Michango kwenye misiba ya wasanii inatoa somo zito kwa serikali na wasanii

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2012
Posts
14,588
Reaction score
32,361
Wakuu tangu jana baada ya kusoma taarifa za kuugua kwa msanii Haitham Kim (R.I.P) na bahati mbaya leo kufariki nimejikuta nikitafakari sana mambo mengi. Nimejitafakari mimi binafsi, familia yangu, wasanii na watanzania wote kwa ujumla kuhusu ishu za afya na kujikuta nikisononeka. Ila wakati nikiwa nasononeka nikajikuta nimesoma habari ya NEMC kuhusu watu kutochimba dawa na kujikuta nimekasirika sana na kuamua kuandika huu uzi.

Kwanza kabisa nitoe pole kwa Ndugu Niiteboshen kwa kuondokewa na mkewe kipenzi. Pia nawapa pole ndugu, jamaa na wadau wote wa tasnia ya muziki. Haitham katangulia na lazima sisi wote tumfuate. Uwe CCM, uwe mnufaika wa michango ya Join The Chain au uwe msanii mkubwa ni kuwa lazima ipo siku turudi mavumbini. Kwahiyo kila kitu fanya kwa kiasi. Lakini je, hivi vifo vinavyotokana na matatizo ya kiafya hayawezi kushibitiwa angalau watanzania tuongeze life expectancy? Hata kama kifo hakitabiriki lakini kuna wajibu wa sisi binadamu kutimiza katika kuepusha vifo.

Nikianza na wasanii ni kuwa mitandaoni tumeona mkilaumiwa kuishi maisha feki ila wakati wa maradhi mnaanza kutembeza bakuli. Hii hoja ina nguvu ila mimi kwa upande wangu siizingatii kwasababu ni muhimu kumsaidia mtu akiwa kwenye maradhi bila kujali alikuwaje wakati akiwa mzima. Ila mimi ninawasihi wasanii kuwa haya maisha yenu mnayoishi wengi wenu ni ya kipuuzi na kutojali afya zenu.

Wasanii wengi mmejikita kwenye vitendo vya ngono na anasa za kishenzi kama vile uvutaji wa shisha, bangi na vitu vingine vyenye madhara kiafya. Wengi wenu huwa tunaambiwa "fulani ni mgonjwa kwa muda mrefu sasa tunaomba mchango"... ila kiukweli huwa tayari mnakuwa mko kwenye lile gonjwa lisilotibika. Hili wala tusibishane. Wasanii wa bongo na ngono ni chanda na pete.

Wenyewe wanaita kudanga.. msipoacha upuuzi hili tatizo la kuomba kuchangiwa halitaisha. Haiwezekani unakuta msanii huyu leo yuko na huyu haipiti hata miezi 6 wameachana kahamia kwingine. Uchafu ni mwingi sana. Ukitoa ngono kuna wasanii wengine huteseka kwa magonjwa yanayosababishwa kwa matumizi ya vitu haramu kama shisha, bangi, pombe na madawa ya kulevya.

Kwa upande wa serikali pia nako kuna tatizo. Mimi siridhishwi na mipango ya wizara ya afya. Waweke juhudi zaidi kuwekeza kwenye afya na kuelimisha raia kuhusu mambo ya bima za afya. Bado raia wengi wakiwemo hao wasanii hawana bima za afya kitu ambacho sio sawa.
 
Wasanii si wanapesa nyingi kwanini wasimfate uwoye au Shishi asolve

Malipo ya matibabu ya huyo msanii.

Tatizo wasanii wa bongo wakishazidiwa utasikia.

