Michango yote Yanga akabidhiwe Zahera

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Wanaoweza kuichangia Yanga wako wengi sana wa sh. 500 hadi 10,000 vijijini hadi mijini hasa kwa kipindi hiki ambacho timu haina hela lakini inafanya vizuri uwanjani. Huyu kocha ndiye nguzo kuu ya mafanikio tunayoyaona uwanjani hivi sasa, Yeye kwa sasa ndiye anaeyafahamu machungu wanayoyapitia wachezaji. Hata kumfukuza Kakolanya na kumvua Yondani unahodha anafanya hivyo kwa shingo upande tu kama ni sehemu ya mbinu za kujaribu kuyalinda mafanikio ya timu yake kwenye kipindi hiki cha mpito. Badala ya yeye kutumia mbinu kama hizi za kuwazuia wachezaji kuonyesha malalamiko yao hadharani. Watu tuna imani kubwa na kocha Zahera kwa mafanikio hayo, hivyo haitakuwa ngumu watu kuchangia kama Zehera atasimama hadharani yeye mwenyewe na kuwaomba wanachama, mashabiki, na wapenda soka wote popote walipo ndani na nje ya nchi waichangie Yanga kupitia Namba yake ya simu ya kiganjani au account yake bila kupitia kwa wababaishaji wengine wapiga dili.

Nina imani yeye akizipata hizo hela atazipeleka pale zinakotakiwa kwelikweli kwa wakati.
 
tunaipenda sana timu yetu tatizo mipango mibovu wanachama na mashabiki tuko tayari tatizo hakuna programme nzuri ya kuwahamasisha mashabiki ni jambo la kawaida kuchangia timu nashangaa eti watu wanasema ombaomba hivi ukuwa na watoto ukawaambia wakupe pesa utahesabika kuw wewe ni ombaomba
 
shida ni pale baba anapotumia vibaya pesa toka kwa wanawe kulewa hadi kubaki uchi, kununua uchawi ili kuwaroga wanawe hao wampe pesa zaidi.
 
Mifumo, mifumo, mifumo. Why always an individual not a strong institution? Wakahi aliyetuloga kafa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…