Michango ya ujenzi wa madarasa imekuwa kero Kata ya Ubaruku, Rais Samia tusaidie

hito

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2018
Posts
501
Reaction score
913
Kwanza nikupongeze kwa mwaka mmoja wa kuwa madarakani binafsi naona Mambo yamenyoka kidogo tofauti na Serikali ya Awamu ya Tano ambapo Uhuru wa kujieleza ulibanwa kweli kweli.

Naomba niende kwenye keep yangu.

Mh Rais sisi wakazi wa wilaya ya Mbarali kata ya Ubaruku mkoani Mbeya tunaomba utusaidie hili suala la michango ya kujenga shule za msingi pamoja na sekondari.

Yaani imekuwa kero sana tunagongewa usiku kuamshwa kama wezi yaani ni usumbufu usumbufu.

Binafsi nimeshalipa ila kero ni kusumbuliwa usiku tunaamshwa kama tupo nchi ya Vita na wilaya hii michango haiishi kila mwaka tunachanga impact za hiyo michango ni kidogo sana.

Nikutakie majukumu mema Rais.
 
Hili ndilo tatizo la kutegemea mtu mmoja afanye kila kitu, kuna mkurugenzi wa halmashauri, kuna M/kiti wa halmashauri, kuna mbunge, kuna Diwani, kuna afisa elimu, kuna mtendaji kata nk.

wote hawa hawawezi kushughulikia tatizo hadi rais, Magufuli ametuachia msingi mbaya sana wa utawala.
 
  • Thanks
Reactions: _ly
Hili ndilo tatizo la kutegemea mtu mmoja afanye kila kitu, kuna mkurugenzi wa halmashari, kuna afisa elimu, kuna mtendaji kata nk.
Sasa Kama hawa nao hawajui majukumu yao na Kama wao ndio wanao watuma
 
Kwanza nikupongeze kwa mwaka mmoja wa kuwa madarakani binafsi naona Mambo yamenyoka kidogo tofauti na Serikali ya Awamu ya Tano ambapo Uhuru wa kujieleza ulibanwa kweli kweli.

Naomba niende kwenye keep yangu.

Mh Rais sisi wakazi wa wilaya ya Mbarali kata ya Ubaruku mkoani Mbeya tunaomba utusaidie hili suala la michango ya kujenga shule za msingi pamoja na sekondari.

Yaani imekuwa kero sana tunagongewa usiku kuamshwa kama wezi yaani ni usumbufu usumbufu.

Binafsi nimeshalipa ila kero ni kusumbuliwa usiku tunaamshwa kama tupo nchi ya Vita na wilaya hii michango haiishi kila mwaka tunachanga impact za hiyo michango ni kidogo sana.

Nikutakie majukumu mema Rais.
Kwani mnalazimishwa? Si mbakubaliana wenyewe? Watoto ni WA Samia au? Mna matatizo sio kidogo.
 
Hili ndilo tatizo la kutegemea mtu mmoja afanye kila kitu, kuna mkurugenzi wa halmashauri, kuna M/kiti wa halmashauri, kuna mbunge, kuna Diwani, kuna afisa elimu, kuna mtendaji kata nk.

wote hawa hawawezi kushughulikia tatizo hadi rais, Magufuli ametuachia msingi mbaya sana wa utawala.
Yaan ktu ambacho nilishakataa ktk maisha yangu ni kutoa michango aisee hata iweje hasha ya shule, hospital, sijui Nini hiyo sio Kaz yangu. Nalipa Kodi na michango nitoe watu wanaenda kula. Tundulisu alinifundisha kitu kikubwa sana. Hakuna mchango wa lazima. Ukishaweka lazima hiyo ni Kodi. Na Kodi Ina taratibu zake
 
Back
Top Bottom