Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
MIAKA 60 YA UHURU WA TANGANYIKA 1961: SALIM AHMED SALIM NA JOSEPH WARIOBA SAKATA LA OIC NA IAO 1993
Picha hiyo ya Salim Ahmed Salim na Joseph Warioba niliwapiga mwaka wa 2017 nyumbani kwa Kleist Sykes, Kawe Beach siku ya mazishi yake baada ya kuwaomba ruhusa.
Leo katika kupita Maktaba nimeikuta hii picha na ikanikumbusha mgogoro wa Zanzibar wa kujiunga na OIC na G 55 kudai serikali ya Tanganyika.
Katika historia ya Tanzania migogoro miwili ilitikisa nchi na katika mitikisiko hiyo ilijibainisha wazi ni watu gani walioshika madaraka ya maamuzi ya serikali ya Tanzania.
Mgogoro wa kwanza ni wa EAMWS uliopelekea serikali kuvunja jumuia hiyo na kuunda BAKWATA na wa pili ni huu wa OIC.
Sababu ya migogoro yote hii ni kuwa kulikuwa na maslahi makubwa kwa Uislam.
Taarifa zinasema kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar iliiomba Serikali ya Jamhuri ya Tanzania kupeleka maombi ya Tanzania kupewa Observer Status katika OIC.
Waziri Mkuu Joseph Warioba akapeleka maombi yale kwa Makamu Waziri Mkuu Salim.
Salim akayazuia yale maombi sababu yataingilia siasa za Tanzania na ndiyo sababu Serikali ya Jamhuri ya Tanzania ikakataa kupeleka maombi yale.
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ikaamua kupeleka maombi yake binafsi si ya Observer Status tena bali ya kuwa mwanachama kamili wa OIC.
Haikupita muda magazeti yakaeleza kuwa Zanzibar imejiunga na OIC.
Moto ulianza kukolezwa kuanzia hapo.
Ndani ya Bunge la Tanzania kuna kundi maalum la maslahi.
Kundi hili likajitenga na kujipambanua kwa Wabunge 55 kudai kureshwa kwa Serikali ya Tanganyika.
Kundi hili la wabunge 55 lilikuja kufahamika kwa jina la G55.
Hili kundi maslahi lipo toka Tanganyika ipate uhuru na lina nguvu kubwa sana.
Lina uwezo wa kuwasha na kuzima.
Wazanzibari katika sakata hili ndipo ilipowadhihirikia na wakajua hadhir kabisa ni nani wanaendesha Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Wazanzibari wakatambua nchi yao wameungana na nani na lipi wanaruhusiwa kufanya na lipi hawana ruksa.
Maneno ya William Lukuvi na marehemu Samwel Sitta kuhusu Zanzibar yalipokuja miaka mingi baada ya sakata la OIC kumalizika wafuatiliaji wa siasa za Tanzania hawakushangazwa.
Mkasa wa OIC ni mrefu na wenye mengi ya kusisimua na kushangaza.
Prof. Kighoma Malima anasema wakati mjadala wa OIC umepamba moto Karimjee Hall iko siku alikwenda ofisini kwa Rais.
Aliyoshuhudia yalimtia simanzi kubwa.
Rais alikuwa kachoka na mtu aliyepwelewa kwa propaganda ndani ya serikali yake, ndani ya Bunge na mawe aliyokuwa akipopolewa na magazeti binafsi na ya chama chake CCM chenyewe.
Kulikuwa na maneno ndani ya Bunge ya kumshtaki Rais kwa kuvunja katiba.
Ikamjia fikra kuwa lazima wapatikane watu nje ya serikali na Chama Cha Mapinduzi kulisaidia Bunge kujiangalia upya.
Haya yakifanyika Prof. Malima aliona Rais atafarijika kwa kutambua kuwa nje ya Bunge ana umma wa watu nyuma yake wenye Imani na yeye na wana nguvu kubwa nje ya Bunge, CCM na serikali yake.
Prof. Malima alikuwa na hakika kuwa haya yakifanyika Bunge litatambua kuwa limewasha moto ambao wao hawana maji ya kuuzima.
Na kwa hakika moto uliwashwa nje ya Bunge na ukakolea vizuri sana.
Siku moja Ahmed Saleh Yahya alinipigia simu akiwa Dar es Salaam kunikaribisha chai kwenye mkahawa wangu niliokuwa nikiumpenda sana, Chef Pride pale Chagga Street.
Ahmed Yahya walikuwa mhariri wa jarida maarufu Africa Events lililokuwa linachapwa London.
Nilijua liko jambo.
Mtu haji Dar es Salaam kutoka London kisha akakualika chai hivi hivi lazima patakuwa na kitu.
Ahmed Saleh akaniambia, ''Mohamed mbona rais anashambuliwa na kila mtu nanyi mko kimya?''
Ukweli ni kuwa hatukuwa kimya.
Moto ulikuwa umekolezeka kupitia gazeti la Annur nan vilevile kulikuwa na makala katika makaratasi yakichapwa na kusambazwa misikitini kika siku ya Ijumaa kumtetea Rais na kuliweka wazi zaidi suala la OIC.
Alichotaka kukiona Ahmed Saleh ni makala katika majarida ya kimataifa kama Africa Events.
Kipindi kile makala zetu zilikuwa zimepigwa marufuku kuchapwa Africa Events kwa makubaliano maalum kati ya Africa Events na watu fulani hapa nyumbani kwa maslahi ya pande zote mbili.
Kuna msemo, ''Nikune mgongo wangu nami nitakukuna wako.''
Hiki ni kisa kingine kinahitaji makala yake makhsusi.
Sikuona haja ya kumwambia Mhariri wa Africa Events kuwa mmetupiga marufuku.
Nilimuahidi kumpelekea makala ya kumhami Rais.
Makala hii ilichapwa bila ya jina la mwandishi na toleo lenyewe ni hilo hapo chini kwenye picha.
Katika kitabu chake Rais Mwinyi ameeleza sakati hili la OIC kwa kirefu lakini kalamu yake ilijifungia ndani ya yale yalikuwa ndani ya Bunge na serikali.
Rais hakunyanyua kichwa chake wakati anaandika kuutazama ule moto uliowashwa nje ya Bunge kwa madhumuni ya kuwatisha maadui zake.
Moto huu ndiyo uliomnusuru na yale yaliyokusudiwa na kupangwa dhidi yake.
Haya kwa bahati mbaya sana hayamo kitabuni.