Miaka 60 ya uhuru wa Tanganyika1961: hotuba ya bajeti ya waziri wa fedha Prof. Kighoma Ali Malima ilipoibiwa wizarani 1994

Miaka 60 ya uhuru wa Tanganyika1961: hotuba ya bajeti ya waziri wa fedha Prof. Kighoma Ali Malima ilipoibiwa wizarani 1994

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
MIAKA 60 YA UHURU WA TANGANYIKA: HOTUBA YA BAJETI YA WAZIRI WA FEDHA PROF. KIGHOMA ALI MALIMA ILIPOIBIWA WIZARANI 1994

Ndani ya Bunge kulikuwa na kundi la wabunge ambao wao walijijumuisha kwa kazi moja tu nayo ni kuhakikisha kuwa Prof. Kighoma Ali Malima wanamzomea kwa kila atakalochangia katika miswada iliyokuwa ikiletwa Bungeni.

Haya wakifanya ndani na nje ya Bunge.

Kundi hili lilikuwa pia linajumisha watendaji wakubwa ndani ya wizara za serikali pamoja na wahariri wa magazeti.

Inasemekana hawa wahariri walikuwa wakipata chochote kitu kwa kufanya kazi hii.

Prof. Malima akifanyiwa kila aina ya vitimbi, hila na hujuma ndani ya serikali yake na Bungeni na katika magazeti akiandikwa vibaya kabisa.

Prof. Malima alikuwa na nani wa kumtetea?

Akihadithia haya baada ya kujitoa serikalini na CCM nilimsikia akisema yeye alikuwa na Allah peke yake.

Hakika Allah alimtosha.

Kuna watu huwa nikaandika historia zao machozi hunilengalenga.

Prof. Malima anasema yeye alikuwa anamtegemea Allah.

Maadui hawa wa Prof. Malima walijishusha chini kiasi cha kuwa mwaka wa 1994 waliiba Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Fedha ambayo Prof. Malima alikuwa aisome Bungeni siku ya pili yake.

Hii kauli yangu yangu ya kusema vitu kadhaa vimeibiwa ilipingwa sana na mhariri wangu wa kitabu cha Abdul Sykes lile toleo la kwanza lililochapwa London mwaka wa 1998.

Mhariri akinidai nitoe ushahidi kuwa kweli kulikuwa na wizi vinginevyo tunaweza kujikuta tuko matatani.

Lakini utasema nini ikiwa Hotuba ya Bajeti inachukuliwa ndani ya ofisi ya serikali na inakuwa katika mikono ya watu?

Siku moja kabla ya Prof. Malima kusoma bajeti yake ya Wizara ya Fedha maadui zake walijifungia kwenye hoteli moja maarufu katikati ya Jiji la Dar es Salaam wakiipitia bajeti ile na kufundishana maswali ambayo wao walidhani yatatia maji hotuba ile na kumfedhehesha Prof. Malima.

Prof. Malima anasema pale tu maadui zake ndani ya Bunge walipoanza kuuliza maswali yao hapo hapo akajua kuwa ile hotuba yake imevujishwa mapema na walikuwanayo wale Wabunge kwa kazi maalum.

Ulikuwa mtu ukibahatika kuzungumza na Prof. Malima utastarehe.

Prof. anasema walipokuwa wanamuuliza yale maswali yao yeye ilikuwa ikimjia picha ya wanafunzi wajinga wasiojiweza katika masomo.

Wanafunzi mbumbumbu wameiba mtihani ili wapasi somo lakini hata hivyo hawawezi kujibu maswali ya mtihani kwa kuwa hawana akili.

Prof. yeye akiwa mwalimu anayaangalia yale majibu ya wanafunzi wake na anaanza kucheka kwa kuchekeshwa na yale majibu.

Hapa ndani ya Bunge la Jamhuri ya Tanzania Prof. Malima alikuwa anachekeshwa na maswali aliyokuwa anaulizwa.

Haya ya wezi kuiba nyaraka za serikali kuja kuifedhehesha serikali hayakupata kutokea katika serikali ya Mwalimu Nyerere.

Hakuna mtendaji aliyekuwa na ujasiri wa kuiba nyaraka za ya serikali akaipeleka kusiko wala hapakuwa ma mtumishi aliyekuwa na ujinga wa kulichezea Bunge na kumchezea waziri wa Mwalimu.

Mwalimu alipata kumuuliza Mkurugenzi Mkuu wa shirika moja la umma aliyekataa kumlipa ndugu yake Amir Jamal kwa kudai kuwa madai yake hayakuwa ya kweli kwa kuwa kulikuwa na matatizo yaani, ’technicalities,’’ ziliyofanya madai yake yakataliwe.

‘’Unasema kuwa Amir Jamal alikuomba umsaidie ndugu yake na wewe ukaahidi kufanya hivyo.

Leo unaniambia kuwa huyu ndugu yake Jamal si mkweli.

Fahamu kuwa Jamal ni waziri wangu na mimi namuamini Jamal.

Ikiwa Jamal kamuamini nduguye na kamkingia kifua kwako na mimi namuamini Jamal basi ikiwa huyu ndugu yake si muadilifu basi hata Jamal hawezi kuwa muadilifu na mimi pia kwa kumuamini Jamal mimi vievile si muadilifu.’’

Ujumbe wa Nyerere ulikuwa umemfikia Mkuregenzi sawia.

Alimuomba radhi Mwalimu na jambo likesha kwa salama.

Haya aliyokuwa yanamfika Prof. Malima yalikuwa hayajapata kutokea wakati wa Mwalimu Nyerere.

Haya yaliyomfika Prof. Kighoma Ali Malima yalikuwa mambo mageni na yalikusudiwa kuwatia hofu wale ambao walikuwa na fikra ya kuwadaia wananchi wanaodhulumiwa haki na usawa.

Screenshot_20211204-141048_Facebook.jpg
 
Buji...
Nataka uhangaishe ubongo wako ili upate jibu wewe mwenyewe la swali lako.

Zanzibar ilijiunga na OIC mwaka wa 1994.
Lakini ikalazimishwa kujitoa.

Unadhani maamuzi haya yalitolewa na nani?

Rais Muislam na Wazanzibari Waislamu?
 
Back
Top Bottom