Michezo magazetini leo...

Status
Not open for further replies.
How Birmingham bucked the Midlands slump against United


By Mike Walters in Mirror Football Blog
Published 22:28 28/12/10







All of a sudden, the Premier League table reads like a ransom note in the Midlands.
West Ham are no longer the only clots in claret and blue because their patent has been copied, and translated into French, by Aston Villa.
Wolves are rock-bottom, West Bromwich Albion are sinking and now one of the great unsolved mysteries is what Birmingham City - beaten at home only once in 15 months - are doing up to their waists in the quicksand.
Carling Cup semi-finalists after sorting out the noisy neighbours, amid the friendly fire of exchanging flares and flying seats, before Christmas, Brum have learned to defend their fortress resolutely when the big guns come to town under Alex McLeish.


Not since January 2008, when Chelsea's goalscorer was Claudio Pizarro, had they lost at home to one of the top four, and Manchester United found the Blues a reliably tough nut to crack again.
McLeish was an accountancy student, the life and soul of balance sheets, when an Aberdeen manager named Alex Ferguson persuaded him to give up number-crunching in 1978 and join his crusade at Pittodrie.
That was the year in which Birmingham last beat United, although the 5-1 win at St Andrews did them a fat lot of good: they were relegated at the end of that season anyway.
Big Eck could never have imagined, when he turned his back on spreadsheets and forged Scotland's finest central defensive double act with Willie Miller, that his adventure with the Dons would lead to breaking the Old Firm's stranglehold and glory in Europe against Bayern Munich and Real Madrid.
So it was a pity that the master and his apprentice could not generate more entertainment between them as they exchanged pleasantries in fluent Glaswegian - subtitles available from all good linguists on Sauchiehall Street - on the touchline last night.
The most enjoyable aspect of the opening 45 minutes was that the fog lifted enough to afford us a decent view of the game; the most disappointing aspect was that the shroud didn't fall again and spare us an unimpaired view of such impoverished scuffling.
As ever, a man called Fergie called the tune - but this time, it was not the godfather of purple noses but Birmingham's industrious midfielder Barry Ferguson in charge of the jukebox.
When the Blues are on song, Ferguson is usually at the heartbeat of their endeavours - and whatever the league table may say, he need have no inferiority complex.
Oh, one other unsolved mystery in the land of strangled vowels: Why was Phil Mitchell from EastEnders refereeing last night's game under the pseudonym Lee Mason?
 
Why Villa stars must heed the fate of West Ham, Newcastle and Leeds if they think they're too good to go down


By Mike Walters in Mirror Football Blog
Published 11:59 29/12/10








Gerard Houllier is down to the last refuge of the terminally desperate in any relegation battle - that Aston Villa are too good to go down.
And on paper, he would be right: how can a squad brimming of internationals, a team who finished sixth three years running under Martin O'Neill, a club who went to Wembley twice last season, be in such a mess?
But make no mistake, Villa are not just in the thick of a relegation battle now. They are in danger of being grounded, like an oil tanker when the tide goes out, after their next four games, which carry all the promise of a ransom note.
Chelsea away? Piece of cake (for Carlo Ancelotti). Sunderland at home? Three points for the taking (if your name's Steve Bruce). Birmingham at St Andrews? Draw the curtain, nurse, Monsieur Houllier is feeling a little giddy. Manchester City at home? Well, Villa softened them up nicely at Eastlands, didn't they?


Don't tip all the blame on Houllier. He is a manager of integrity and pedigree. You don't win three cups in one season at Liverpool by throwing the jigsaw pieces in the air and hoping they land in a passable order.
But he is presiding over a decline at Villa Park which is breathtaking. And if Villa go down, it would not just be a crying shame for a proud club... it would be a scandal.
Let's put some cards on the table here. Villa are one of my favourite clubs. They have a fabulous ground dripping in tradition, and only a club with a touch of class would run the late Brian Moore's commentary of Peter Withe's winner in the 1982 European Cup final across a banner behind one goal.
For a while, it looked as if O'Neill was going to bring the glory days back to Spaghetti Junction, but his departure, five days before the season kicked off, was ill-timed. By the time Houllier had been identified as his successor, and released from the French Football Federation's handcuffs, the transfer window had long since been sealed and double-glazed.
So as senior players have fallen by the wayside with injuries, leaving youngsters with bags of promise but little streetwise knowledge of the Premier League to hold the fort, Villa have slipped down the greasy pole.
If the decline is not arrested soon, there is only one man who will pay the price by losing his job. But can Villa's nucleus of first-team regulars really look themselves in the mirror and say, with conviction, that they are too good to go down?
West Ham thought they were immune to the drop in 2003 when they had David James, Joe Cole and Jermain Defoe in the team. They were wrong. Leeds United had delusions of grandeur about conquering Europe when Peter Ridsdale was buying expensive goldfish and signing players on exorbitant wages. They were nearly bankrupted by the folly. And Newcastle United's recent experience should serve as a public health warning to all clubs blinded by the 'too good to go down' mantra.
Unless Villa pull out of their nosedive soon, they are in grave danger of dipping out of the top flight for the first time in 24 years. Don't kid yourself that it can't happen. From unthinkable to improbable, it's beginning to look quite likely.




 
Yanga yasaka bil. 4.5


Na Elizabeth Mayemba

KLABU ya soka ya Yanga inatafuta sh.bilioni 4.5 kwa ajili ya ujenzi wa Uwanja wa Kaunda na jengo la Mtaa wa Mafia, Kariakoo Dar es Salaam.Akizungumza Dar es Salaam jana, Msemaji wa klabu hiyo, Louis Sendeu, alisema
wamepanga kujenga uwanja mkubwa wa kisasa na jengo lao la Mafia ambalo litakuwa la ghorofa 10.

"Mambo yanakwenda vizuri, na Kamati ya miradi iliyochaguliwa chini ya Mwenyekiti wake Mbaraka Igangula, inafanya vizuri kazi hilo, hivyo kila kitu kitakwenda sawa," alisema.

Alisema Kampuni ya Ujenzi ya NEDCO, ndiyo iliyopata tenda ya kusimamia ujenzi wa uwanja na jengo, ambapo wameanza kwa kuchora ramani ya uwanja.

Sendeu alisema klabu hiyo imebuni mbinu ya kukusanya fedha kwa ajili ya ujenzi huo, ambapo watakuwa wakiandaa chakula cha jioni na kualika watu mbalimbali kwa lengo la kuomba michango.

Msemaji huyo alisema mchezaji wao Shamte Ally, anaendelea vizuri baada ya kufanyiwa matibabu wiki mbili zilizopita, na ameanza kufanya mazoezi mepesi ya kutembea mwenyewe.

Alisema mwanzo alikuwa akitembelea magongo, lakini sasa anaweza kutembea mwenyewe na Januari 8, mwakani atamtoa bandeji ngumu (POP).
Wakati huo huo, uongozi huo umesema kwamba, mazungumzo kati yao na klabu ya Tang Long ya Vietnam inayomhitaji kiungo wao Abdi Kassim 'Babi', yanaendelea vizuri.

