DOKEZO Miaka 60 ya Jeshi la Wananchi pasipo suluhisho kwa wazee wetu waliopigana Vita ya Kagera

DOKEZO Miaka 60 ya Jeshi la Wananchi pasipo suluhisho kwa wazee wetu waliopigana Vita ya Kagera

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Leo tumeshuhudia miaka 60 ya jeshi letu, tumefurahi, tumekunywa na tumekula. Hongereni sana.

Changamoto yangu katika jeshi letu limewasahau wazee wetu waliopigana vita vya Kagera pasipo kuwapa japo kifutia jasho cha vita. Leo wazee wetu hawana hata shughuli za kufanya zaidi ya kusubiri kifo tu.

Mara kadhaa wameitwa wanachukuliwa taarifa hakuna lolote linalaoendelea wanarudi tena wanawachukua taarifa wanaondoka ndivyo wanavyofanya kila wakati. Je, wanasubiri hawa wazee wafariki wote? Na hizo pesa zao nani azitumia na ni haki zao?

Natoa ushuhuda huu kwani mzee wangu ni muhanga wa tatizo hili.

Naombeni msaada wenu kwani kaishazunguka sana pasipo mafanikio yoyote. Na hili litawasaidia na wale wasiokuwa na sauti.

Pia soma:
 
Vita yenyewe haikuwa na sababu ya msingi shida ilianzia hapo. Mzee alipigana vita sasa hivi pesa zinanunua v8 na kuwalipa machawa
 
Back
Top Bottom