kimoja ili uchumi uimarike? You must be clueless; au pengine umri wako mdogo sana. Kwa taarifa yako wakati tunaingia uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi 1995 nchi hii ilikuwa imepiga magoti kiuchumi; hoi kabisa. Miaka kumi baadaye, mwaka 2005 kila Mtanzania alitembea kifua mbele. Uchumi umeimarika sana na ingawa demokrasia ya vyama vingi ilikuwa bado changa uongozi uliithamini wakijua ndio ufunguo wa maendeleo.
 
Tukipata watanzania kama wewe nchi itazidi kuwa maskini na dhaifu, nakuona km umekuja kudai demokrasia ya mikutano sisi tunawaza maendeleo na sasa nchi inajengwa

History inaoesha tangu mfumo wa vyama vingi ndio uchumi ulianza kuyumba


USSR
Mimi wala vyama vingi havinipi shida; kinachonipa shida ni Uhuru na Haki.
Maendeleo ya nchi hayazuiwi na mimi kuwa na Uhuru na Haki yangu ya kiutu.
Lakini najua kwa watu waliosinyaa ubongo kama wewe huwezi kuyaelewa haya.
 
Ubaya haulipwi kwa Ubaya
Hekima na Busara ndio silaha
Tusilazimishe machafuko ndio tuseme tumekombolewa
Walichokifanya Chadema ni zaidi ya ufahamu wa watu mia
Sasa mlitaka kifanyike nini?
Mbona ninyi kama viongozi mnaishia kuandikaaaaa weeeee
Mbowe ameuwa ndege kumi kwa jiwe moja


Mtawala si mnamjua akigeuka hiyo u turn yake mtasimulia
*lets give this a chance tuone labda mkulu ataelewa
Kwani nyie mlitakaje?
Tuingie porini au!
 
Nimeahirisha kusoma baada ya kuona mwandishi wa makala hizi.
Akili zangu nazijua mwenyewe hahahahaahahaaaaaaaah...
 
Zitto mnafiki sana. Wakati wenzake upinzani wanagoma hotuba ya kwanza ya rais bungeni yeye na kiherehere alikuwapo bungeni. Leo wenzake wanaenda ktk maadhimisho povu lamtoka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…