Daah, sasa ndo umeamua kumwaga mchele hapa !? Halafu ile thread kuhusu yule binti wa SAUT nimeona kwenye newspaper moja la udaku, sasa sijui walikuomba ruhusa kuchapisha habari yako au la!!Pole ndugu yetu,
Kuna kamchezo siku hizi watu wanatest kwanza siku ya harusi unakuta bibi harusi kavimba, hapo hapo tunajua mdau alikuwa anatest ishu kama productive hapo inabidi uvumilie tu linaweza kuwa tatizo kwako alafu mkeo akajaribiwa nje ikawa noma. Mfarijiane tu.
... Pole sana - Hii hali huwa ni mtihani mkubwa na inahitaji uvumilivu wa kupita kiasi
Pole ndugu...sina ushauri ila nitawaweka mikononi mwa Mungu na Mungu atawasaidia!
Pole sana ndugu yangu;
Pole sana mkuu...
Ramos, pole sana kwa hii hali.
Pole sana Ramos, ...
Hivi wale washauri nasaha huwa wanatoa pole kwa mshauriwa?Pole ndugu yetu,...
...kuna watoto kibao,wanahitaji 'homes' suala la kuadopt tusiliache kuwa ni la wazungu na culture yao!
Hivi wale washauri nasaha huwa wanatoa pole kwa mshauriwa?
Hi wanaJF
Mimi ni mwanaume, nimeoa miaka mitatu iliyopita. Kwa sasa nina miaka 32 ya umri. Mimi na mke wangu hatuna mtoto kwa miaka hiyo mitatu. Tatizo ni kuwa siku hizi nimeanza kuingiwa na kaushawishi ka kutafuta mtoto nje ya ndoa. Najua ni hatari kiafya lakini najishawishi kuwa nitafanya taratibu zote za kuwa mwangalifu. Siku zote kila ninapowaza hilo la kwenda nje ya ndoa nakumbuka siku ile pale kanisani nilipoahidi mbele ya mashahidi, mbele ya padre na mbele ya mungu kumpenda na kumlinda mke wangu katika SHIDA na raha. Kinachonishangaza ni kuwa hiyo consiousness siku hizi inapungua, nazidiwa na ushawishi. Nikisikia rafiki zangu wakiongelea watoto wao, nikisikia stori kuwa kuna watu hawakuwa na watoto kwenye ndoa, wakajawapata nje, na nikiwaza kuwa nina kazi nzuri kidogo itakayonofanya pengine niwe na raslimali zitakazohitaji kurithishwa baadae najihisi kama nitashawishika. Jingine kubwa ni kuwa mke wangu nae ni mkubwa kidogo (miaka 31) na siku zinakwenda.
Tulishachukua hatua ya kucheki kama tuna matatizo kiafya, lakini sote hatukuonekana kuwa na matatizo, ingawa ni katika vipimo vile vya kawaida hospitali zetu ziliweza kuhandle (najua kuna vipimo complex nje ya nchi ambavyo uchumi hauturuhusu kuvipata). mi na mke wangu tunaheshimiana sana, tunapendana sana lakini naogopa na sijawahi kuonyesha hali yoyote kwake kuwa nawaza kutafuta mtoto nje.
WanaJf naombeni ushauri wenu...

pole sana jamaa, tafadhali naomba uniPM (uniandikie Private Msg), kuna maswali ya papo kwa papo nataka kukuuliza and then ntajitahidi nikupe ushauri ambao umewasaidia wengi, na nina uhakika mtafanikiwa kupata mtoto, if and only if mlishawahi kwenda kuchekiwa na kuambiwa wote mko mswano