Utawasaidia wengi sana kama utaweka hapa; Na hili jambo muhusika keshaliweka wazi kwanini unataka kwenda mafichoni?
japo hata kama magonjwa yanafanana lakini kwa daktari anaingia mmojmmoja na mlango unafungwa, japo jamaa kaweza wazi lakini asilimia kubwa ya maelezo hayapo wazi, hivyo privace inahitajika kwa kiasi fulani
Ramos, miaka mitatu ni michache sana kwa suala la mimba!! Wapo wengi waliodumu kwa miaka 15-20 na wakapata watoto!!! Kama huna tatizo kisayansi basi geukieni pia kwa Mungu wenu. Kuna vifungo vingi ambavyo binadamu hufungwa na shetani kupitia kwa wanadamu hivyo hebu jaribuni maombi kwa watumishi wa Mungu. Fahamu kuwa kuna mapepo, majini na nguvu nyinginezo za jiza ambazo zinaelekezwa kwa binadamu na binadamu mwingine kwa makusudi ya kishetani. Amini kuwa Mungu anaweza na utafanikiwa mno. Pia naomba mfanye kipimo cha damu yako na ya mkeo, kuna damu nyingine ni tatizo pia. Kipimo hicho kipo hata hapa Tz si lazima nje ya nchi. Nendeni kwa Gyno atawasaidia!!!
Pia wakati wa tendo la ndoa, relax kabisa na mkeo, atoe stress na mawazo kuwa sipati mimba. Ajione ndiyo kwanza mmemkutana leo. Hofu wakati mwingne ni mbaya sana hasa katika kutunga mimba. Kwa mantiki hii ni vema mkawapata pia Counselors ya masuala ya ndoa na mapenzi.
Hi wanaJF
Mimi ni mwanaume, nimeoa miaka mitatu iliyopita. Kwa sasa nina miaka 32 ya umri. Mimi na mke wangu hatuna mtoto kwa miaka hiyo mitatu. Tatizo ni kuwa siku hizi nimeanza kuingiwa na kaushawishi ka kutafuta mtoto nje ya ndoa. Najua ni hatari kiafya lakini najishawishi kuwa nitafanya taratibu zote za kuwa mwangalifu. Siku zote kila ninapowaza hilo la kwenda nje ya ndoa nakumbuka siku ile pale kanisani nilipoahidi mbele ya mashahidi, mbele ya padre na mbele ya mungu kumpenda na kumlinda mke wangu katika SHIDA na raha. Kinachonishangaza ni kuwa hiyo consiousness siku hizi inapungua, nazidiwa na ushawishi. Nikisikia rafiki zangu wakiongelea watoto wao, nikisikia stori kuwa kuna watu hawakuwa na watoto kwenye ndoa, wakajawapata nje, na nikiwaza kuwa nina kazi nzuri kidogo itakayonofanya pengine niwe na raslimali zitakazohitaji kurithishwa baadae najihisi kama nitashawishika. Jingine kubwa ni kuwa mke wangu nae ni mkubwa kidogo (miaka 31) na siku zinakwenda.
Tulishachukua hatua ya kucheki kama tuna matatizo kiafya, lakini sote hatukuonekana kuwa na matatizo, ingawa ni katika vipimo vile vya kawaida hospitali zetu ziliweza kuhandle (najua kuna vipimo complex nje ya nchi ambavyo uchumi hauturuhusu kuvipata). mi na mke wangu tunaheshimiana sana, tunapendana sana lakini naogopa na sijawahi kuonyesha hali yoyote kwake kuwa nawaza kutafuta mtoto nje.
WanaJf naombeni ushauri wenu...
Mkuu,
Kuna watu wanapata watoto wakiwa na 40 na kuendelea - Mimi sio malaika (nina mtoto nje ya ndoa pia), lakini na ndani ya ndoa ninao wawili - Tatizo kubwa ni kwamba ukitoka nje ya ndoa unaweza usirudi! Also unaweza kutoka na bado uka-end up hupati mtoto : Hii ni Game of Chance! Kwahiyo ni vyema ukaendelea kuwa na uvumilivu na kutafuta ushauri wa Madaktari wnegi zaidi - Kwa ushauri wangu, mpaka pale Daktari atakapowahakikishieni kuwa HAMUWEZI kupata mtoto/watoto ndio ufanye yafuatayo:
1. Chukua mtoto kutoka nyumba za watoto (orphanage) = Adopt
2. Jadili na mke wako kwa kina kuwa unadhamira ya kutoka nje na aridhie (ni ngumu sana hapa - hasa kwa wakristo)
3. Ishi hivyo milele mpaka mwisho wa maisha (waweza kuwachukua watoto wa ndugu na ukakaa nao kama wanao)
Pole sana - Hii hali huwa ni mtihani mkubwa na inahitaji uvumilivu wa kupita kiasi
Kaka hapa umenigusa, kumbuka watoto ni rizki kama unavyopata ugali, na mungu amesema katika vitabu vitakatifu ya kwamba nitawapeni watoto wakike na wengine wakiume watupu, na wengine nitawachanganyia wakike na wa kiume, na wengine watakosa kabisa.
Hivyo kumbuka hakuna kaburi la mgumba. Omba mungu na atakusaidia mungu hashindwi na kitu miaka 3 ni kidogo sana, kuna watu wamekaa miaka 13 na zaidi na walifanikiwa kupata watoto.
Mpende mkeo na usimnyanyapae kwa kukosa kuzaa kwani ukumbuke na yeye anamuhitajia sana huyo mtoto. Mwisho usizini kama vipi oa mke mwengine wa halali lakini mkeo wa kwanza no kumuacha (kama nabii ibrahimu aliomba dua na akapata watoto uzeeni basi hilo kwake mungu kwako ni dogo,amka usiku uone utukufu wa mungu