Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
MIAKA 60 YA UHURU WA TANGANYIKA 1961: "UAMUZI WA BUSARA" KITABU KUADHIMISHA MIAKA 50 YA KURA TATU 1958
Utangulizi
Kitabu hicho hapo chini, "Uamuzi wa Busara," mwaka nilikiandika mwaka wa 2008 kwa shinikizo kutoka Abantu Publishers, Nairobi wakitaka pawepo kitabu kitakachokuwa kama rejea la tukio hili muhimu katika historia ya uhuru wa Tanganyika.
Fikra yao ilikuwa kukifikisha kitabu hicho katika ngazi za juu za CCM na serikali yake na ikiwezekana kiongozi wa juu kabisa aandike utangulizi wake.
Haya yote hayakufanikiwa lakini Abantu Publishers walikichapa kitabu.
MWAKA 1958 serikali ya kikoloni baada ya kushindwa ilikubali ufanyike uchaguzi wa Baraza la Kutunga Sheria ambao viti vilikuwa vishindaniwe kwa misingi ya rangi.
Kulikuwa na viti kwa ajili ya Wazungu, Wahindi na Waafrika.
Masharti mengine ya kumwezesha Mwafrika kupiga kura yalimtaka awe na kipato cha paundi mia nne za Kiingereza kwa mwaka, awe na kiwango cha elimu ya darasa la kumi na mbili na awe ameajiriwa katika kazi maalum. Haya yalikuwa masharti magumu na yaliyoonekana kama hayataweza kukubalika na TANU.
TANU ilifanya mkutano wake mkuu wa mwaka wa 1958 mjini Tabora kuanzia tarehe 21-26 Januari, 1958 kujadili miongoni mwa mambo mengine ikiwa ishiriki katika uchaguzi chini ya haya masharti ya kibaguzi yaliyowekwa au isusie uchaguzi.
Mkutano huu wa Tabora ulitishia kuigawa TANU katika kambi mbili hasimu.
Kambi moja ni ile ya wenye siasa za wastani waliopendelea kushiriki katika uchaguzi na ile ya pili ni ile ya wenye msimamo mkali waliotaka uchaguzi ususiwe kabisa.
TANU ilinusurika na kile ambacho kingeweza kuwa mgogoro ndani ya chama ambao ungewafanya wale wenye msimamo mkali kama Sheikh Suleiman Takadir, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU katika makao makuu, Zuberi Mtemvu, wakati huo katibu mwenezi wa TANU, kufanya mapinduzi ambayo yangekigawa chama mapande mawili kama isingelikuwa busara ya Mwalimu Nyerere, Abdallah Rashidi Sembe, Hamisi Heri na viongozi wa TANU wa Tanga ambao walipanga mkakati wa kuwashinda 'siasa kali' katika chama.
Lakini ili kuzielewa hisia za wanachama wa TANU, uongozi wake na nguvu zilizokuwa zikidhibiti siasa Tanganyika wakati ule wa ukoloni, na ili kuelewa kwa nini Kura Tatu ilizua mgogoro na kutoelewana katika uongozi, inatubidi turudi nyuma.
Tunahitaji kuyatazama mambo kwanza kuanzia Tanga mahali ambapo Mwalimu Nyerere na uongozi wa TANU Tanga walikutana kwa siri kuweka mikakati ya mkutano wa Tabora.
Baada ya kufanya hivyo tufichue jambo moja baada ya jingine katika mkakati wa Sheikh Abdallah Rashid Sembe, Mwalimu Kihere na Mwalimu Nyerere uliofanya wafuasi wa siasa za wastani wawashinde wale waliokuwa na msimamo mkali.
Inasikitisha kuwa kisa hiki cha ujasiri na mbinu za hali ya juu kama zilivyoonyeshwa na watu wa Tanga hadi leo kimebaki siri kuu.
Wanaokifahamu kisa hiki wengi wao wameshakufa.
Picha ya kitabu, Mwalimu Kihere, Sheikh Abdallah Rashid Sembe, Wagombea wa TANU katika Uchaguzi wa Kura Tatu 1958 wakiwemo Waafrika, Waasia na Wazungu,