Michael B Jordan na Taraj P Henson wanauhusiano gani na kiswahili?

dramaqueen1

Senior Member
Joined
Apr 23, 2018
Posts
115
Reaction score
111
Majina ya nyota hawa wawili wa hollywood yananifanya niwaze kwa sauti kutokana na kuwa na uhusiano na lugha ya kiswahili

Michael B Jordan ambae jina lake limekuwa likifananishwa na mcheza basketball maarufu Michael Jordan, amefunguka akisema kuwa jina lake yeye ni Michael B Jordan, herufi B ikiwa inasimama badala ya jina la kiswahili Bakari likiwa na maana ya 'noble promise'

Anasema " B stands for Bakari, it's Swahili and it means noble promise"

Tuje kwa Taraj P Henson ambae jina lake kamili ni Taraj Penda Henson.

wikipedia inaandika kuwa "Her First and middle names are of swahili origin, Taraj means 'hope' and Penda means 'love' "
'_
Nawazaje kwa sauti?
Ni kuwa huenda watu hawa wazazi wao au bibi zao walihamia America kutokea East Africa(hasa Tanzania) na wakabadilisha identity zao na kuwa za huko maana majina yao ya kiswahili yananikanganya, tena Michael B Jordan ana Dada aitwae Jamila ( jina limekaa kiswahili kabisa), dictionary.com inafafanua jina Jamila kuwa " a female given name from a Swahili word meaning 'beautiful'

Kiukweli hawa Waamerika wenye majina ya kiswahili wamenikanganya kunifanya Niquestion originality identity zao.
 
Duh hata hatujamjibu mtoa mada!

Niliwahi kufanya kazi na dada mmoja anaitwa AMANI. Mahali nilipokuwa, niliposikia hilo jina tu nikajiaminisha huyu atakuwa mbongo mwenzangu. Sikutegemea angekuwa wa kike. Baada ya mazungumzo na yeye aliniambia hilo jina alipewa tu na mama yake na wala hana connection yoyote na huku kwetu.

Mwingine ni bibi wa kizungu ambaye binti yake anaitwa MALAIKA. Anasema alipata uja uzito wakiwa Arusha na mumewe. Wakati huo wimbo ule wa "manalika, nakupenda malaika.." ulikuwa unavuma sana. Hivyo alipojifungua akamuita bintiye hivyo.

Mtoa mada, huenda majina ya uliowataja yanatokana na mojawapo ya sababu hizo. Labda kwa kuwa umeanza utafiti umalizie tu huko huko google na ukipata jibu uje utufahamishe zaidi.

Sidhani kama kuna uhusiano wa majina yao na ancestors wao. Wengi wa watu wetu hawakupelekwa Marekani. Walikwenda Uingereza.
 

Humu watu hawakosi cha kujibu yaani, na ukiona wanaweka komedi ujue majibu hawana.

Ila haya majina yanakuwa na coincidence nyingi, mimi kuna Mzungu Tumefanya naye kazi PWC anaitwa David Tarimo, yaani ni full mzungu, ukijoin unaweza kudhani ni mchaga, ukija kumwona sasa ni mbali mbali hata kiswahili hajui kabisa.

Tulipewa story ya hilo jina ila siikumbuki ilikuwaje.
 


Hahahaha TARIMO kabisa!??? aisee hiyo kali kuliko...

Aisee umenikumbusha AMANI. Ngoja nimtafute sijui atakuwa wapi yule binti. Alikuwa mzuriiiii. Nimshawishi abaki bongo tu.
 
Umeona eee,kuna taraji na kuna yule sijui nani nimemsahau jina kwenye how did i get married yupo ana mdomo sana hata kwenye empire yupo ndo dadake taraj,kwenye desperate house wives yupo yaani ni kivuruge jamani,hawa mentor na don c wasitutoea kwenye mstari wale ni ndugu zetu kabisa
Tena atakua mpemba yule
 
Nilikutana na mmarekani mweusi mmoja huko kwao anaitwa "Kijana". Nilipomwuliza alisema mama yake alilipenda tu hilo jina jina mama yake alimwambia maana yake ni "handsome boy"....
Mama mkali, kamdanganya mwanae maana_
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…