Sendeu alisema klabu hiyo imeomba imnunue mchezaji huyo kwa dola 35,000 za Marekani, lakini uongozi wa Yanga umetaka walipwe dola 40,000.
"Hata hivyo, tutafikia muafaka na kumruhusu akacheze huko, na tutampa baraka zote kama viongozi," alisema.
 
...Kuitangaza nafasi ya Mpangala


Na Elizabeth Mayemba

UONGOZI wa klabu ya Yanga unatarajia kuitangaza nafasi ya Meneja wa timu hiyo mwakani.Kwa sasa nafasi hiyo inashikiliwa na Emmanuel Mpangala, ambaye katika uongozi uliopita alikuwa Katibu wa Kamati ya Mashindano.Habari za
kuaminika zilizopatikana ndani ya klabu hiyo Dar es Salaam jana, zilidai kuwa, uongozi huo tangu wiki iliyopita ulikuwa ukiitafakari nafasi hiyo.

"Meneja wa sasa mwisho wake ni Desemba mwaka huu, hivyo kuanzia mwakani atatafutwa mwingine, kwa upande wetu hatuoni kama Meneja wa sasa ni mbaya, lakini kwa kuwa uongozi umeamua hatuna budi kukubaliana nao," kilieleza chanzo cha habari.

Chanzo hicho kilieleza kuwa, sifa mojawapo inayotakiwa kwa Meneja huyo, anatakiwa awe mwanachama halali wa Yanga, aliyewahi kuichezea timu hiyo, elimu na awe karibu na wachezaji.kilieleza kuwa, meneja wa sasa, Mpangala hatakatazwa kuomba nafasi hiyo kama anajiona anavigezo vinavyotakiwa, kwani ni haki ya kila mwanachama kuomba nafasi hiyo.

Hata hivyo, kuna baadhi ya viongozi ambao wameliafiki suala hilo, lakini mmoja wa viongozi wa juu wa klabu hiyo, hakubaliani na maamuzi hayo ambaye alisema haoni sababu ya kuitangaza nafasi hiyo.
 
Yanga kutumia 4.5 bilioni kwa ukarabati
Thursday, 30 December 2010 20:57

Clara Alphonce
KLABU ya Yanga inatarajia kutumia shilingi 4.5 Bilioni kwa ajili kukarabati Uwanja wao wa Kaunda na kukarabati jengo lao la mtaa wa Mafia Jijini Dar es Salaam ili liwe la kisasa zaidi, ukarabati ambao utachukua miaka miwili.

Afisa Habari wa Yanga, Louis Sendeu alisema kwa sasa wameshaingia mkataba na Kampuni ya Nedco ambayo imeshaanza uchoraji ramani wa Jengo hilo ambalo litakuwa na gorofa 10 pamoja na ukaguzi wa uwanja kabla hawajaanza kazi rasmi.

Alisema kuwa makubaliano hayo ya kuanza kwa ujenzi huo yamefikiwa baada ya Kamati ya kuendeleza Miradi ya Yanga kukutana ikiwa chini ya Mwenyekiti wake Baraka Igangula na ikiwa na wajumbe nane.

Alisema uwanja huo wanataka kuutengeneza na kuwa wa kisasa zaidi ambao utachukua mashabiki elfu 25.

Alisema kwa sasa klabu yao haina fedha, ila kampuni ya uchoraji itakapokamilisha uchoraji wa ramani, klabu ya Yanga itakuwa ikifanya tafrija mbali mbali kama kuandaa chakula na kuwaarika waheshimiwa na makampuni mbali mbali kwa ajili ya kuchangia na kufanya matamasha ambayo yataiingizia Yanga fedha za kukamilisha ujenzi huo.

Wakati Sendeu akisema hivyo mwanzoni mwa mwaka jana uongozi wa Yanga chini ya mwenyekiti wake Iman Madega kwa kushirikiana na mfadhili wao mkuu Yusuf Manji waliahidi kujenga uwanja huo na kufanya ukarabati mkubwa wa makao makuu ya klabu hiyo.

Katika hatua ya awali, akishirikiana na uongozi wa Yanga, Manji alianza ukarabati wa jengo ikiwamo kupakwa rangi ili liendane na hadhi yake na baada ya hapo, aligeukia ukarabati wa Uwanja wa Kaunda na jengo, ili kuifanya klabu kuwa ya kisasa kwa gharama ya zaidi ya Shs 900m.

Kwa mujibu wa Madega, uwanja huo ulitakiwa kuwa na uwezo wa kuchukua mashabiki 15, 000 waliokaa, ili baadhi ya mechi za Ligi Kuu kuanzia mzunguko wa pili wa msimu huu zichezewe uwanja wa Kaunda.

Lakini hadi sasa ukarabati wa jengo na uwanja bado haujakamilika hali iliyosababisha Manji kutishia kujitoa kuifadhili klabu hiyo mwishoni mwa mwezi Novemba huku akiwalalamikia watendaji wa Yanga kwamba wamekuwa wazito katika kuchangamkia vitu vya maendeleo akitolea mfano duka la klabu hiyo ambalo mpaka leo halijapangishwa pamoja na watu ambao walipewa jukumu la kuhakikisha watu waliovamia kiwanja cha Yanga, Mtaa wa Twiga na Jangwani wanaondolewa ili ujenzi wa uwanja uanze mara moja, lakini watu hao wamekuwa wazito kitu ambacho kinamkatisha tamaa.

Pia Sendeu aliongelea kuhusu suala la mchezaji wao Abdi Kassim ambaye anatakiwa na klabu ya Dong Long Ham ya Vietnam.

Sendeu alisema wamekuwa wakiendelea na mazungumzo na timu ya Dong Long Ham ya Vietnam mpaka sasa, ambapo klabu ya Dong Long Ham inataka kutoa dola 35,000 lakini Yanga inataka Dola 40,000 hivyo bado wanaendelea na mazungumzo na endapo watakubaliana basi watamuuza mchezaji huyo.

Kwa upande wa ushiriki wao katika michuano ya Mapinduzi, Sendeu alisema Yanga itaondoka Dar es Salaam siku ya Jumapili ikiwa na wachezaji 22 na viongozi watano.

Alisema wachezaji watakaobaki ni wale watano waliopo kwenye timu ya Taifa na wengine wawili ambao ni majeruhi Athuman Idd 'Chuji' anayesumbuliwa na kuchanika kwa misuli na Shamte Ally ambaye amefanyiwa upasuaji wa goti hivi karibuni.

Afisa Habari wa Yanga alisema kabla timu hiyo haijaondoka kesho itacheza mechi ya kirafiki na JKT Ruvu kwa ajili ya kujiandaa na mashindano hayo ya kombe la Mapinduzi. .

