Miaka inaenda familia inamkatalia asioe...

chitanda.nyoka

Senior Member
Joined
May 3, 2012
Posts
193
Reaction score
43
Wana jf kuna kaka yangu ana miaka 31 ana kazi nzuri inayomtosha kuanzisha family pia kuna dada yetu mkubwa ana miaka 33 ambaye hajabahatika kupata mume wala hana mtoto kwa kweli amekua na mawazo sn anaweza akapata bf wanakaa km miez 3 au 4 then jamaa anapotea,ss tatizo kaka anataka kuoa mama anamkatalia anamwambia asioe mpaka dada aolewe coz atajisikia vibaya mdogo wake akianza kuoa kabla yake.jf tunamshauri vp huyu kijana coz huyo dada yetu hata dalili hana maana afadhari kungekua na mtu kaleta angalau barua kidogo tungekua na moyo.
 
Poleni sana. dada yenu akiahirisha kuolewa sijui itakuaje. mia
 
Hiyo mipango kaweka nani ya kuwa mkubwa ni lazima aoe au aoelewe ndio wadogo wafatize. Mtafutieni wazee wamuelimisha ikiwezekana hata wakuu wa dini ajue hiyo itasababisha kijana kuendelea kuzini. Ikishindikana, mimi sioni tatizo ya yeye kuendelea kumtii mamake kwa hilo. Kama anaweza oa bila kushirikishwa itakuwa ni bora, blessing zinatoka kwa mungu hasa ikiwa ni kitu chenye kheri.
 
Kwa hiyo huyo dada asipoolewa kabisa wadogo zake wote hawataoa wala kuolewa?? aisee hii ni brand new kwangu!
 
mnashangaa! hili ni jambo la kawaida kwenye familia nyingi. marriage order = child order
ushauri ni kaka aoe kama kapata mwenzi, dada yake akiumia roho atajiju
 
hii tabia ipo sana jamani, ila mama akielimishwa ataelewa, rafiki yangu ilimtokea, dadake mkubwa hakuwa ameolewa mama akagoma ila baada ya kushauriwa mama akakubali na tukacheza harusi. Inawezekana
 
mh,mila na destury zingne zishapitwa na wakat. nahc hii ni mila ya kabila flan. to hell bana mwambie kaka yako amchukue msichana wake aishi nae dada ake akiolewa ndo aende nae kufunga ndoa. mila nyingne noma!
 
Utamaduni mwingine wakiduanzi kinoma.
 
Mimi nilioa kabla kaka yangu hajaoa,tatizo ni nini?
 
Suala la kuoa na kuolewa ni la mtu binafsi na sio la Familia. Nashangaa mtu ana mwenye umri unaozidi miaka 18 eti bado anafanyiwa maamuzi na wazazi wake, huo ni utumwa kuliko ule wa waarabu. Wazazi kazi yao ni kushauri na wala sio kuwafanyia maamuzi ndugu. Pia usisahau kuwa Mungu ndiye aliyeumba wazazi ni vyombo vilivyotumika kwa hivyo maamuzi yako kwenu.

Asanteni sana!!
 
kwa hiyo dada yenu asipoolewa kaka yenu nae hatooa? ina maana familia nzima haitooa wala kuolewa?
ama kweli urasimu hadi kwenye familia sio mchezo.......

kaka yako anajua kuwa anaishi maisha yake?
na kila mtu ana uhuru na uamuzi juu ya maisha yake?
:shock:
 
Mdogo wangu kaolewa 2010,wakati mimi kaka yake bado sijafikiria kuoa,je ingekua lazima tusubirie mkubwa aoe kwanza huoni apo dada yng angekosa mume?mila nyingine hazina umuhimu wowote zaidi ya uchuro tu.
 
kwani mama yenu ni mungu mtu..........usikute huyo kaka yako ni bank teller af unamuona kasooooooma.....yeye ndiye tatizo...mama hana tatizo..kaka yako ndiye zoba
 
Samahani lakini huyo Bi mkubwa wenu ana sababu hiyo tu au zaidi ya hiyo? Na kaka yenu mwenyewe anasemaje na uamuzi wa mama yenu? Tahadhari kunaweza kukawa na sababu nyengine na kwa kupoza pengine mama anahisi huduma atakazotowa kaka zitashifti kwa mke hivyo anajificha kwa kutumia dada yenu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…