Michango ya wana JF kuhusu Q-Net imeniokoa nisitapeliwe Mwanza

Hawa ni wengine wapo maeneo ya mkolani
Ila kuna dada na mume wake wao wana nyumba kubwa na gari range
Nao wanasema vitu vyao vyote wamepata kupitia Q-net na watu wameanza kuwaita freemason kwa wanavyodai na nilifika hadi hapo wanapo kaa kwasababu nilipelekwa na vijana wengi wanaenda ila wakaaminishwe juu ya mafanikio watakayo yapata
Ila hesabu zangu ziligoma kuweza kupata mtu wa kumshawishi afanye biashara ya 6M and ni kama Virtual na sio physical zaid
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ kikundi cha wehu haha β€œGood morning”! Yani mtu bado unatoa million 3! Walio wajinga wanaendelea kuliwa hakuna pesa bila kufanya kazi ni bora vikoba kuliko hao wehu wa good morning
Tuzidi kutoa maarifa tu mkuu ili na wengine wapate kuelewa mkuu
Bila kufanya hivyo watu wengi watakuwa gizani
 
Yani una bahati sana mkuu, hizi network marketing sio za kujihusisha nazo kabisa, zinafilisi na kulemaza ubongo.
 
Duuh nakumbuka hawa jama walikua na ofisi nje kwetu makumbusho 2018
Nikaulizia wakaniambia 4M
Sasaivi naona wamepanda mpaka 6M
Kiukweli kwa kipindi kile kilichobisaidia sikua na hio ela
Ila hao jamaaa ni wanaku manipulate unaona utajiri huu apa ,,, wana brain wash
Huyo ndugu yako mkuu mpaka umtoe hapo umuombee pia maana sio kawaida
 
Kumbe Qnet bado ipo mpaka leo.
 
Uko sahihi
Kuna kijana mmoja alitaka kunitapeli na hii Q Net Dar es salaam....walipanga nyumba mikocheni...halafu sebuleni hakuna hata viti...ukutani wamebandika leseni....imefubaa kwa kupigwa copy....watu wakiingia wanasimama pale sebuleni....wakisubiri kila mtu kuitwa na mjinga wake chumbani ili aweze kumpanga.......Sasa huyu kijana sababu namfahamu nikamuomba yeye anipe kiingilio manake ana uhakika na biashara yenyewe....cha ajabu anasema hana kitu....poa....wakati wa kutoka nikampiga mzinga....bado anazidi kulia...nikampa maneno mawili tu....mpaka leo sijamsikia yuko wapi.
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ kikundi cha wehu haha β€œGood morning”! Yani mtu bado unatoa million 3! Walio wajinga wanaendelea kuliwa hakuna pesa bila kufanya kazi ni bora vikoba kuliko hao wehu wa good morning
VICOBA ina msaada sana....lakini Q Net ni wasanii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…