[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading"]Daktari: Je, minyoo inasababisha kuwashwa sehemu ya haja kubwa?[/TD]
[TD="class: buttonheading, align: right"][/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD]KUSIKIA muwasho sehemu za haja kubwa si jambo geni kwa wengi na pengine wewe unayesoma makala hii ulishawahi kupatwa na tatizo hili.Hili ni miongoni mwa matatizo ambayo husumbua kwa mda mrefu na pengine bila kupatiwa matibabu, kwani watu huona aibu kusema kwa vile ni sehemu nyeti ya mwili wa binadamu.
Wakati mwingine ule muwasho husumbua ukiwa katika kadamnasi, hivyo inabidi mhusika kwenda sehemu ya faragha kujikuna, kwani kufanya hivyo kwenye kadamnasi humfanya ajisikie aibu.Hata wale wanaomuona mtu akijikuna maeneo nyeti kama hayo hushangaa kwa kuwa si jambo la kawaida. Ukweli ni kwamba katika maisha binadamu inatokea kuwashwa sehemu ya haja kubwa.
Minyoo na muwasho
Sababu za kuwasha sehemu ya haja kubwa ni nyingi; lakini leo nitajibu swali la msomaji linalohusiana na minyoo na hasa ile ya tumboni.
Sehemu ya haja kuwa ni sehemu ya mwisho kabisa ya utumbo mpana ambayo hupitisha kenyesi kutoka tumboni. Ni kweli kabisa kuwa kuna minyoo inayosababisha kuwasha sehemu hii. Minyoo hii pengine ulishaiona kwa macho kwani ina rangi nyeupe na wakati mwingine utaona imeshika kama utando kwenye makalio ya nyuma ya mtoto au miguu yake kwani inaweza kutoka tumboni yenyewe.
Kwa kiingereza minyoo hii ina majina kibao. Wengine huiita ‘pinworm', ‘seatworm' au ‘threadworms'. Kwa jina la kitaalamu minyoo hii hutwa ‘Enterobius Vermicularis'.
Tatizo la minyoo hii huwakumba watoto wa shule na wale wanaokaribia kuanza shule zaidi. Unaweza kukuta nusu ya wanafunzi wana minyoo hii kwa sababu inaambukiza na kwenye familia wanaweza kuwakumba watu zaidi ya mtu mmoja.
Si kawaida kwaingia watu wazima ila unawaza kuukuta kwa mama mzazi wa mtoto mwenye minyoo. Pengine kwa sababu ya mahusiano ya mama na watoto kuwa karibu (kama kumuogesha mtoto nk).
Minyoo inaambukiza kwa njia ya kinywa. Mayai ya minyoo kutoka haja kubwa yanaweza kuishi kwa muda wa wiki mbili kwenye ngozi, nguo, taulo, shuka, blanketi; hivyo ni rahisi kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine na hasa kama atakula bila kunawa mikono.
Tofauti na minyoo ya aina nyingine, ugonjwa huu zaidi ya kuwasha sehemu ya haja kubwa na ukeni kwa wanawake, mara chache sana kuumwa tumbo, kukosa hamu ya kula na kukosa usingizi.
Sababu zingine za kuwashwa sehemu ya haja kubwa ni fungusi, viotea au heamorrhoiss, choo ngumu, kula viungo vikali ikiwemo pilipili kwa wingi.
Tunashauriwa kuhakikisha kuwa tunanawa kwa sabuni kabla ya kula. Tuwe na tabia ya kuwafanyia watoto uchunguzi na kuwapa dawa za minyoo angalau kila baada ya miezi mitatu, kufanya usafi wa nguo, taulo na mashuka mara kwa mara.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]