Miaka miwili ya Rais Samia Suluhu

Miaka miwili ya Rais Samia Suluhu

kalacha mateo

Senior Member
Joined
Sep 27, 2021
Posts
119
Reaction score
240
CHARLES JAMES SHANKLY

MIAKA miwili. Yes miaka miwili ya Mwanamke na Mama ambaye ameibeba Tanzania katika mazingira magumu na kuivusha.

Miaka miwili ya kunyooshewa kidole na wahafidhina lakini akawaumbua.

Miaka miwili ya Mwanamke kutoka Zanzibar, Mama na Jemedari mwenye maono chanya kwa Taifa hili la Nyerere na Karume.

Miaka miwili ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Alipotuambia Kazi Iendelee hatukumuelewa, alipotuambia ataliponya Taifa hatukumuelewa, alipotuambia ukimzingua atakuzingua pia tulimshangaa.

Leo! Leo ni wote tunahubiri habari njema, nzuri na za kupendeza za Mama huyu.

Watumishi wa umma wamefunikwa na tabasamu lenye sura ya Mama Samia kwenye nyuso zao.

Madaraja takribani 190,000 yamepandishwa, tunavyozungumza hakuna mtumishi wa umma anayedai malimbikizo yake, mishahara imepandishwa kama alivyoahidi.

ELIMU: Hapa ndio usiseme kwa mara ya kwanza Shule zimefungiliwa Januari na hakuna Mzazi aliyechangishwa fedha za madawati wala madarasa.

Mama Samia kwa upendo wake ameamua kubeba mzigo wa Watanzania kwenye Elimu.

Amejenga madarasa 8,000 pamoja na samani zake Nchi nzima hapa sijazungumzia fedha za uviko-19 ambazo pia ziligawiwa kwenye Halmashauri kwa ajili ya miradi ya elimu.

Kwenye sekta ya utalii wote ni mashuhuda, Filamu ya Royal Tour aliyoifanya inajadiliwa Duniani kote na kwa hakika imeongeza idadi kubwa ya watalii wanaomwagika kuja nchini.

Mama Samia anaponya, huamini? Waulize wapinzani. Kero yao kuhusu mikutano ya kisiasa imemalizwa.

Mama ameruhusu, fanyeni mikutano mtakavyo, fanyeni maandamano mtakavyo ni haki yenu kikatiba kaondoa zuio lililokuepo.

Rais wetu ni mwerevu na mwenye busara hivi Karibuni katangaza wafanyabiashara wanaonzisha biashara mpya watafanya biashara zao kwa miezi sita hadi mwaka mmoja bila kulipa Kodi.

Maana yake anarahisisha na kufungua mianya kwa watanzania wengi kuanzisha biashara zao.

Sijagusia kwenye sanaa namna ambavyo wasanii wanapata mirabaha yao na kuanza kukopesheka hadi kiasi cha Sh Milioni 40.

Sijagusia michezo ambapo tunaona anavyomwaga fedha za hamasa kwa Simba na Yanga kwenye michuano ya kimataifa.

Hatujaziba masikio, tumesikia pia kuwa Serikali inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ndio itakayomlipa mshahara Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa 'Taifa Stars'.

Sijasahau kwamba Rais Samia amefungua mipaka yetu, amefungua nchi yetu kimataifa sasa tunazungumza na wenzetu Lugha moja, hatujajifungia kama kisiwa.

Ni miaka miwili tu, miaka miwili yenye bahati ya kuongozwa na Mama, Bibi na Dada yetu.

Jina lake Samia mwenye Suluhu.

0683 015145
Tanzania-president-Samia-Suluhu-Hassan-2022.jpg
 
Uongo mbaya Mama kapiga kazi nzuri, Kajitahidi ILA:

1. Kikotowo hakifai

2. Kukatika kwa maji na umeme ni embarassment. Mwezi November mwaka huu kukitokea mgao mwingine itakua aibu yake:

3. Kufukuza wamachinga kwa staili ile ni mbaya sana.

4. Deni la Taifa linazidi kuwa kubwa sana.

5. Bei za vifurushi vya simu iko juu mno.

6. Gharama za maisha, mfumuko wa bei na bei za vyakula ziko juu sana.

7. Mafisadi wanakula nchi bila kunawa, kuna upigaji wa kutisha kwenye halmashauri.

8. Kuwaondoa wamasai kibabe kule Loliondo ili kuiacha ile kampuni ya kiarabu ya OBC ipate eneo kubwa la shughuli zake ni aibu.
 
Back
Top Bottom