Idd Ninga
JF-Expert Member
- Nov 18, 2012
- 5,497
- 4,775
1.Tulimponda fulani,kwamba anacheka cheka
Kila siku yu angani,na madege anaruka.
2.Leo katua jamani,yule alofikirika
Ukiuleta utani,ni fimbo anakunyuka.
3.Miguu katia ndani,myaka mitatu yafika
Madili ya kibandani,yameanza sahulika.
4.Nalo joto la jioni,linazidi kutushika
Posho zile vikaoni,nazo zimeadimika.
5.Na wanyonge kilioni,wengine wafurahika
Kuipata ahueni,ile ilohitajika.
6.Ni mpingo wa porini,kwa shoka hutokatika
Panga lako ni la nini,bure utaaibika.
7.Korosho za mashambani,ndo hivyo zinabebeka
Ila zile za rohoni,mbali zaenda jizika.
8.Mze Baba yu vitani,magwanda yanavalika
Kabeba debe la tani,na bakora kaishika.
9.Wale wavaa vidani,wameanza kuchizika
Wanashanga vifuani,za dhahabu zatoweka.
SHAIRI-MZEE BABA.
MTUNZI-Idd Ninga,Tengeru Arusha.
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com
Kila siku yu angani,na madege anaruka.
2.Leo katua jamani,yule alofikirika
Ukiuleta utani,ni fimbo anakunyuka.
3.Miguu katia ndani,myaka mitatu yafika
Madili ya kibandani,yameanza sahulika.
4.Nalo joto la jioni,linazidi kutushika
Posho zile vikaoni,nazo zimeadimika.
5.Na wanyonge kilioni,wengine wafurahika
Kuipata ahueni,ile ilohitajika.
6.Ni mpingo wa porini,kwa shoka hutokatika
Panga lako ni la nini,bure utaaibika.
7.Korosho za mashambani,ndo hivyo zinabebeka
Ila zile za rohoni,mbali zaenda jizika.
8.Mze Baba yu vitani,magwanda yanavalika
Kabeba debe la tani,na bakora kaishika.
9.Wale wavaa vidani,wameanza kuchizika
Wanashanga vifuani,za dhahabu zatoweka.
SHAIRI-MZEE BABA.
MTUNZI-Idd Ninga,Tengeru Arusha.
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com