Michango ,na kwa style ya maisha yao wanayo onesha mitandaoni kukoga pesa watu hawawezi kuwachangia

Ova
 
Uwe CCM, uwe mnufaika wa michango ya Join The Chain au uwe msanii mkubwa ni kuwa lazima ipo siku turudi mavumbini. Kwahiyo kila kitu fanya kwa kiasi.
Walishakuambia CCM hawafi kamwe!! Wangekuwa wanakufa ufisadi ungekuwa ulikwisha pamoja na wanaokufa
 
Wakuu tangu jana baada ya kusoma taarifa za kuugua kwa msanii Haitham Kim (R.I.P) na bahati mbaya leo kufariki nimejikuta nikitafakari sana mambo mengi. Nimejitafakari mimi binafsi, familia yangu, wasanii na watanzania wote kwa ujumla kuhusu ishu za afya na kujikuta nikisononeka. Ila wakati nikiwa nasononeka nikajikuta nimesoma habari ya NEMC kuhusu watu kutochimba dawa na kujikuta nimekasirika sana na kuamua kuandika huu uzi.

Kwanza kabisa nitoe pole kwa Ndugu Niiteboshen kwa kuondokewa na mkewe kipenzi. Pia nawapa pole ndugu, jamaa na wadau wote wa tasnia ya muziki. Haitham katangulia na lazima sisi wote tumfuate. Uwe CCM, uwe mnufaika wa michango ya Join The Chain au uwe msanii mkubwa ni kuwa lazima ipo siku turudi mavumbini. Kwahiyo kila kitu fanya kwa kiasi. Lakini je, hivi vifo vinavyotokana na matatizo ya kiafya hayawezi kushibitiwa angalau watanzania tuongeze life expectancy? Hata kama kifo hakitabiriki lakini kuna wajibu wa sisi binadamu kutimiza katika kuepusha vifo.

Nikianza na wasanii ni kuwa mitandaoni tumeona mkilaumiwa kuishi maisha feki ila wakati wa maradhi mnaanza kutembeza bakuli. Hii hoja ina nguvu ila mimi kwa upande wangu siizingatii kwasababu ni muhimu kumsaidia mtu akiwa kwenye maradhi bila kujali alikuwaje wakati akiwa mzima. Ila mimi ninawasihi wasanii kuwa haya maisha yenu mnayoishi wengi wenu ni ya kipuuzi na kutojali afya zenu.

Wasanii wengi mmejikita kwenye vitendo vya ngono na anasa za kishenzi kama vile uvutaji wa shisha, bangi na vitu vingine vyenye madhara kiafya. Wengi wenu huwa tunaambiwa "fulani ni mgonjwa kwa muda mrefu sasa tunaomba mchango"... ila kiukweli huwa tayari mnakuwa mko kwenye lile gonjwa lisilotibika. Hili wala tusibishane. Wasanii wa bongo na ngono ni chanda na pete.

Wenyewe wanaita kudanga.. msipoacha upuuzi hili tatizo la kuomba kuchangiwa halitaisha. Haiwezekani unakuta msanii huyu leo yuko na huyu haipiti hata miezi 6 wameachana kahamia kwingine. Uchafu ni mwingi sana. Ukitoa ngono kuna wasanii wengine huteseka kwa magonjwa yanayosababishwa kwa matumizi ya vitu haramu kama shisha, bangi, pombe na madawa ya kulevya.

Kwa upande wa serikali pia nako kuna tatizo. Mimi siridhishwi na mipango ya wizara ya afya. Waweke juhudi zaidi kuwekeza kwenye afya na kuelimisha raia kuhusu mambo ya bima za afya. Bado raia wengi wakiwemo hao wasanii hawana bima za afya kitu ambacho sio sawa.
Umesikika Mama
 
Nadhani hapo kwa miezi 6 kuachana nadhani kajala atakuwa amekuelewa vilivyo
 
Wanaambukizana kijinga halafu baadae kuja kutulilia huku wakijua wana magonjwa yasiyotibika. Yaani kila msanii lazima apatwe na gonjwa baya kabisa.
 
Kweli haya maisha ni kujipanga,kuishi maisha feki si uungwana kabisa.
 
Back
Top Bottom