Michango maalum ya "harusi" kila mwezi kwa ajiri ya JF

Sabi Sanda

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2006
Posts
409
Reaction score
31
Wakuu,

Habari za mchana?. Pamoja na upya wangu katika JF, nimevutiwa kupita kiasi na JF inavyoendeshwa na jinsi wakuu mnavyochangia. Mtoto, Next LeveL, Original Pastor--Hongereni sana. Bila kuwasahau wengine wengi tu. Moderator MUNGU akubariki sana na uishi miaka aliyoishi Baba wa Imani.

Sasa Wakuu, kama shukurani kwa wana JF na jinsi mnavyoifurahisha akili na moyo wangu kila nisomapo posting zenu, pamoja na mchango wangu wa kila mwezi wa shilingi elfu 20 nilioahidi, naomba tuanzishe michango maalum ya kila mwezi kwa ajili ya JF. Naomba michango hii tuite MICHANGO YA "HARUSI" YA KILA MWEZI KWA AJILI YA JF. Kwa kuwa tuko zaidi ya 8000 naomba lengo letu la mwezi liwe ni kupata pledges na michango kutoka kwa wana JF wasiopungua elfu moja.

Kwa upande wangu naomba niahidi kutoa shilingi elfu 50 mwezi ujao wa 12 kama mchango wangu wa kwanza wa "HARUSI' kwa ajili ya JF.

Kwa upande mwingine napendekeza hii michango ya "HARUSI" iwe na akaunti yake maalum.

Naomba kuwasilisha na MUNGU azidi kuwabariki.

Salaam

Josephat S. Sanda
0712 540 415
Dar es Salaam
 
mkuu wazo zuri lakini mimi binafsi bado sijakuelewa kidogo hapo kwenye michango ya harusi, lengo ni kutaka wana JF wafunge ndoa pasina kuogopa gharama au ni vipi?, nifafanulie mkuu.
 
Dear George,

Hapana Mkuu. Nia nikupata fedha za kutosha kwa ajili ya kuiendesha JF yetu bila tatizo kuanzia Januari Mwakani, 2010.

Salaam

Sabi Sanda
 
Kuuita mchango wa harusi una maana gani?
 


Ndugu yangu nakushukuru kwa mchango wako mzuri wa mawazo.Wasiwasi wangu hili la kuchangia JF tu kwa ajili ya malipo ya kuiwezesha kuwepo inatushinda, sembuse mchango wa harusi!
 
Ndugu yangu nakushukuru kwa mchango wako mzuri wa mawazo.Wasiwasi wangu hili la kuchangia JF tu kwa ajili ya malipo
ya kuiwezesha kuwepo inatushinda, sembuse mchango wa harusi!

Kama nilivomuelewa, sio michango ya harusi ila ni ''Michango ya harusi'' akimaanisha kwamba Tuichangie JF na michango hiyo tuipe jina la ''Michango ya harusi''
 
Mlachake,

Mkuu, nakushukuru sana kwa ufafanuzi ulio SAWIA.

Wakuu, kama alivyopendekeza Next Level huko nyuma ni muhimu sana sasa tukaanza kutoa ahadi zetu thabiti za kuichangia JF kama tufanyavyo katika kuchangia HARUSI ZETU KILA UCHAO.

Salaam

Josephat S. Sanda
 
Kwa mawazo yangu nadhani umeona tatizo watanzania walilonalo la kuendekeza michango ya harusi na wengine mpaka wana lazimisha uwachangie. Nafikiri unataka kuona je, watu kwa kuona neno "harusi" basi michango itatiririka.....

Nakushukuru kwa message yako na naomba jamani watanzania tubadirike.......hivi mbona ukiwa unaumwa ukiomba msaada watu wala hata hawana habari......lakini tangaza tu unaoa/unaolewa......mpaka watu wataanza kuku uliza ......hivi sherehe ni lini ili wachange.

Kwa nini hiyo michango tusi iweke kwenye mambo ya maendeleo? Mfano ktk mtaa au hata marafiki ktk ofisi moja kwa nini msiweke michango ya aina hiyo kila mwezi ili muanzishe mradi wa maendeleo?? na huo mradi baadaye uwasaidie kusomesha watoto wenu na hata kuwa na mradi mdogo wa umeme au maji ktk mtaa au kijiji chenu??

Watanzania natamani wote mgekuwa na mawazo kama yangu.....harusi kwangu ni mimi na mtarajiwa wangu tutajuana padri kanisani basi!!!

Kwa mfano kituo kidogo cha umeme wa sola chenye uwezo wa kuhudumia familia 10 kwa mwanga, kuchaji simu, TV, na redio kina gharama ya TZS milioni 30. Hii ni gharama ambayo wananchi wakijiunga ktk maofisi au hata ktk biashara wanaiweza ni suala la kuweka malengo ya muda mrefu na mfupi. lakini utakuta mtaa mpya unakaa bila umeme miaka 5 eti wanasubiri TANESCO ambayo iko hohe hahe, na wakakti huo huo wananchangia harusi mpaka milioni 7 kwa mtu mmoja na wanakunywa pombe na kula ubwabwa.
 