Sendeu alitaja viingilio katika mchezo huo kuwa VIP sh7,000, Jukwaa kuu sh 5,000, Kijani sh 3,000 na Mzunguko ni sh 2,000.

Katika Hatua nyingine Sendeu alizungumzia usajili wa mchezaji wao Green Atupele kutoka kikosi cha pili ambaye amepandishwa kikosi cha kwanza kuwa hakusajiliwa kwa sh 15 milioni, ila Atupele na mwenzake John Simbeya walisajiliwa kwa 3.5 milioni.
 
Waziri Nahodha aikuna BASATA


Na Addolph Bruno

BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA) limeguswa na kauli ya Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mheshiwa Shamsi Vuai Nahodha ya kuzitaka idara za Serikali kutumia sanaa katika kutoa elimu kwa Umma.Akizungumza Ofisini kwake jana
Katibu Mtendaji wa BASATA, Ghonche Materego alisema, kauli hiyo inaonyesha wazi kwamba Waziri Nahodha anatambua umuhimu wa sanaa katika kufikisha ujumbe kwa jamii na kwamba BASATA inamuunga mkono na kumpongeza sana kwa kuwa na mtazamo huo chanya kuhusu sanaa.

Waziri Nahodha hivi karibuni, alitoa agizo kwa idara za serikali kutumia sanaa kama njia ya kuelimisha jamii juu ya masuala mbalimbali yanayowahusu wananchi ili ujumbe uweze kuwafiki wananchi wengi hasa kwa kuwa wananchi wanapenda sana kuangalia vipindi vya sanaa kuliko vipindi vingine.

Kwa kauli hiyo ya Nahodha Ghonche amesema inayofaa kuungwa mkono si kwa sababu amezungumzia masuala ya sanaa bali ni kwa sababu ameona umuhimu wa kutumia mbinu inayokubalika na kuaminiwa katika katika kufikisha ujumbe.

"Sanaa ni chombo chenye nguvu katika kufikisha ujumbe na inafahamika hivyo, sisi kama wadau wa masuala ya sanaa tunamshukuru Waziri Nahodha kwa kuliona hilo na kutoa wito kwa idara za Wizara yake kutumia sanaa katika kuwaelimisha wananchi juu ya masuala mbalimbali, kwa kweli tumefarijika sana kuona mtu ambaye si mwana sanaa anatambua hilo na kulisema hadharani," alisema Ghonche.

Amesema pamoja na kauli hiyo ya Waziri Nahodha ni vyema idara na asasi zingine zinazotaka kutumia sanaa katika kuelimisha jamii zikawatumia wasanii waliosajiliwa na BASATA na wenye vibali badala ya kutumia tu wasanii wasiotambuliwa.

"Katika kutekeleza hili ni vyema wakatumika wasanii ambao wamesajiliwa na wanatumbuliwa na BASATA ili kuepusha ubabaishaji," alisema Ghonche.





 
Wachezaji wote Misri-TFF
Thursday, 30 December 2010 20:47

Waandishi wetu

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limezitolea nje klabu za Simba na Yanga zilizoomba wachezaji wao waenguliwe kwenye kikosi cha timu ya Tanzania 'Taifa Stars' kinachojiandaa na mashindano ya Bonde la Mto Nile ili waungane na wachezaji wenzao kwenye klabu kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya klabu bingwa Afrika na Shirikisho mwezi ujao.

Makamu Mwenyekiti wa Simba, Godfrey Nyange ' Kaburu' alisema kuwa baada ya kuwaandikia barua TFF, kuwaomba wachezaji wao kwa ajili ya kuendelea na programu ya kocha Patrick Phiri kwa michuano ya kimataifa, TFF juzi iliwajibu barua hiyo kuwa haitawaruhusu wachezaji hao kurudi katika klabu zao.

Hata hivyo Kaburu alisema kuwa kitendo hicho kitaathiri sana programu ya kocha Phiri kwa sababu wachezaji hao watarudi wiki moja kabla ya safari yao ya kwenda Comoro Januari 28 kwa ajili ya mchezo wao wa awali ambapo kwa mujibu wa Ratiba ya CAF mchezo huo unaweza kuchezwa Januari 28,29 au 30.

Kitendo cha Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kukataa kuwaachia wachezaji wa klabu za Simba na Yanga ambao wapo katika timu ya Taifa (Taifa Stars) kimeungwa mkono na wadau mbalimbali wa mchezo huo nchini na kusema TFF imeangalia utaifa zaidi.

Wakizungumza na Mwananchi jana kwa nyakati tofauti wadau hao walisema kuwa uamuzi wa TFF ni wa busara kwa sababu mashindano hayo ni muhimu, pia yatawapa nafasi wachezaji hao kujitangaza kimataifa ikiwa ni pamoja na kujiweka fiti kabla ya kuziwakilisha klabu zao kwenye michuano ya Klabu bingwa Afrika na ile ya Shirikisho.

"Kwanza tunatakiwa tufanye vizuri katika mashindano hayo kwa sababu ndiyo kwanza yameanzishwa, pili yatasaidia kuwapa mazoezi ya uhakika wachezaji wa Yanga na Simba,
"Hakuna sababu ya kuanza kurumbana kwani TFF wameangalia zaidi utaifa na baada ya hapo mambo mengine yanafuata," alisema Shaaban Geva mchezaji wa zamani wa timu ya Simba.

"Jambo kubwa lililoangaliwa hapa ni umuhimu wa mashindano hayo licha ya watu kuyaona kama hayana umuhimu, lakini kwa hakika yana umuhimu wake mkubwa ambapo pia ni faida kwa timu za Simba na Yanga," alisema Kabange.

Naye Daktari wa timu ya Taifa Stars, Festo Mwamkemwo amesema wachezaji wote wa Stars wamepewa dose ya ugonjwa wa Malaria kwa ajili ya kujikinga na ugonjwa huo.

Akizungumza na wachezaji hao Dk huyo alisema amelazimika kuwapatia wachezaji hao dawa hiyo kutoka na idadi kubwa ya mbu waliopo nchini Misri.

"Mgonjwa anatakiwa kumeza vidonge vinane kwa mara moja, lakini nyinyi mnatakiwa kumeza vidonge vinne na baada ya saa mbili mnameza viwili,"alisema Dk Mwamkemwa.

Aliwataka wachezaji hao kuzingatia masharti ya dawa hizo kwa sababu zitawasaidia wakiwa nchini Misri na kwamba watakaopuuzia watasumbuliwa na malaria na mwisho watarudishwa nyumbani.

"Tukifika Misri halafu mtu aumwe malaria atalazimika kurudi nyumbani na hivyo kuigharimu timu kwa sababu kila mchezaji katika timu ana umuhimu wake na ndiyo maana ameitwa,"aliongeza dk Mwamkemwo.

Habari hii imeandaliwa na Clara Alphonce,Sweebert Lukonge, Jackson Odoyo,
 
Jay Dee azindua Maji
Thursday, 30 December 2010 20:46

Vicky Kimaro
MWANAMUZIKI Judith Wambura 'Lady Jay Dee' amezindua rasmi maji yenye nembo ya jina lake huku akisema atazindua pia mgahawa wake wa chakula hivi karibuni.

