Michango shule ya sekondari Borega

Michango shule ya sekondari Borega

Mausingizii

Member
Joined
Jul 14, 2022
Posts
90
Reaction score
74
Shule ya sekondari Borega ,iliyoko mkoani Mara ,Musoma vijijini kwakweli imezidisha michango kwa wanafunzi mpaka kero.

Cha kushangaza tunapofanya malipo wanafunzi hawarudi na risiti, tulitangaziwa kusitishwa kwa ada kwa wanafunzi wa Elimu ya juu ,lakini form six wa awamu hii bado wanalipa kwa kigezo kuwa ilikuwa ishakuja oder ya malipo ,mara cjui nn.

Mfano, tulilipa sh 105000 lakini bado kuna 30000 ya vifaa vya maabara ikidaiwa kuna watu walikamatwa na stop watch hivyo form six wote walipe, 16000 ya mitihani na bado tunadaiwa 30000 ya ada cha kushangaza imeongezeka tena sh 12000 ya vifaa vya maabara na michango kede kede .

Wanafunzi wanapitia mazingira magumu, Mara waambiwe hawatofanya mitihani, Mara watabaki baada ya kumalizika kwa mitihani. Ukiwapigia wahausika hawana majibu ya kueleweka ,jmn naomba Muongozo tukalalamike wapi, wenye maisha ya kuunga unga.

Pia naomba wenye mamlaka mlifuatilie suala hili ,na nieleweshwe km kuna malipo pasipo risiti.
 
Back
Top Bottom