Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
MIAKA 60 YA UHURU WA TANGANYIKA 1961: HOTUBA YA KUPANDISHA BENDERA YA TANGANYIKA LINDI SOUTHERN PROVINCE ILISOMWA KUNUT
Leo ukieleza kuwa mikutano ya TANU ilikuwa ikifunguliwa kwa dua na ikifungwa kwa dua na unaweza ukazusha ubishi mkubwa sana.
Halikadhalika ukisema kuwa usiku wa tarehe 8 kuamkia tarehe 9 Desemba 1961 bendera ya Tanganyika ilipopanda Lindi Southern Province iisomwa kunut katika hotuba ya kupokea uhuru utasababisha malumbano yenye hisia kali.
Lakini ukweli ni kuwa huko ndiko walikotokea wazee wetu katika harakazi za kupigania uhuru wa Tanganyika.
Hapa kuna ihistoria ya kusisimua kidogo kwa nini hotuba ya kupokea uhuru Uwanja wa Gofu Lindi ilisomwa kunut?
Wakati wanaanza pilikapilika za kuunda TANU Lindi mwaka wa 1955 tayari Mwalimu Nyerere alikuwa keshakwenda UNO safari ya kwanza na kurudi.
Kuanzia kipindi hicho TANU ikaanza kujulikana kote Tanganyika na taratibu kupata nguvu.
Masudi Mnonji na vijana wake Salum Mpunga walikuwa wanakwenda huku na huko kueneza TANU wakijaribu kufungua matawi lakini kulikuwa na kizingiti kikubwa kilichokuwa kinawakabili.
Jimbo la Kusini Kanisa lilikuwa likiwatahadharisha na kuwaonya waumuni wake wasijiunge na TANU kwa kuwa hizo ni harakati nyingine za kutaka kuzusha vita vingine vya Maji Maji safari hii dhidi ya Waingereza.
Watu wa kusini wote walikuwa wanajua yaliyowafika wazee wao waliposimama na kunyanyua silaha dhidi ya Wajerumani.
Kumbukumbu na athari ya vita vile vilikuwa wazi kwani Maji Maji na TANU vilipishana kwa miaka 50 tu.
Vita vilianza mwaka wa 1905 na kumalizika mwaka wa 1907 na Wajerumani waliwanyonga hadharani majemedari wanaofikia 60 na zaidi kidogo na kuwazika katika kaburi moja la halaiki isipokuwa Abdulrauf Songea Mbano yeye kaburi lake liko peke yake.
Hiki ni kisa kingine.
Wamishionari waliwaonya waumini wao kujiweka mbali na TANU yasije yakawafika yaliyowafika hata wanawake waliopigana dhidi ya Wajerumani kama Bi. Khadija Mkomanile.
Bi. Khadija Mkomanile ndiyo mwanamke pekee aliyenyongwa katika Vita Vya Maji Maji.
Kwa ajili hii basi ilibidi utumwe ujumbe maalum kutoka Lindi kwenda Dar es Salaam Makao Makuu ya TANU New Street ili kuomba Rais wa TANU Julius Nyerere afike Lindi kupambana na propaganda hii ambayo ilikuwa kwa hakika inaviza juhudi zote za kuijenga TANU Southern Province yote.
Salum Mpunga na Ali Ibrahim Mnjawale wakatumwa kwenda Dar es Salaam kueleza tatizo hili na kumtaka Mwalimu Nyerere afanye ziara ya Lindi ili kupambana na propaganda hii.
TANU Makao Makuu iliitika mwito huu na Mwalimu Nyerere akiongozana na Ali Mwinyi Tambwe na Rajab Diwani walifunga safari ya Lindi na wakafanya mikutano mikubwa sana Lindi, Mikindani na kwengineko.
Mwalimu Nyerere alipoondoka Southern Province kurejea Dar es Salaam aliicha TANU katika hali nzuri na wananachi wakajua kuwa TANU haikuundwa kuhamasisha vita bali inadai uhuru wa Tanganyika kwa njia ya amani.
Sasa usiku wa kuamkia tarehe 9 December siku ya uhuru umma wa wananchi waliohudhuria sherehe ya uhuru Uwanja wa Gofu walimsikia kijana Yusuph Chembera akisoma hotuba ya kupokea uhuru mbele ya DC hotuba iliyoandikwa na mwalimu wake aliyemsomesha Qur'an udogoni, Sheikh Yusuf Badi.
Yusuf Chembera alisoma kunut na uwanja mzima uliitikia mwalimu na sheikh wake Sheikh Yusuf Badi wakiwa kati ya waliohudhuria sherehe ile.
Sheikh Yusuf Badi haikumpitikia hata siku moja kama itakuja siku mtotoa liyemsomesha mwenyewe siku moja atasimama mbele ya hadhara kubwa kupokea uhuru na kusoma hotuba ambayo ataiandika yeye.
Sheikh Yusuf Badi aliingizwa katika TANU na Yusuf Chembera na Salum Mpunga wote wanafunzi wake walipokuwa wadogo.
Kuingia kwa Sheikh Yusuf Badi katika TANU kuliipa TANU nguvu kubwa sana kwani Sheikh Badi alikuwa kati ya wanazuoni wakubwa Tanganyika.
Nilipozungumza na Yusuf Chembera kuhusu siku hii nakumbuka ilikuwa mwezi wa Ramadhani niko nyumbani kwake asubuhi tu baada ya Fajr.
Yusuf Chebera alisema, ''Siku ile ya uhuru ilikuwa siku kubwa kwetu kwani historia ya TANU ilikutana na vikwazo vikubwa hakuna aliyetegemea kuwa TANU itapata nguvu na wale waliokuwa wanatisha wananchi wasijiunge na sisi kwani tulikuwa tunatayarisha Maji Maji nyingine walikuwapo Uwanja wa Gofu kupokea uhuru.''
Mji wa Lindi umempa Sheikh Yusuf Badi mtaa kwa ajili ya mchango wake katika kupigania uhuru wa Tanganyika.
Picha ya kwanza gazeti la Uhuru 9 December 1961, Mtaa wa Sheikh Yusuf Badi Yusuf Chembera na Salum Mpunga.