Naomba kuwasilisha na MUNGU azidi kuwabariki.

Salaam

Josephat S. Sanda
0712 540 415
Dar es Salaam
Ni vizuri kama kila anayeahidi kuchanga aweke pia jina lake halisi na contacts kama alivyofanya mkuu Sanda !!
 
....anayeahidi kuchanga aweke pia jina lake halisi na contacts kama alivyofanya mkuu Sanda !!

Aweke jina kale halisi ili iweje? na kwa manufaa ya nani?
Unahakika gani kama jina lililotumika na anwani ni halisi?
 
Watu ni wagumu kuchangia mambo mengine meengi ya maendeleo ya mtu au kikundi cha watu.Inagharimu roho ya aina ya REGINALD MENGI flani!
Lakini kwenye michangi ya harusi tunatoa sana!
Kwa dhana ya mtoa mada, basi mchango huu uitwe wa harusi ili iwe ni Driving force ya ya kuwasukuma watu kuchanga!
 
Brilliant idea! hii imekaa vizuri sana kuliko ile ya kupambanisha Simba na Yanga.

Ngoja na mimi nijipapasen papase kutokana na mwelekeo wa ubebaji box nione naweza kuchangia ndawira ngapi
 

Naona mkuu SS umeipitia taratibu ile thread ya Sikonge.....''Changia JF mkono mtupu haulambwi''...In fact kila mmoja angepata muda wakupitia michango kny thread ile, wengi wangepata mwamko kama wa mkuu SS, kule wadau wengi sana walitoa mawazo mazuri sana ya namna ya kuiwezesha JF iwe hewani muda wote!

Tatizo mwamko umekuwa mdogo sana, response ya watu kny michango ya maendeleo ni ndogo sana, tunapenda sana mambo yanayokuja na kupita fasta, hatutaki sana kuchangia mambo yanaweza kuleta maisha bora kwa miaka 200 au zaidi ijayo...we just care about today not tomorrow! Hopeful kina Sanda wengi mkiongezeka na kuhubiri haya pengine wengi ''tutaokoka''! na kupenda kuchangia maendeleo sio kwa maneno tu bali kwa vitendo!

Sanda unapigia hesabu ya TZS 20,000 kwa kila mwezi, well kwa mtu anayeweza kumudu! Lakini sisi tulikuwa tunasuggest kila member achangie at least TZS 5000 kwa mwaka (8000*5000=40,000,000) sasa wakiwepo watu kama 500 kati ya hao wanoweza kutoa hata 50,000 kwa mwaka..maake unazungumzia extra money ya TZS 22.5mil..total TZS 62.5mil...hii si haba sana kwa kuifanya JF iwe hewani!

Lakini member tuliowengi kila kitu we turn into politics wakati kila siku tukiamka tunawaza kuingia kijiweni kubarizi.....kwa nini hatujiulizi, nani anagharamia JF kuwepo hewani kila siku na kwa faida gani hasa?
 
Ni vizuri kama kila anayeahidi kuchanga aweke pia jina lake halisi na contacts kama alivyofanya mkuu Sanda !!

"kuchangatutachanga lakini si kutajana majina alisi, tusije tukarudi kule kule kwa hosea na wabunge"
 
Dear Next Level & Wengine Wengi Wana JF;

Nawashukuru sana. Binafsi nachukia sana utegemezi na ninakerwa kupita kiasi. Kuna kitU kinaitwa THE POWER OF NUMBERS (Sanda, July 2003). Kizuri ni kuwa MUNGU ametupa hiyo nguvu ya ajabu na tunayo kwa kiwango cha kutisha. Tuko zaidi ya ELFU NANE na tunaendelea kuongezeka kila UCHAO. Hebu fikirieni tukiipeleka JAMIIFORUMS katika SHULE ZOTE ZA SEKONDARI HAPA NCHINI NINI KITATOKEA--ziko 4102 (MoEVT, July 2009). Someni the BEST BOOKLET OF JULY 2009. Naomba Sana Tuingie Kazini. Angalau Kila Mmoja Wetu Aweke Lengo la Kuchangia sio chIni ya Shilingi ELFU TATU KILA MWEZI ILI TUONE KITAKACHOTOKEA---ZABURI YA 23 NA MITHALI 20:1.

SIKU NJEMA KWENU WOTE NA SALAAM KWA FAMILIA ZENU NA WAPENDWA WOTE MLIO KARIBU NAO.

Salaam

Josephat Sabi Simon Sanda (JSSS)
Dar es Salaam
Tanzania
0712 540 415
---------------------------------------------------------------------------------
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…