Akizungumza na waandishi wa Habari kwenye ukumbi wa Serengeti Paradise Hotel jijini jana, Jay Dee alisema Maji hayo ambayo yanajulikana kama Lady Jay Dee Pure Drinking Water yanatengenezwa na kampuni ya Mohamed Interprises 'Melt' kwa makubaliano maalum.

"Maji haya yana ujazo wa ml 600 na yatauzwa kwa bei ya kawaida sana kama yalivyo maji mengine na tutaendelea kutoa ujazo tofauti kulingana na mahitaji wa wateja wetu,"alisema Jay Dee au Jide.

"Pia kama mnavyojua nisingekuwa mwanamuziki ningekuwa mpishi, nina mpango wa kufungua mgahawa wangu mkubwa sana mwezi huu wa Januari, utakuwa na vyakula tofauti tofauti hasa vya kiafrika nitavipa majina ya nyimbo zangu na ya watu maarufu,"alisema Jay Dee

Alisema pia kuanzia mwezi Januari atafuta shoo zake zote na kubakiza shoo moja ya kila ijumaa ambayo itafanyika Mzalendo Pub ili aweze kufanya shuguli za kijamii.

"Nimekuwa nikifanya shoo nyingi sana bila kupumzika mwezi mzima, mwaka 2011 nataka uwe mwaka wa mabadiliko kwangu, nikiwa kama balozi wa Fistula nataka kufanya kazi za kuisaidia jamii yangu....."Nimeingia mkataba pia na kampuni ya Rock Star ambayo ina mkataba na wasanii mbali mbali wa hapa nchini kama Ally Kiba ambaye walimpeleka akaenda kurekodi na mwanamziki mkubwa duniani R Kelly, hivyo nitakuwa nafanya kazi nyingi za kampuni hiyo ndio maana nimepunguza shoo za ndani,"alisema.

"Machozi bendi itakuwepo kama kawaida na itafanya shuguli zake chini ya Machozi Company Limited ambayo pia itasimamia shuguli zangu zote chini ya mkurugenzi wangu Gadna Habash,"alisema Jay Dee .

Wakati huo huo Jay Dee alisema yupo mbioni kukamilisha albamu yake ya tano nje ya bendi 'Solo Artist'.

 
Mash:Tunasaka heshima, vipaji baadaye
Thursday, 30 December 2010 20:45

Jackson Odoyo
KOCHA Msaidizi wa timu ya Taifa ya Tanzania,Taifa Stars, Sylvester Mash amesema, timu kufanya vizuri ama kufanya vibaya ni matokeo ya kuvuna walichokipanda.

"Tunavuna tulichokipanda katika soka letu hakuna haja ya kulaumiana wala kutupiana mpira pale timu inapofanya vibaya"alisema Mash.

Mash ambaye ameachiwa jukumu la kuiandaa timu hiyo kwa ajili ya mashindano maalum ya bonde la mto Nile yatakayofanyika nchini Misri kuanzia Januari 5 hadi 17, alisema baada ya madai ya baadhi ya wadau wa soka kupinga uteuzi wake wa wachezaji wakongwe katika timu hiyo.

Akitetea uamuzi wake wa kuwaita wakongwe katika timu hiyo huku akiwaacha vijana, Mash alisema lengo lao nikujenga heshima na sio kuinua vipaji.

"Mwanzo nilisema tunavuna tulichokimanda kwa sababu hatuna malengo ya kuandaa wachezaji kwa ajili ya baadaye na ndiyo maana bado tunarudi kuwakumbatia wachezaji wenye umri mkubwa," alifafanua Mash na kuongeza.

"Kuna vijana wengi wenye umri mdogo, lakini hatuna utaratibu wa kuwaanda kwa ajili ya faida ya baadaye, nilipotoka Brazil nilisema wale vijana waandaliwe ili muda wao ukifika waisaidie taifa na huu ndiyo ulikuwa muda wao je wako wapi hivi sasa?" alihoji kocha huyo.

Alifafanua kuwa Tanzania wamezoea kuandaa timu katika mazingira magumu na ya muda mfupi ndiyo maana wameitwa wakongwe na baadaye wakiachana na soka wataanza tena maandalizi kama hayohayo ya kuokotana kila inapofika mashindano.

Alisema, lengo la kujenga heshima nikuwafanya Watanzania waiunge mkono timu yao kupitia wachezaji hao hao waliopo hivi sasa na ndiyo maana wakati wa mashindano ya Chalengi walifanikiwa kwa sababu lengo lao ilikuwa ni kujenga heshima.
 
Mash:Tunasaka heshima, vipaji baadaye
Thursday, 30 December 2010 20:45

Jackson Odoyo
KOCHA Msaidizi wa timu ya Taifa ya Tanzania,Taifa Stars, Sylvester Mash amesema, timu kufanya vizuri ama kufanya vibaya ni matokeo ya kuvuna walichokipanda.

“Tunavuna tulichokipanda katika soka letu hakuna haja ya kulaumiana wala kutupiana mpira pale timu inapofanya vibaya”alisema Mash.

Mash ambaye ameachiwa jukumu la kuiandaa timu hiyo kwa ajili ya mashindano maalum ya bonde la mto Nile yatakayofanyika nchini Misri kuanzia Januari 5 hadi 17, alisema baada ya madai ya baadhi ya wadau wa soka kupinga uteuzi wake wa wachezaji wakongwe katika timu hiyo.

Akitetea uamuzi wake wa kuwaita wakongwe katika timu hiyo huku akiwaacha vijana, Mash alisema lengo lao nikujenga heshima na sio kuinua vipaji.

“Mwanzo nilisema tunavuna tulichokimanda kwa sababu hatuna malengo ya kuandaa wachezaji kwa ajili ya baadaye na ndiyo maana bado tunarudi kuwakumbatia wachezaji wenye umri mkubwa,” alifafanua Mash na kuongeza.

“Kuna vijana wengi wenye umri mdogo, lakini hatuna utaratibu wa kuwaanda kwa ajili ya faida ya baadaye, nilipotoka Brazil nilisema wale vijana waandaliwe ili muda wao ukifika waisaidie taifa na huu ndiyo ulikuwa muda wao je wako wapi hivi sasa?” alihoji kocha huyo.

Alifafanua kuwa Tanzania wamezoea kuandaa timu katika mazingira magumu na ya muda mfupi ndiyo maana wameitwa wakongwe na baadaye wakiachana na soka wataanza tena maandalizi kama hayohayo ya kuokotana kila inapofika mashindano.

Alisema, lengo la kujenga heshima nikuwafanya Watanzania waiunge mkono timu yao kupitia wachezaji hao hao waliopo hivi sasa na ndiyo maana wakati wa mashindano ya Chalengi walifanikiwa kwa sababu lengo lao ilikuwa ni kujenga heshima.
 

