Miaka 60 ya uhuru wa Tanganyika Burma Infantry 6th battalion vita vya pili vya dunia na msingi wa TANU 1945

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
BURMA INFANTRY 6th BATTALION

Hiyo picha hapo chini imepigwa Burma wakati wa WWII na hao ni baadhi askari waliokuwa katika Burma Infantry.

Nimeweka pia picha ya Abdul Sykes na Ally Sykes wakiwa Burma.

Katika hawa askari wote nimeweza kupata majina mawili tu nalo ni wa pili kushoto ni Ally Sykes na wa nne ni kijana mwenzake kutoka Bagamoyo.

Kikosi hiki kilikuwa cha askari kutoka nchi nyingi za Afrika zilizokuwa zinatawaliwa na Uingereza kama Northern Rhodesia (Zambia), Southern Rhodesia (Zimbabwe), Nyasaland (Malawi), Belgian Congo (Congo), Nigeria, Gold Coast (Ghana), Kenya, Uganda, Zanzibar na Tanganyika.

Katika kundi hili wapo askari ambao kabla ya kupelekwa Burma walishapigana Abbyssinia (Ethiopia) na Somaliland (Somalia) Uingereza na Afrika Kusini walipopigana na Wataliani.

Katika jeshi hili wapo askari ambao wao walijitolea kwenda kupigana Burma.

Askari hawa kabla ya kupelekwa Burma walifikishwa kwanza Ceylon kwa ajili ya mafunzo ya kupigana vita vya msituni mbali na mafunzo waliyopata Lower Kabete Kenya.

Baada ya mafunzo haya ndipo wakapelekwa Burma kwenda kupigana na Wajapani.

Inashangaza lakini yote haya ni katika changamoto za ukoloni, Mwafrika anajitolea kumtetea yule anaemtawala ashinde vita aendelee kumtawala zaidi.

Moja ya meli iliyokuwa na askari waliokuwa wanaelekea Burma ikitokea Mombasa ilishambuliwa na makombora ya chini ya bahari ya Wajapani na askari wote walikufa ila mmoja tu akiitwa Magembe, kijana kutoka Tanga.

Bahati mbaya sana katika orodha iliyochapwa na jeshi ya askari waliopotea baharini lilikuwa jina la Ally Sykes.

Ally hakuwepo ndani ya meli hii na alifika Burma salama.

Taarifa zikapelekwa katika kambi zote na Abdul Sykes alisoma taarifa ya kifo cha ndugu yake katika gazeti la jeshi likiitwa "Echelon,'' na yeye mara moja akapeleka taarifa hizo kwa baba yake Dar es Salaam.

Nyumbani kwao uliwekwa msiba na khitma ikasomwa msikiti wa Kipata.
Hii Burma Infantry iliongeza nguvu kubwa sana katika vita vya Waingereza dhidi ya Wajapani.

Mafunzo ya vita vya msituni kwa miezi minne yalifanyika sehemu moja inaitwa Kurnegala na kutokea hapo wakaingizwa melini kuelekea Burma kutokea bandari ya Trincomalee na kutoka hapo wakaenda Chittagong.

Safari yote hiyo baharini meli zao zikisindikizwa na British Royal Navy mwendo ukiwa wa taratibu wakichuua tahadhari dhidi ya mashambulizi ya Wajapani.

Hapo Chittagong ndipo askari hawa wa Burma Infantry walipojua nini maana ya vita. Kutoka bandarini hadi kambini ilikuwa kipande cha kilomita 10.

Barabara ilikuwa mbovu sana na tope tupu mguu ukikakanyaga chini unazama hadi vifundoni.

Mvua za Moonson zilikuwa zinanyesha na askari kabeba mzigo wake mzito mgongoni - kitbag, haversack bunduki na risasi.

Ally Sykes alikuwa na umri wa miaka 16 ametoroka kwao nyumbani kuingia jeshini kuja kupigana Burma.

Kufika kambini hakuna kupumzika wakaanza kuchimba mahandaki yao na ya wakubwa zao Waingereza.

Nilikuwa nikikaa na Ally Sykes sichoki kumsikiliza. Yeye alikuwa bingwa wa shabaha na anayo nishani kwa hilo.

Yapo mengi sana ya kuhadithia.

Hii Burma Infantry ndiyo baada ya vita wakiwa Kalieni Camp nje kidogo ya Bombay hapa siku ya mkesha wa Christmas 24 December 1945 askari hawa wakisubiri kurudishwa makwao ndipo Abdul Sykes akawaeleza wenzake wote kuwa wakifika makwao lazima waanze juhudi za kuwaondoa Waingereza katika nchi zao.

Hii ndiyo siku ilipoamuliwa kuunda TANU na taarifa hizi zimo ndani ya shajara ya Abdul Sykes ya mwaka huo.

Ahmed Rashad Ali wakati ule mwanafunzi akisoma Bombay akitokea Zanzibar alifika katika kambi hii kumsalimu Abdul na mdogo wake Ally kabla hawajarudi Tanganyika.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…