Miaka 60 ya Uhuru wa Tanganyika 1961: Zarula Bint Abdulrahman wa Tabora

Miaka 60 ya Uhuru wa Tanganyika 1961: Zarula Bint Abdulrahman wa Tabora

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
MIAKA 60 YA UHURU WA TANGANYIKA 1961: BI. ZARULA BINT ABDULRAHMAN WA TABORA

Nimekuwa kwa miaka mingi nikitafuta picha ya Bi. Zarula bint Abdulrahman wa Tabora mwanamama ambae alikuwa mstari wa mbele katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Kama nisingemtaja jina lake katika kitabu cha Abdul Sykes pengine asingefahamika na historia yake ingepotea.

Ilikuwa katika kuandika historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika mitandaoni ndipo mwanae akasoma jina la mama yake.

Aliniandikia pembeni na akanifahamisha kuwa Bi. Zarula ni mama yake.

Namweka hapa chini Bi. Zarula kama nilivyomwandika katika kitabu cha Abdul Sykes:

''Waliounganisha na kuviongoza vyama vya wanawake na harakati za kudai uhuru Dar es Saaam walikuwa Bibi Titi Mohamed na bibi mmoja wa Kimanyema, Hawa binti Maftah.

Bibi Hawa bint Maftah, kama kiongozi wa lelemama, alijulikana kwa jina la ''Queen.''

Hakuna hata mtu mmoja Tanganyika nzima, mbali na Nyerere mwenyewe, aliyeweza kuifanya TANU kuwa maarufu kama Bibi Titi Mohamed.

Bibi Hawa Maftah ndiye aliyeiingiza kwa mara ya kwanza nyimbo za lelemama ziimbwe katika mikutano ya TANU kama mbinu ya kuhamasisha wananchi kukipenda chama.

Tabora vyama vya wanawake vilikuwapo - Nujum ul Azhar, Waridatil Hubb na Egyptian Club vilivyokuwapo chini ya uongozi wa Bi. Nyange bint Chande na Bi. Zarula bint Abdulrahman.

Vyama hivi vya akina mama vilisaidia sana kuipa TANU nguvu katika Jimbo la Magharibi.

Muziki na ujumbe katika nyimbo zilizotungwa maalum kuinua mioyo ya wanachama wa TANU vilikuwa na athari kubwa, hususani katika wakati ule ambapo serikali ya kikoloni ilimpiga marufuku Nyerere kufanya mikutano ya hadhara.

Ili kuepuka kadhia hiyo TANU ilikuwa ikiandaa taarab na Nyerere alikuwa akikaribishwa kama mgeni wa heshima.

Nyerere alikuwa akisimama kufungua hafla na katika kufanya hivyo alisema maneno machache.

Kwa namna hii ule moto wa kudai uhuru ulibaki ukiwaka. Kwa njia hii Nyerere aliweza kuwasiliana na wananchi.

Halikadhalika kupitia taarab TANU ilikusanya fedha kwa ajili ya harakati.

Bi. Nyange bint Chande, mwanachama wa moja ya vikundi vya lelemama mjini Tabora alijitolea nyumba yake kama ofisi ya kwanza ya TANU katika Jimbo la Magharibi.

Amani Idd alikuwa muuza kadi za TANU na baadae alisaidiwa kazi hiyo ya kuuza kadi za TANU na Zarula bint Abdulrahman.

Bi. Zarula alikuwa mmoja wa wajumbe wa Tabora katika mkutano wa Kura Tatu."

Leo asubuhi nimepokea picha Bi. Zarula bint Abdulrahman na ndiyo hii nimeiweka hapa.

Mwanae kaandika maneno hayo hapo chini:

"Zarula bint Abdulrahman wa Tabora aliyesahaulika katika Chama ambae ndio alikuwa muhamasishaji mkubwa Tabora na ndio alikuwa akiandika kadi za Chama kwa kina mama kwa uficho.''

May be an image of 1 person and standing
 
Ahsante Sheikh Mohammed kwa kutuhabarisha kuhusu huyu mama kwa jina la Bi Zarula binti Abdirrahman.

Samahani naomba kuuliza kwa kujielimisha: hivi vyama vyengine vya wanawake vyenye majina ya kiarabu vilikuwa navyo vi vya lelemama?
Pia nilikuwa sifahamu kwamba ngoma ya lelemama kumbe asili yake ni Wamanyema. Visiwani Unguja na Pemba ni ngoma maarufu sana (pamoja na ile ngoma ya kilua ambayo ndiyo tulikuwa tunajua ni ya Wamanyema).
 
Back
Top Bottom