Miaka ya 2000 mwanzoni UKIMWI ulikuwa tishio, ule wakati ulikuwa ukipata slim unageuka kuwa kama zombi huku watu wakikuhesabia siku. Tusichukulie poa

Eli Cohen

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2023
Posts
4,460
Reaction score
13,715
Nakumbuka hata neno ukimwi likitajwa ,moyo wako unaenda mbio sana maana ilionekana ni mtoa roho. Hata kuna jamaa walikuwa wakikonda ghafla kidogo walikuwa wakihusishwa kuwa na ngoma.

Yani ilikuwa ukipata hili dude haukai sana, hata familia yako inakataa kukuhudumia wakidhani hata kukugusa tu na wao wanaupata.

Watu wengi walikuwa wanasema ukimwi umeletwa na Mungu kwa sababu ya hasira yake juu yetu ndio maana hauna tiba.

Ulifyeka watu kwa kasi sana kupelekea karibia kila nyumba kuwa na mwanajamii, jirani, ndugu, etc anaeumwa ukimwi. Duh ilikuwa tishio, watoto waliachwa yatima wengi sana kupelekea ongezeko kubwa la watoto wa mtaani in early 2010s.

 
Kilichosaidia ni dawa. Na hivi dawa za misaada ya Marekani zinaondolewa, tusipojipanga huu UKIMWI unaweza kurudi.
 
A.k.a mimi
Natesa sana ninapokuingia mwilini
Akina gono, kaswende
Wote baba yao mimi
Amini mimi ndio kubwa la maadui
Na leo nakuja kwako
Usizuhe kama hunijui
Ukiingia kwenye ukoo wenu ni km jini utatembea kizazi na kizazi hautoki ng'o yaan km Bibi alikwenda nao basi kuna uwezekano mjukuu kwenye rukaruka akanasa
 
it is re-coming soon, maana ARV zitakuwa za kulipia cash for life, TRUMP Kama akifanya kweli kutubania, maana ARV zilikuwa full funded na "U.S. President's Emergency Plan for AIDS Relief" (PEPFAR)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…