Uwanja wa kisasa Yanga kugharimu Bil 4/
-
Imeandikwa na Betram Lengama; Tarehe: 30th December 2010 @ 23:59

KLABU ya soka ya Yanga imetenga bajeti ya Sh bilioni nne na nusu kwa ajili ya kutekeleza miradi ya ujenzi wa uwanja wa kisasa wa soka pamoja na jengo la kitegauchumi, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mikakati ya klabu hiyo kujiondoa kwenye utegemezi.

Ofisa habari wa Yanga, Louis Sendeu alibainisha hayo jana Dar es Salaam wakati akizungumzia masuala mbalimbali ya klabu hiyo ambapo alibainisha kuwa klabu hiyo itaujenga upya uwanja wake wa Kaunda uliopo makao makuu ya klabu hiyo mtaa wa Twiga na Jangwani na kuwa wa kisasa.

Kwa mujibu wa Sendeu uwanja huo ambao utakuwa na uwezo wa kuchukua watu zaidi ya 25,000 utajengwa na kampuni ya ukandarasi ya Nedco ambayo ndio imepewa zabuni ya kujenga uwanja huo na kamati ya kuendeleza miradi ya klabu hiyo ambayo inaongozwa na Baraka Igangula.

"Ujenzi huo wa uwanja wa kisasa wa klabu yetu utasimamiwa na kampuni ya Nedco ambayo ndio imepewa kazi ya kusimamia miradi hiyo miwili ya ujenzi wa uwanja pamoja na kitega uchumi cha klabu yetu katika mtaa wa Mafia-Kariakoo hapa jijini," Sendeu alibainisha.

Aidha Sendeu amebainisha kuwa kitega uchumi ambacho kitajengwa katika mtaa huo wa Mafia ni jengo lenye ghorofa zisizozidi 10 na kwamba ujenzi wa miradi hiyo miwili unatarajiwa kukamilika si chini ya kipindi cha miaka miwili ambapo fedha za ujenzi huo Sh bilioni 4.5 zinatarajiwa kupatikana kupitia hafla mbalimbali za kuchangia miradi hiyo kama ile ya kuandaa chakula cha usiku ambao watu maarufu pamoja na wanachama wa klabu hiyo watakaribishwa kuchangia.

Mbali na kufanyika kwa hafla hizo, pia watapeleka maombi mbalimbali kwa kampuni za ndani na nje ya nchi kudhamini miradi hiyo miwili ili kuwezesha klabu hiyo kutimiza malengo yake hayo.

Hata hivyo suala la ujenzi wa uwanja wa kisasa wa klabu hiyo lina ukakasi kiasi kwani awali ilikuwa inafahamika kuwa ujenzi wa uwanja huo unafadhiliwa na mdhamini mkuu wa klabu hiyo Yusuf Manji, ingawa uongozi wa Yanga ulipoulizwa juu ya suala hilo ulikana Manji kuhusika na kugharamia ujenzi huo.

Katika hatua nyingine, Yanga jana ilithibitisha rasmi kushiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Januari 2 mjini Zanzibar na kufikia kilele Januari 12 ambapo ndio sherehe za kuadhimisha miaka 36 ya Mapinduzi.

Sendeu alisema kiungo Athumani Iddi hatokuwepo kwenye kikosi kitakachokwenda Zanzibar keshokutwa kutokana na kuumia nyama ya paja.

"Athumani Iddi amekuwa haonekani katika mazoezi na mechi za siku za hivi karibuni kutokana na kuwa majeruhi, anasumbuliwa na matatizo ya misuli ya paja kuchanika na ndio maana hatosafiri na timu kwenda Zanzibar kwenye michuano hiyo ya Mapinduzi," alisema Sendeu.

Mbali na Iddi, mchezaji mwingine ambaye atakosa michuano hiyo ni Shamte Ally ambaye bado anaendelea na matibabu ya mguu ambao umefungwa plasta ngumu (P.O.P) ambayo itaondolewa Januari 8 mwakani na kwa sasa mchezaji huyo ameanza mazoezi ya kutembea.



Jumla Maoni (1) Maoni Na wasiwasi sana na hizo figure watakazotumia.Being an Engineer na wasiwasi kama wamefanya analysis vizuri ya ujengi.Jengo gani la ghorofa kumi linalogarim bil 4.5 kwa gharama za ujenzi za siku hizi ? labda ghorofa la makuti.hata gharama za uwanja wa watu hao 25,000 ni kitu kama billioni 20 hivi unless ujengwe tu ili uwe kama mao-tse -tung kule znz
 
Uchaguzi mkuu ZFA hapatoshi

Imeandikwa na Issa Yussuf, Zanzibar; Tarehe: 30th December 2010 @ 23:50


MBIVU na mbichi juu ya uongozi wa Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) zitajulikana leo kwenye uwanja wa Gombani, Chakechake, Pemba pale wajumbe wa kamati ya Utendaji watakapokutana kuchagua viongozi wapya wa chama hicho.

Kamati hiyo inatarajiwa kuchagua Mwenyekiti mpya na Makamu Mwenyekiti wa ZFA huku wanaomaliza muda wao Ali Fereji Tamim na Hajji Ameir wakikabiliwa na ushindani mkubwa katika nafasi wanazotetea.

"Tuko tayari kwa uchaguzi kesho (leo) na wajumbe wote wametakiwa kuzingatia muda, tunataka kumaliza kila kitu mpaka ikifika kesho mchana," alisema Katibu Mkuu wa ZFA Mzee Zam Ali.

Alisema Waziri anayehusika na michezo Abdilahi Jihadi Hassan atakuwa mgeni rasmi ambapo atazungumza na wajumbe kabla ZFA haijatoa taraifa za uongozi unaomaliza muda wake kwa kipindi cha minne iliyopita.

"Baada ya taarifa ya uongozi uliopita, tutafanya uchaguzi wa kuchagua viongozi wapya," alisema Ali.

Wanaowania nafasi ya Mwenyekiti ni Munir Zakaria ambaye ni mtangazaji wa kituo cha runinga cha Channel 10, Zanzibar, Suleiman Mahmoud Jabir na Hafidh Kassim mtangazaji wa Radio Zenji FM.

Wanaowania nafasi ya Makamu mwenyekiti ni Amani Makungu ambaye ni mmiliki wa timu ya soka ya Zanzibar Ocean View na Ali Khatib Dai.

Wengine wanaowania nafasi hiyo kutoka Pemba ni Suleiman Amour na Ali Mohamed.
 
Papic atoa baraka kwa Babi
Thursday, 30 December 2010 20:43

Doris Maliyaga
KOCHA wa Yanga, Kostadin Papic ametoa baraka zote kwa kiungo wake Abdi Kassim ‘Babi' anayekwenda kucheza soka ya kulipwa Vietnam katika klabu ya Long Tang na kuwahahasa wengine kuongeza bidii.

