Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
MIAKA 60 YA UHURU WA TANGANYIKA: SALUM ZAHORO (1936 - 2020) NA KIKO KIDS JAZZ
Haikupata kunipitikia hata siku moja kuwa jina langu litatokeza hadharani na kwenye cover ya muziki wa Salum Zahoro na bendi yake ya Kiko Kids.
Imekuwaje sasa jina langu likawa katika cover hiyo pmoja na majina ya watu wengine ambao walikuwa katika mchakato wa kumtafuta Salum Zahoro na kutoa muziki wake upya, muziki ambao ulikuwa ukivuma na kupendwa zaidi ya miaka 50 iliyopita?
Salum Zahoro alikuwa akifahamiana na baba yangu baba akipenda sana muziki wake.
Naamini alikuwa na santuri zake zote kwani mimi napata akili sawasawa nimekuta santuri hizi katika maktaba yake na mara moja moja akizipiga katika record player yake ya Danset au kwenye radiogram.
Mara ya mwisho kumuona Salum Zahoro ilikuwa kiasi cha miaka 30 iliyopita alikuwa kasimama kituo cha basi cha uhuru pembeni ya Shule ya Wavulana ya Uhuru.
Mimi nilkuwa nimeongozana na binamu yangu Zuhra bint Hussein Milala.
Wote wawili wametangulia mbele ya haki vifo vyao vikifuatana.
Zuhra akachepuka kwenda kumwamkia na mimi nikamfuata.
Hawa wote ni watu wa Tabora na koo zinafahamiana.
Sikupata nafasi ya kuzugumza na Salum Zahoro lakini ilinitosha kuwa nilimwamkia.
Mwaka huu nikaona picha ya Salum Zahoro katika mtandao ikieleza kuwa ni mgonjwa.
Salum Zahoro alikuwa mtu wa kujipenda sana hasa katika mavazi na Allah alimjaalia sura jamili.
Picha ile niliyoiona akiwa katika maradhi ilinichoma sana nami sikusita nikampelekea taarifa rafiki na ndugu yangu Hamisi Delgado.
Delgado kwa miaka mingi sana alihamia Ulaya lakini kila akija nyumbani kusalimia jamaa lazima atapita kwangu kunijulia hali.
Nilimpelekea taarifa hii ya ugonjwa wa Salum Zahoro kwa kuwa nilijua yeye ni mzee wake.
Halikadhalika taarifa hii niliwarushia na jamaa wengine wenye asili ya Tabora wafahamu na ikiwezekana watoe msaada katika tiba.
Delgado hakukawia siku ile ile alinijibu na kuniambia kuwa anafuatilia maradhi ya Salum Zahoro kwa karibu na atakuja Dar es Salaam.
Wakati huu wa maradhi ya Salum Zahoro kulikuwa na mradi wa kukusanya baadhi ya muziki wake na kutengeneza album Ujerumani na Delgado alikuwa mmoja wa wahusika wakuu.
Delgado alikuja na kumtembelea Salum Zahoro hospitali ya Amana alikokuwa amelazwa na alitoa msaada mkubwa kwake.
Haukupita muda mrefu Salum Zahoro akafariki.
Mwezi uliopita Delgado alikuja Dar es Salaam na kunipa album ya Salum Zahoro na Kiko Kids na ndani nikakuta jina langu limetajwa kama shukrani kwa kufahamisha jamii maradhi ya Salum Zahoro.
Nilishangaa kuona kuwa album hii ni katika santuri na siyo CD.
Delgado akanifahamisha kuwa Ulaya kwa hivi sasa wamereja tena kwenye santuri.
Ndani ya album hii kuna kurasa kadhaa zenye historia na picha za Salum Zahoro akiwa kijana mdogo wa miaka 20 mwaka wa 1953 alipoanza muziki.
Delgado kafanya kazi kubwa sana katika historia ya wanamuziki wa Tanzania kwa kuandika maisha ya Salum Zahoro.
Katika kufanya hivyo kaandika mengi kuhusu mchango wa Salum Zahoro na Kiko Kids kutunga nyimbo nyingi za kuhamasisha uhuru wa Tanganyika na maendeleo yake baada ya uhuru.
Mwenyezi Mungu amsamehe madhambi yake na amuweke mahali pema peponi.
Picha ya kwanza ni cover ya album kwa mbele ikimuonyesha Salum Zahoro na picha ya pili ni nyuma ya cover.
Picha ya tatu ni Salum Zahoro na Kiko Kids wa kwanza kulia waliokaa.
Amin.