Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 33,679
- 49,841
Kuna kipindi nilipitia wakati mgumu, wa kuuguza watu wangu wa karibu wawili kwa wakati mmoja, na ikapelekea hali ya kuyumba kiuchumi. Kwa sababu pia matibabu yao yalikuwa yako juu.
Nilikomba mpaka senti ya mwisho; hakuna rafiki, kikundi, wala ndugu aliyejigusa. Wengi walikaa mbali na mimi, zaidi ya kuniambia pole tu, Mungu atakusaidia.
Ikafikia mpaka hatua za kutaka kuuza rasilimali zangu; kilichonisaidia, ilibidi nikope bank ili kuweka mambo sawa. Bahati nzuri, hicho kipindi kikapita, ingawa nilipoteza mmoja kati ya wale niliokuwa nawapambania.
Baada ya muda nikawa nimerudi kwenye mstari; sasa changamoto inayojitokeza, ni baadhi ya vikundi kuniletea kadi za michango; mara mchango wa jengo la kuabudia, mara jumuia, mara harusi, mara shida mbali mbali n.k
Sasa najiuliza, mimi ndio natakiwa kutoa tu na si kusaidiwa pale na mimi ninapotaka uhitaji?
Kwa kifupi wakuu, mi sitoi mchango, na wala sichangii chochote, ni bora hiyo hela nikapige bia pamoja na mtoto mrembo pale kwa mangi maisha yaendelee.
Waniite mbahili powa tu, lakini chakula cha muumba ni sala na si hela.