Kiungo huyo wa kimataifa wa Tanzania, alifuzu majaribio yake aliyoyafanya kabla ya michuano ya Chalenji na sasa anatarajiwa kuungana na Danny Mrwanda.

Akizungumza na Mwananchi Papic alisema, kuondoka kwa mchezaji huyo kwake ni faraja na anasikia furaha kwa sababu amekamilisha ndoto zake zinazotegemewa na kila mchezaji.

"Kwangu ni faraja na mafanikio kwa sababu anakamilisha ndoto na isiishie kwa huyo tu na wengine wajitahidi ili wafikie viwango vya juu watoke kama mwenzao,''alisema Papic.

Kwa upande wa Babi amesema kila kitu kinakwenda sawa ambapo timu ya taifa tayari nayo imetoa baraka zake ikimruhusu kwenda na ataondoka muda wowote kuanzia sasa.

"Kila kitu kinakwenda sawa nitaondoka muda wowote kuanzia sasa kwa sababu walimu wote wameniruhusu hakuna tatizo na naahidi naenda kuwafanyia kazi ya mafanikio,''alisema Babi aliyewahi kuichezea Mtibwa Sugar ya Morogoro.

Kwa mujibu wa katibu wa Yanga, Laurence Mwalusako alidhibitisha kuwa uongozi wake ulifanya mazungumzo na Long Tang na kumwachia kiungo huyo kwa gharama za milioni 40 wakati Long Tang wamerizika kutoa milioni 35 baada ya 100m ambazo walizitaja awali.
 

Michuano Vijana: Azam1- AFC 1


Imeandikwa na Evance Ng'ingo; Tarehe: 30th December 2010 @ 23:40

Mchezaji wa Azam FC, Fred Songoro (kushoto) akiudhibiti mpira huku Kilala Hussein wa AFC Arusha akijiandaa kumkabili wakati wa mashindano ya vijana chini ya miaka 20 ya Kombe la Uhai yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam jana. Timu hizo zilitoka sare ya 1-1. (Picha na Fadhili Akida).


TIMU ya vijana ya Azam FC jana ilijikuta ikitunishiana msuli na timu ya AFC Arusha kwa kutoka sare ya bao 1-1 katika mchezo wa ligi ya vijana inayoendelea kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.

Azam ilianza kuliona lango la AFC dakika ya 24 kupitia mchezaji wake Joseph Mahundi ambaye alipiga shuti lililogongana na beki wa AFC na kufunga bao la kwanza.

Kuingia kwa bao hilo kuliifanya AFC izinduke na kupata bao la kusawazisha katika dakika ya 71 kwa mkaju wa penati iliyopigwa na Emanuel Mollel iliyomwacha kipa wa Azam Daud Mwasongwa akiwa chini, penati hiyo ilitokana na mchezaji wa Azam kushika mpira katika eneo la hatari.

Katika mchezo wa jana asubuhi Polisi Dodoma ilicheza dhidi ya Ruvu Shooting ambapo Polisi ilishinda bao 1-0 lililofungwa na Keneth Masumbuko aliyepiga shuti kali.

Polisi ndio ilionekana kuutawala mchezo huo na kufanya mashambulizi ya mara kwa mara lakini hata hivyo iliishia na ushindi wa bao hilo moja.

Ligi hiyo inaendelea tena leo asubuhi kwa kuzikutanisha timu za vijana za Yanga na Simba.
 
Malaysia yatwaa ubingwa wa Asia
Thursday, 30 December 2010 20:40

KUALA LUMPUR, Malaysia

SERIKALI ya malaysia imetangaza kuwa leo itakuwa ni siku ya kupumzika na kusheherekea ushindi ilioupata baada ya kuichapa Indonesia 4-2 na kutwaa ubingwa wa kombe la ASIAN Suzuki.

Malaysia na Indonesia nchi ambazo ni jirani zilicheza mechi ya kwanza mjini Kuala Lumpur, ambapo Malaysia ilishinda bao 3-0, lakini katika mechi ya marudiano iliyofanyika Jakarta, Indonesia ilishinda bao 2-1, hivyo Malaysia kushinda 4-2.

Waziri Mkuu wa Malaysia, Najib Razak alitangaza kwenye televisheni ya Taifa kwamba ushindi iliopata Malaysia ni jambo zuri kwa soka la Malaysia.

"Nawapongeza vijana wa Malaysia, mlicheza vizuri kama timu na mmeipeperusha vizuri bendera ya Malaysia, nawapongeza sana," alisema waziri Mkuu wa Malaysia.

Malaysia na Indonesia ni nchi ambazo mashabiki wake huwa wanatupiana maneno ya kejeli na timu hizo zikikutana mechi kuwa na upinzani mkali, pia nchi hizo mbili zina ushindani wa mambo mengi ukiacha mchezo wa soka.

Mashabiki wa Indonesia wanadai kuwa katika mechi ya kwanza waliyofungwa mabao 3-0 mjini Kuala Lumpur kipa wao alikuwa akipigwa na mwanga wa kijani machoni ambao ulikuwa ukitoka kwenye kalamu walizokuwa nazo mashabiki wa Malaysia.

Mashabiki wa Indonesia wanadai ilifika wakati mwamuzi wa pambano alikuwa akiwaomba mashabiki wa Malaysia kuacha kuonyesha mwanga huo kwa kipa wa Indonesia uliokuwa ukimsababishia kushindwa kuona vizuri na kuruhusu mabao matatu.

Huku wakiogopa huenda vurugu zingeweza kujitokeza, katika mechi iliyofanyika Jakarta,Indonesia kulikuwa na ulinzi mkali waliokuwa wamebeba silaha kubwa.

Nchi ya Indonesia ina watu karibu 240 milioni wakati Malaysia ina watu 28 milioni.

Katika mechi iliyofanyika mjini Jakarta kwenye uwanja wa Gelora Bung Karno, raisi wa Indonesia, Susilo Bambang Yudhoyono alihudhuria mechi hiyo.

Walikuwa Malaysia waliopata bao la kwanza wakiwa ugenini ambalo lilifungwa na mfungaji bora wa mashindano hayo ya kombe la Asia, Mohammad Safee Bin Mohammad Sali, kabla ya Mohamed Nasuha kuisawazishia Indonesia na Mohammad Ridwan kuingezea Indonesia bao la ushindi.

 

Kigoma yaanza maandalizi michuano ya Wanawake

Imeandikwa na Fadhili Abdallah, Kigoma; Tarehe: 30th December 2010 @ 23:30


TIMU ya soka ya wanawake ya Manispaa ya Kigoma Ujiji inatarajia kuanza mazoezi Januri 10 tayari kwa mashindano ya mkoa yatakayoanza mapema Februari.

Kocha wa timu hiyo Maduwa Almasi alisema kuwa mazoezi kamili ya timu hiyo yataanzia siku hiyo katika Uwanja wa michezo wa Lake Tanganyika mjini hapa.

