Miaka kumi na saba (17) ya bonde la mto Nile - Nairobi, Kenya

Miaka kumi na saba (17) ya bonde la mto Nile - Nairobi, Kenya

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
MIAKA KUMI NA SABA (17) YA BONDE LA MTO NILE - NAIROBI, KENYA.

Mhe. Eng. Maryprisca Mahundi (Mb) ambaye ni Naibu Waziri wa Maji mnamo tarehe 22 Februari 2023 ameiwakilisha Tanzania katika sherehe za miaka 17 ya Bonde la mto Nile Jijini Nairobi Kenya mkutano uliojumuisha nchi Kumi na Moja wanachama.

Awali sherehe hizo zimetanguliwa na maandamo ambapo mkutano huo umelenga kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi sambamba na matumizi bora ya mto Nile.

Katika hotuba yake Mudavadi amehimiza Mataifa wanachama kuhifadhi maji yanayotokana na mvua kwani wakati mwingine huleta migogoro katika nchi hizo za Afrika Mashariki.

Kwa upande wake Mhe. Eng. Mahundi ambaye pia ni Mwenyekiti wa mkutano huo amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kulipa ada zote za uanachama hivyo Tanzania kutokuwa na deni.

Aidha, Mhe. Eng. Mahundi amezitaka nchi wanachama kutunza mto Nile ili uwe endelevu na kusisitiza utoaji elimu kutunza mazingira na vyanzo vya maji ili maji ya mto Nile yatumike pia kuzalisha umeme na kilimo cha umwagiliaji.

#NileDay2023
#MajiniUhai
#KaziIendelee
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-02-25 at 20.08.11(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-02-25 at 20.08.11(1).jpeg
    68.6 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2023-02-25 at 20.08.15(2).jpeg
    WhatsApp Image 2023-02-25 at 20.08.15(2).jpeg
    25.9 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2023-02-25 at 20.08.15(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-02-25 at 20.08.15(1).jpeg
    36 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2023-02-25 at 20.08.15.jpeg
    WhatsApp Image 2023-02-25 at 20.08.15.jpeg
    49.8 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2023-02-25 at 20.08.13.jpeg
    WhatsApp Image 2023-02-25 at 20.08.13.jpeg
    53.5 KB · Views: 4
Back
Top Bottom