Miaka 75: Jinsi India ilivyotoka kwenye ukoloni wa Muingereza mpaka uchumi wa tano imara zaidi Duniani

Miaka 75: Jinsi India ilivyotoka kwenye ukoloni wa Muingereza mpaka uchumi wa tano imara zaidi Duniani

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Leo ni sherehe za uhuru nchini India toka walipopata uhuru kutoka kwa Muingereza mwaka 1946. Kwa miaka 75 India imejenga uchumi unaokua haraka zaidi huku ikiwa imebeba miongoni mwa watu matajiri zaidi duniani na kulingana na umoja wa mataifa punde itaipita China kwa idadi ya watu.

"Muda umefika ambapo unakuja mara chache kwenye historia, tunapotoka kwenye zamani kwenda kwenye mpya". "Pale umri unapoisha na pale moyo wa Taifa unapokandamizwa muda mrefu, unapata sauti" Ilikuwa kauli ya Waziri mkuu wa kwanza wa India wakati wanajitwalia uhuru wao mwaka 1946 huku ajenda kuu ikiwa kuzaliwa upya.

Miaka 75 baadae India ya Modi unaweza usiitambue kutoka kwenye India ya Jawaharlal Nehru.

Pamoja na utajiri mkubwa unaomwagika India, umasikini ni mkubwa kwa mamilioni ya wahindi huku kukiwa na tofauti kubwa kati ya wenye nacho na wasio nacho.

India independence.jpg

UCHUMI
Baada ya uhuru India iliingia kwenye janga, umwagaji damu kutokana na mgawanyiko ukiua watu kati laki tano na milioni mbili. Umri wa kuishi ukiwa miaka 37 kwa wanaume na 36 kwa wanawake huku ikikumbwa na umasikini uliokubuhu.

Karne kasoro robo, Uchumi wa India unakaribia dola trilioni 3 huku ikiwa na uchumi wa tano imara zaidi duniani na unaokua kwa kasi.

Umri wa kuishi unakadiriwa miaka 70 huku wahindi wakitawanyika Dunia nzima na kushika nafasi mbalimbali muhimu hasa makampuni makubwa ya teknolojia.

Sehemu kubwa ya mabadiliko yalitokea miaka ya 90 ambapo waziri mkuu wa wakati huo, Narasimha Rao na waziri wake wa fedha waliifungua nchi kukaribisha uwekezaji wa nje baada India kukumbwa na deni kubwa ikiambatana na mfumuko mkubwa wa bei, India ilibadili sera ya Ujamaa iliyotengezwa Nehru kwa utawala kuingilia mambo nchini humo.

USAWA KATI YA RAIA
India ni moja ya nchi yenye tofauti kubwa zaidi kati ya tajiri na masikini. Asilimia 10 ya wahindi wanashikilia 77% ya utajiri wa India huku 90% wakigawana kinachobaki huku kasi ya watoto ombaomba ikiongezeka katika mitaa ya India.

Akiwa amesimama mbele ya ngome nyekundu ya kihistoria, Waziri mkuu Modi ameahidi mabadiliko na kuibadilisha India kuwa na uchumi ulioendelea kwenye miaka 25 ijayo kuelekea kutimiza karne moja

India inequality.jpg
 
Uchumi wa kipuuzi ambao sitaki hata kuusikia huo. Mfyuuuuuu
 
Back
Top Bottom