Maduwa alisema kuwa mazoezi hayo yataanza rasmi kwa ajili ya kujiwinda na mashindano ya mkoa yatakayoshirikisha timu kutoka wilaya zote za mkoa huo.

Alisema kuwa mashindano hayo yanatarajia kuanza Februari 12 mwakani katika Uwanja wa michezo wa Lake Tanganyika ambayo ndiyo yatakayoteua timu ya Mkoa itakayoshiriki mashindano ya taifa ya Kombe la Taifa.

Maduwa alitoa wito kwa wachezaji wa timu hiyo kujitokeza siku hiyo kwa ajili ya kuanza mazoezi tayari kushiriki mashindano hayo.

Alisema kuwa sambamba na wachezaji wa timu hiyo ambao wameshashiriki mashindano mbalimbali na timu hiyo pia ametoa wito kwa wasichana wengi zaidi wenye shauku ya kujiunga na timu hiyo kujitokeza.
 
Chelsea yashinda, Liver yateswa
Thursday, 30 December 2010 20:42

LONDON, England
BAADA ya kushindwa kushinda mechi sita mfululizo kwenye Ligi Kuu ya England, Chelsea imeichapa Bolton bao 1-0 kwenye Uwanja wa Stamford Bridge

Katika mechi hiyo, kocha Carlo Ancelotti alimuanzisha Nicolas Anelka kwenye kikosi cha kwanza, lakini ukuta wa Bolton ulikuwa imara katika kipindi cha kwanza kuzuia washambuliaji wa Chelsea kupiga mashuti katika lango la Bolton.

Kipindi cha pili mshambuliaji wa Chelsea, Didier Drogba alitoa pasi ambayo ilimkuta Florent Malouda ambaye aliipatia Chelsea bao la ushindi katika dakika ya 61 na kuirudisha Chelsea katika nne bora juu ya Tottenham.

Baada ya kupatikana kwa bao hilo kocha Carlo Ancelotti alionekana kushangilia sana kufuatia timu yake kupata ushindi kwa mara ya mwisho Novemba 10.

"Hii ilikuwa ni hatua muhimu, sina uhakika kama mambo yataendelea kuwa mazuri, inabidi tusubiri tuone mechi ijayo, lakini ligi ipo wazi tena kwetu sisi,hatuna hali nzuri,hatujiamini na upepo siyo mzuri kwetu, tunatakiwa tufanye vizuri,"alisema Ancelotti.

Mechi nyingine ilikuwa ni kati ya Arsena dhidi ya Wigan, ambapo Arsenal imeshindwa kuitambia timu hiyo baada ya kulazimishwa sare ya 2-2 na Wigan ambayo ilikuwa ikicheza na wachezaji 10 uwanjani.

Walikuwa ni Wigan ambao walipata bao kwanza lililofungwa na Ben Watson, lakini Andrei Arshavin aliisawazishia Arsenal bao hilo na Nicklas Bendtner aliiongezea bao la pili Arsenal.

Katika dakika ya 78 mchezaji wa Wigan, Charles N'Zobia alitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kumpiga kichwa Jack Wilshere waliyekuwa wakirushiana maneno.

Katika dakika 81 beki wa Arsena Sebastien Squillaci alijifunga katika harakati za kuokoa mpira kwenye lango lao hivyo kuikosesha pointi tatu Arsenal.

Katika mechi ya Liverpool dhidi ya Wolves, nafasi ya kocha wa Liverpool Roy Hodgson imezidi kuwa kwenye nafasi mbaya baada ya Liverpool kufungwa na Wolves bao 1-0 kwenye uwanja wa Anfield.

Liverpool mpaka hivi sasa kwenye msimamo wa ligi kuu ya England inashika nafasi ya 12, ambapo katika mechi 18 ilizocheza imeshinda mechi sita tu.

Katika mechi hiyo dhidi ya Wolves, Nahodha wa Liverpool Steven Gerrard alianza katika kikosi cha kwanza tokea alipocheza mechi dhidi ya Stoke ambayo Liverpool ilifungwa bao 2-0, lakini kurudi kwake nahodha huyo hakukuleta mabadiliko yoyote.

Katika kipindi cha kwanza Liverpool ilipata nafasi za kufunga, lakini wachezaji wake Raul Meireles, Fernando Torres walishindwa kuzitumia nafasi walizopata katika kipindi cha kwanza.

Kipindi cha pili Wolves walifika mara nyingi kwenye lango la Liverpool ambapo walifanikiwa kupata bao la ushindi lililofungwa na Stephen Ward katika dakika ya 56.

Baada ya kufungwa bao 1-0 mashabiki wa Liverpool walisikia wakimlaumu kocha Roy Hodgson na wakiimba kocha wao wa zamani Rafa Benitez aridishwe Liverpool.

Mashabiki hao pia walikasirishwa na kitendo cha kocha Hodgson kumtoa David Ngog ambaye alikuwa akipeleka mashambulizi kwenye lango la Wolves na kumuingiza Ryan Babel ambaye alionekana kupooza katika mchezo huo.

Mashabiki wa Liverpool walikuwa wakiichukulia mechi hiyo dhidi ya Wolves ni mechi ya kupata ushindi na kufunga mwaka wakiwa kwenye nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi kwa sababu Wolves ipo chini kwenye msimamo wa ligi.

Katika mechi za hivi karibuni ilizocheza Liverpool imeweza kufungwa na na Blackpool, Stoke na Newcastle vipigo ambavyo vimewahuzunisha sana mashabiki wa Liverpool.

 

Mr 11 apania kuinua michezo Mbeya


Imeandikwa na Joachim Nyambo, Mbeya; Tarehe: 30th December 2010 @ 23:20

UKOSEFU wa viwanja vya michezo ya Kikapu, Wavu na Netiboli umeelezwa kumuumiza kichwa Mbunge wa Mbeya Mjini na mmoja wa waasisi wa muziki wa kizazi kipya nchini Bongofleva Joseph Mbilinyi maarufu kama Mr. II.

Akiwa katika mkutano wa kuwashukuru wananchi kwa kumchagua kushika nafasi ya kuwawakilisha bungeni, Mr II alisema anaandaa mikakati ya kuinua michezo hiyo ili itoe ajira kwa vijana jijini hapa lakini viwanja bado ni tatizo.

Alisema kwa miaka mingi vijana wapenzi wa michezo hiyo wamekuwa wakilazimika kuomba viwanja vilivyopo katika eneo la jengo la vijana Wakatoliki la Youth Centre lakini kutokana na uwepo wa kumbi za mikutano katika jengo hilo vijana hao huzuiwa kuendelea na michezo siku za mikutano.

"Tumekuwa tukitumia viwanja vilivyopo pale Youth Centre nakumbuka tangu nikiwa mdogo lakini pale kuna shughuli nyingi zinazofanywa.

Kukiwa na mikutano vijana hawaruhusiwi tena kucheza na hawawezi kubisha kwakuwa pale wanakaribishwa tu," alisema.

