Miaka 60 ya uhuru wa Tanganyika 1961: John Rupia na Julius Nyerere

Miaka 60 ya uhuru wa Tanganyika 1961: John Rupia na Julius Nyerere

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
MIAKA 60 YA UHURU WA TANGANYIKA: JOHN RUPIA SIKU ZOTE ALIKUWA PEMBENI YA JULIUS NYERERE

Shughuli ilikuwa fupi.

Waandaaji wa hafla siku hizi wamekuwa makini sana kwa muda.

Hupenda kuzipeleka ratiba mbio ili watu wakafanye mambo yao mengine.

Tulikuwa tumefikia karibu ya kufunga ghafla Joyce ananiomba nimzungumze Mzee John Rupia.

Nikamwambia kuwa sikujitayarisha kuzungumza.

"Sikutaka ujitayarishe nilitaka umzungumze John Rupia kama umjuavyo.''

Nilizungumza maneno machache kwa kuwagutusha wanahistoria kumtazama vizuri Mzee John Rupia kwa sura yake nyingine ya mtu wa fikra.

Wasimtazame John Rupia kama anavyoelezwa kuwa alikuwa mfadhili wa TANU tu.

Wamtazame John Rupia kutokea mwaka wa 1950 alipokuwa mjumbe ndani ya TAA Political Subcommittee akiwaunga mkono vijana wanamapinduzi walioigeuza TAA kuwa chama cha siasa bila ya katiba ya siasa.

Nilipomaliza kuzungumza wajukuu wa John Rupia na watu wengine wakawa wananifata wakati wa chai kutaka niwaeleze zaidi kuhusu mzalendo huyu.

Nilikuwa nikiwachekesha wajukuu wa Mzee Rupia kwa kuwaambia kuwa wasidhani babu yao alikuwa "Sanduku la Fedha."

Niliwaambia kuwa John Rupia alikuwa na mchango mkubwa wa fikra mbali ya uwezo wa mali.

Niliwaambia kuwa kama vile alivyoendesha makampuni yake kwa ufanisi ni hivyo hivyo ndivyo alivyoisaidia TANU kufanikiwa na kuwa chama imara.

Niliwaeleza kuwa sahihi yake ipo katika nyaraka muhimu sana ya Mapendekezo ya Katiba yaliyopeleka kwa Gavana Edward Twining mwaka wa 1950.

Mapendekezo haya yalijadiliwa kwenye mkutano wa TAA wa 1954 uliounda TANU na ni sehemu ya hotuba aliyotoa Julius Nyerere UNO mwaka wa 1955.
 
Shukrani mwandishi.
Kuipata historia ya wapigania uhuru hawa inakuwa mtihani mgumu sana.
 
Historia ni mwalimu mzuri sana maana tunapata kuwafahamu waasisi wa taifa hili kiundani zaidi. Ubarikiwe sana mkuu.
 
Aisee Mzee shukrani unatutendea haki sisi wajukuu zako,nilikua nasikia Kwa wazee flani wakimhadithia huyo John Lupia ya Kwamba Ndio alikua Moja ya watu weusi matajiri sana hapa Tanganyika Miaka hiyo ya ukoloni,wengine ni kina
Aziz Ally & family,kina Sykes & family na wengineo wajanja wa enzi hizo
Ila katika kitu kinachonisikitisha na kuona Kuna watu hawana shukrani ni jinsi mwisho wa Dosa Aziz Ally ulivyokuwa mbaya yaani Mtu alietoa Mali zake za thamani kama majengo magari kama Benz na voskwagen za gharama kuzunguka nchi nzima kuhamasisha watu wajiunge na TANU mwisho
Anafia kwenye nyumba ya udongo na makuti huko mlandizi daaaaa iliniuma sana rafiki uliekua unamthamini Kwa Hali na Mali anakudump kisa kakalia ikulu na Bata zote anapiga anasahau alikotokea!
Anyway sio kesi just memory tu!
 
Back
Top Bottom