Miaka Miwili Baada ya Kifo Cha Balozi Abass Sykes

Miaka Miwili Baada ya Kifo Cha Balozi Abass Sykes

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
Nimeandika mengi hapa kuhusu Abbas Sykes.

Mengi sana.

Atakae kumjua Abbas Sykes atafute tu hapa na kwengineko ataisoma historia yote ya kupigania uhuru wa Tanganyika kwa undani wake.

''Hesabu yangu ya wanachama watatu waliobakia wa siku za mwanzo za TANU na harakati za kudai uhuru mwaka wa 1954 imepungua baada ya kufariki Abbas Sykes.

Yawezekana sana kuwa bado wapo waasisi wengi wa TANU walio hai lakini hawajulikani.

Daftari langu limebakia na Mama Maria Nyerere na Mzee Athmani Matenga wa Magomeni Mwinyimkuu.''

''Abbas Sykes alinambia, ‘’Nilimwambia Dossa lazima ahudhurie mkutano wa Kizota na nilihakikisha hilo.

Nilimwambia tutaondoka pamoja kwenda Dodoma kwa hiyo nilimnunulia nguo na viatu.’’

Balozi alinieleza maneno haya kwa shida sana na kwa hakika niliona kuwa historia ya Dossa ilikuwa imemuumiza sana.''

''Hapo King's College Budo ndipo Abbas Sykes ailipokuja kusoma na Freddie Mutesa ambae baadae akajakuwa Kabaka wa Buganda na Rais wa Uganda mwaka 1962 Uganda ilipopata uhuru.

Balozi Sykes anakumbuka kumuona mama yake Freddie Mutesa akiwa kavaa yale magauni ya Kiganda akija shule kumtembelea mwanae na jinsi shule nzima ilivyokuwa ikitetemeka kwa ujio wa bi. mkubwa yule kwani Freddie ndiye aliyekuwa akitegemewa kuwa Kabaka wa Uganda.''

''Ananihadithia safari yake ya London akiwa Mwenyekiti wa ATC alipokwenda kuchukua mwili wa ndugu yake, kama alivyomwita mwenyewe, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Abbas Sykes kamjua Nyerere mwaka wa 1952 na Nyerere alipoacha kazi ya ualimu akaja kuishi nyumbani kwa Abdul Sykes wakati wanamtafutia makazi yake.

Kifo cha Mwalimu na Abbas Sykes yumo ndani ya ndege ya ATC analiangalia jeneza la Nyerere.

Hili lilimrudisha nyuma sana wakati wako katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Fikra zake zilikarudi nyuma sana wako Mnazi Mmoja katika mkutano wa TANU yeye kijana wa kiasi cha miaka 24 hivi ikamjia picha Nyerere kaishiwa maneno anamwambia Bi. Titi, ''Titi hebu zungumza wewe.''

''Abbas Sykes alinihadithia anasema Nyerere alikuwa akija Dar es Salaam kutoka Pugu kuja kuonana na kaka yake alikuwa anapanda basi moja la Muhindi likiitwa ''Majigo.''

Kituo cha basi hili kilikuwa Mtaa wa Msimbazi na Aggrey.

Ukiingia na mzigo ndani ya basi basi yule Muhindi utamsikia akipiga kelele, ''Majigo juu, majigo juu.''

Maana ya maneno haya ilikuwa, ''Mzigo juu.''

Yaani mizigo ipandishwe juu ya basi kwenye ''carrier.''

Hivi ndivyo basi lile lilivyopata umaarufu wake na kuishia kuitwa ''Majigo.''

Hiki kilikuwa kipindi kabla ya Nyerere hajajiuzulu ualimu.

Nyerere alikuwa akishashuka pale kwa Majigo atashika njia kuelekea Kariakoo Market ofisini kwa Market Master Abdul Sykes.''

1684162662708.jpeg
 
Kuna Sykes mmoja anaitwa Abraham kama sikosei alikuja kuwa Meya wa Dar wakati wa Mkapa...alikuwa ni mtoto wa Sykes yupi?
 