Hata hivyo Mbilinyi alisema tayari amekutana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji Juma Iddi ambaye amempa ruksa ya kuchagua moja kati ya maeneo ya wazi yaliyopo ajenge viwanja hivyo.

Alisema Mkurugenzi huyo amemruhusu kuchagua moja kati ya maeneo mawili ya wazi moja likiwa ni lililopo eneo la Sabasaba karibu na Shule ya Sekondari ya Meta na lingine ni lile linalojengwa bustani na maegesho ya magari karibu na Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine.

Alisema bado hajafanya tathmini ni eneo lipi litafaa kwa ujenzi wa viwanja hivyo kati ya maeneo hayo mawili lakini akasisitiza kuwa mpango huo ni lazima ukamilike ili kutowanyima fursa vijana kuibua na kukuza vipaji vyao.

Aidha, Mr II pia alisema ana mpango wa kuanzisha bonanza litakalotumika pia kuwakutanisha watu wa kada mbalimbali na kujadili mipango ya kimaendeleo tofauti na sasa ambapo wakazi hulazimika kukutana sehemu za vileo pekee hususani baa kujadiliana mambo hayo.

"Mbeya mkitaka kukutana mzungumze ni lazima mwende baa hakuna mahala pengine. Sasa kupitia bonanza letu machinga atapata fursa ya kukutana na meneja wa Vodacom na wakaweza kubadilishana mawazo," alisema.


 

Jay Dee azindua maji yake


Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 30th December 2010 @ 23:10


MALKIA wa miondoko ya muziki wa kizazi kipya Judith Wambura maarufu kama ' Lady Jay Dee' amezidi kupiga hatua katika tasnia ya muziki nchini baada ya kuingia ubia na Kampuni ya Mohamed Enterprises ya kutangaza maji ya kunywa yanayotengezwa na kampuni hiyo.

Meneja wa Masoko wa mwanamuziki huyo ambaye pia ni mumewe Gadner Habash alibainisha juu ya ubia huo alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana katika hafla ya uzinduzi wa maji hayo ambayo yatajulikana kama ‘Lady Jay Dee Pure Drinking Water'.

"Lady Jay Dee sasa ana bidhaa mpya ambayo inazalishwa na Kampuni ya Mohamed Enterprises na tukio hili ni kutumika kwa azma ya mmiliki wa Kampuni ya Mohamed Enterprises kufanya kazi na Jay Dee katika kumuendeleza zaidi," alisema Habash.

Kwa upande wake Lady Jay Dee ambaye pia ni Balozi wa ugonjwa wa Fistula alisema kutokana na majukumu kuongezeka kuanzia mwakani atapunguza maonesho ya bendi yake ya Machozi kufika onesho moja ambalo litakuwa likifanyika Ijumaa pekee kwenye ukumbi wa Mzalendo Pub jijini na Machozi Band itakuwa ikijiendesha yenyewe.

"Kwa sasa majukumu yameongezeka mno mbali na ubia huo na Mohamed Enterprises pia ninafungua mgahawa mkubwa maeneo ya kinondoni nyuma ya Best Bite na pia nimepata mikataba mipya ambayo itanifanya nipunguze baadhi ya mambo ili kupata nafasi ya kuitumikia jamii,"alisema Jay Dee.

Katika hatua nyingine Habash alibainisha kuwa Jay Dee amepata mkataba wa kuwa mmoja wa wasanii watakaokuwa kwenye mradi wa Rock Stars , kauli ambayo ilithibitishwa na mwakilishi wa Rock Star kwa ukanda wa Afrika Mashariki Christina Mosha ‘Seven' ambapo kutokana na mkataba huo ambao pia msanii Ali Kiba tayari yumo, Jay Dee atapa fursa ya kufanya maonesho katika mataifa mbalimbali ndani na nje ya nchi akishirikiana na wanamuziki nyota duniani.

Katika mradi huo wa Rock Star msanii Ali Kiba ambaye ndiye alikuwa wa kwanza hapa nchini kuingia mkataba kwenye mradi huo alipata fursa ya kurekodi wimbo na nyota wa muziki wa R & B duniani Mmarekani Robert Kelly (R. Kelly) akiwa na nyota wengine saba kutoka Afrika akina 2Face – Nigeria, Amani – Kenya, Fally Ipupa – DRC,4X4 – Ghana, JK – Zambia, Movaizhalene – Gabon na Navio kutoka Uganda.

Aidha Jay Dee amebainisha kuwa atatoa albamu yake mpya itakayokwenda kwa jina la ‘Ya Tano' akiwa pekee bila ya bendi yake akiwashirikisha wasanii nyota wa hapa nchini pamoja na sehemu nyingine za Afrika .
 

Nahodha aikuna Basata

Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 30th December 2010 @ 23:00 Imesomwa na watu: 38;

BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA) limeguswa na kauli ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Shamsi Vuai Nahodha ya kuzitaka idara za Serikali kutumia sanaa katika kutoa elimu kwa umma.

Akizungumza ofisini kwake jana Katibu Mtendaji wa BASATA, Ghonche Materego alisema, kauli hiyo inaonesha wazi kwamba Waziri Nahodha anatambua umuhimu wa sanaa katika kufikisha ujumbe kwa jamii na kwamba BASATA inamuunga mkono na kumpongeza kwa kuwa na mtazamo huo chanya kuhusu sanaa.

Waziri Nahodha hivi karibuni, alitoa agizo kwa idara za Serikali kutumia sanaa kama njia ya kuelimisha jamii juu ya masuala mbalimbali yanayowahusu wananchi ili ujumbe uweze kuwafikia wananchi wengi hasa kwa kuwa wananchi wanapenda kuangalia vipindi vya sanaa kuliko vipindi vingine.

Kwa kauli hiyo ya Nahodha Ghonche alisema ni kauli inayofaa kuungwa mkono si kwa sababu amezungumzia masuala ya sanaa bali ni kwa sababu ameona umuhimu wa kutumia mbinu inayokubalika na kuaminiwa katika kufikisha ujumbe.

"Sanaa ni chombo chenye nguvu katika kufikisha ujumbe na inafahamika, hivyo sisi kama wadau wa masuala ya sanaa tunamshukuru sana Waziri Nahodha kwa kuliona hilo na kutoa wito kwa idara za Wizara yake kutumia sanaa katika kuwaelimisha wananchi juu ya masuala mbalimbali, kwa kweli tumefarijika sana kuona mtu ambaye si mwanasanaa anatambua hilo na kulisema hadharani," alisema Ghonche.

Alisema pamoja na kauli hiyo ya Waziri Nahodha ni vyema idara na asasi nyingine zinazotaka kutumia sanaa katika kuelimisha jamii zikawatumia wasanii waliosajiliwa na BASATA na wenye vibali badala ya kutumia tu wasanii wasiotambuliwa.

"Katika kutekeleza hili ni vyema wakatumika wasanii ambao wamesajiliwa na wanatumbuliwa na BASATA ili kuepusha ubabaishaji," alisema Ghonche.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…