Miaka 60 ya uhuru wa Tanganyika: kura tatu na uamuzi wa busara 1958

Miaka 60 ya uhuru wa Tanganyika: kura tatu na uamuzi wa busara 1958

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
MIAKA 60 UHURU WA TANGANYIKA: KUMBUKUMBU YA KURA TATU NA UAMUZI WA BUSARA WA TABORA 1958.

"Katikati ya hotuba katika uwanja wa sokoni Tabora Mwalimu Julius Nyerere hakuweza kuendelea na hotuba akaangua kilio."

Huyo anaezungumza maneno hayo ni Mzee Bilali Rehani Waikela.

Mwaka wa 1989 niko nyumbani kwa Mzee Bilal Rehani Waikela pamoja na wapigania uhuru wenzake, Mohamed Mangiringiri na Ramadhani Singo.

Hadi kufika hapo kwenye kilio cha Mwalimu Nyerere Mzee Waikela katutoa mbali katika historia yake na Julius Kambarage Nyerere mwaka wa 1955 alipokuja Tabora kaongozana na Bi. Titi Mohamed.

Waikela na wenzake wengine kama Abdallah na Maulidi Kivuruga, ndugu wawili hawa, Juma Mrisho mcheza mpira maarufu wa Gossage, Fundi Muhindi kwa kuwataja wachache waliwaalika Bi. Titi Mohamed na Julius Nyerere waende Tabora ili watie hima TANU isimame vyema Western Province.

Kulikuwa na mgogoro.

Wanagombana na Germano Pacha aliyewakilisha Western Province katika mkutano ulioasisi TANU 1954.

Sebule ya Mzee Waikela ilikuwa kimya mimi na yeye tunatazamana uso kwa macho mimi nainama kuandika kisha nanyanyua uso kumtazama.

Wale wapigania uhuru wenzake wametulia wakisikiliza utadhani hawaijui historia hii na wanaisikia kwa mara ya kwanza.

Pembeni yangu nimezungukwa na wapigania uhuru wote ukiwaangalia wamechoka lakini wameitika mwito wa Mzee Waikela kufika nyumbani kwake asubuhi ile.

Taarifa zilizowafikia ati kaja msomi wa Chuo Kikuu Cha Dar-es-Salaam anataka kuandika historia ya uhuru wa Tanganyika.

Mpeleka taarifa kaeleza kuwa na huyo msomi ni mjukuu wa marehemu Baba Popo.
Baba Popo ni babu yangu Salum Abdallah Mwekapopo.

Nani asiyemjua mzalendo huyu?
Kaongoza migomo mitatu ya wafanyakazi dhidi ya Waingereza 1947, 1949 na 1960.

Mjukuu wake ndiye kaja Tabora kuandika historia ya uhuru.
Wazee wa Kimanyema wanachekeshana.

"Mimi si siku zote nawaambieni sisi Wamanyema tuna wazimu."
Haya maneno hayakuwa ya bure yalikuwa na maana kubwa nyuma yake.

Siku zile watu walikuwa wanaogopa kueleza historia ya TANU nje ya ile rasmi.

Babu yangu na Waikela wote waliwekwa kizuizini Jela ya Uyui mwaka wa 1964 baada ya uhuru kupatikana mwaka wa 1961.

Waliposikia nimekwenda kukutananao tuandike historia ya uhuru wakajua hapa lipo jambo na haikuwashangaza kuwa mwandishi ni mjukuu wa Baba Popo.

"Huyu Mohamed Said kachukua wazimu wa babu yake."

Mimi nimesindikizwa kwa Mzee Waikela na wenyeji wangu Salum Ali Mkangwa na Ilunga Hassan Kapungu.

"Peter Mhando alitumwa na Nyerere aje Tabora kuangalia kwa nini hapa viongozi haweshi kugombana."

Waikela anaendelea.
Waikela anazungumza kwa taratibu sana lakini fasaha.

"Sasa katika taarifa yake akamwambia Nyerere kuwa pamoja na hayo mengine Mkutano Mkuu wa TANU wa mwaka wa 1958 ufanyike Tabora."

"Baada ya kupiga kura kuingia kwenye Uchaguzi Mkuu wa Kura Tatu ndiyo siku ya pili tukafanya mkutano pale sokoni na siku ile Nyerere akasema ikiwa Waingereza watakataa kutupa uhuru wetu sisi tutamshtaki kwa Mungu.

Alipomaliza kusema maneno haya Nyerere akaangua kilio na uwanja mzima tulilia."

Mzee Waikela kanifunza mengi kanieleza mengi katika harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika.

(Picha zote kwa hisani ya Abdulaziz Ali Khamis).

Screenshot_20211117-224309_Facebook.jpg
 
Back
Top Bottom