Interesting history
The Boss,
JVM anasema amekuja Dar es Salaam mara ya kwanza mwaka wa 1957 na alifikia nyumbani kwa Abdul Sykes.

Kleist alikuwa mtoto mdogo wa miaka saba.

JVM anasema Kleist alikuwa akimvusha barabara ya Kitchwelle wanakwenda Amana Cinema, Ilala kuangalia movie ''Shane'' ya Audie Murphy.

Hii movie ilipendwa sana wakati wetu.
Itafute YouTube uiangalie.

JVM alinipa stori hii siku ya maziko ya Kleist.

Nakuwekea picha hapo chini unione mimi na Kleist na WMM na rafiki zetu wengine kama tulivyokuwa 1968:

1684253134926.jpeg

Kulia: Mohamed Said, Yusuf Zialor, Kleist Sykes, Bubby Bukhari, Abdallah Tambaza
Waliochutama Kulia Abdul Mtemvu, Wendo Mtiga Mwapachu, Kaisi
Picha hii tulipiga nyumbani kwa Mama Mary Mackeja mama yake sasa Chief Edward Makwaia wa Siha kama miezi mitatu hivi baada ya kifo cha uncle Abdul Sykes ilikuwa party tunamuaga Liliane Abbas Sykes anakwenda shule Ufaransa.
Chief Makwaia na Lily mama zao ni ndugu.
The Boss hawa ni katika jamaa zako lazima ujue historia yenu.
 
Napenda sana kuwajua hawa
Edzane,
Huu ukoo wa Sykes wana historia kubwa sana.

Mimi babu yangu Salum Abdallah alikuwa akifanyakazi Tanganyika Railways na Kleist Sykes na walikuwa majirani Mtaa wa Kipata (sasa Mtaa wa Kleist Sykes) 1920s.

Mke wa Kleist Bi. Mluguru bint Mussa na mke wa babu yangu Bi. Zena bint Farijala (nyanya yangu) walikuwa mashoga na watoto wao (Salum, Humud, Sikuzani, Abdul, Ally na Abbas) wakicheza pamoja na wakisoma shule moja Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika katika miaka ya 1930s.

Shule hii ilijengwa na babu zetu (Kleist Sykes, Mzee bin Sudi, Ali Said Mpima kwa kuwataja wachache) na ipo hadi leo ingawa imetaifishwa na serikali baada ya kuvunjwa kwa EAMWS na kuundwa BAKWATA 1968.

Babu zetu ndiyo walioasisi African Association 1929 na Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) 1933 na ndiyo waliyojenga jengo lililokuja kuwa ofisi ya AA kisha TAA palipozaliwa TANU 1954.

Leo hapo kuna jengo la CCM.

Inasikitisha kuwa ndani ya jengo hili hakuna hata picha moja ya kumbukumbu ya babu zetu.

Mimi ni sehemu ya historia ya hawa babu na baba zangu akina Abdul Sykes na ndiyo kisa nikaijua vyema historia ya uhuru wa Tanganyika.

Julius Nyerere alipokelewa Dar es Salaam na mchanganyika wa hawa babu zangu akina Schneider Plantan na watoto wao akina Abdul Sykes ambao ni baba zetu.

Sisi miaka ya 1950 ni watoto wa wadogo kabisa lakini tumekua tukiona historia yote ikifunguka machoni petu na tukisikiliza mengi waliyokuwa wakihadithia wazee wetu.

Unaweza kusoma kitabu hicho hapo chini kwa mengi kuhusu kizazi hiki kilichopigania uhuru wa Tanganyika:

1684254362517.jpeg

1684255156529.jpeg

Al Jamiatul Islamiyya Muslim School ilijengwa kona ya New Street na Stanley Street 1936 safari ya kwanza ya Nyerere UNO 1955 hafla ya kumuaga ilifanyika ndani ya jengo hili.

1684255460413.jpeg

Mzee bin Sudi alikuwa katika uongozi wa uliojenga jengo la AA (1929 - 1933) uongozi wa Al Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika uliojenga jengo shule ya Al Jamiatul Islamiyya Muslim School 1936.

 
Back
Top Bottom