Na mimi na familia yetu zile milioni 2 nilizotuma kwa njia ya voda pesa sijui mumezipata? Sio baada ya uchaguzi kuisha mujekutuambia majambazi yalivamia hazina ya chadema na kutoroka na pesa zote!!!
Hata kama mimi sio chadema lakini nadhani naruhusiwa kuchangia maana hata yule mhindi wa ccm si alichangia milioni 100?
Sisi huwa tunachangia chama chochote kinapoomba msaada lakini sharti fedha zionekane zinafanya kazi! Sio mtu kama mbowe anaedaiwa mamilioni ya mkopo wa benki azitumie fedha zetu kulipia madeni yake! Kwa kweli mutaturudishia fedha zetu kama mutazifisidi maana binaadamu yoyote anaasili ya uroho!!
Hayo yameshatokea ktk nchi zilizoingia ktk uchaguzi na kuleta uongozi mpya matokeo yake ufisadi uliongezeka maradufu! Mfano, kenya, zambia, senegal,malawi, ethiopia,eritrea, nk. Hivyo chadema sidhani kama nyinyi ni malaika muliotumwa toka mbinguni tutawaamini vipi kama nyinyi hamna mafisadi?