Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
- Thread starter
-
- #3,221
Jesus aiangamiza Yanga
Imeandikwa na Evance Ng'ingo; Tarehe: 19th January 2011 @ 10:16 Imesomwa na watu: 179; Jumla ya maoni: 0
Wachezaji wa klabu ya Yanga, Kigi Makassy (kushoto) na Abuu Zuberi (kulia) wakiwania mpira dhidi ya mchezaji wa klabu ya Atletico Paranaense ya Brazil, Jonatas Cardoso wakati wa mechi ya kirafiki ya kimataifa iliyofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jana. Yanga ililala kwa magoli 3-2. (Picha na Fadhili Akida).
TIMU ya Yanga ya Dar es Salaam jana ilishindwa kutamba kwenye Uwanja wa Taifa jijini baada ya kulala kwa mabao 3-2 dhidi ya Atletico Paranaense ya Brazil.
Katika mchezo huo Atletico ndio waliokuwa wa kwanza kuliona lango la wapinzani wao kupitia Bruno Costa dakika ya 12.
Baada ya bao hilo Yanga walikuja juu na Davies Mwape kuisawazishia timu yake dakika ya 30 akiunganisha vema krosi Salum Telela hivyo kufanya timu zote kwenda mapumziko zikiwa sare ya bao 1-1.
Hata hivyo Wabrazil hao walianza mchezo taratibu wakionekana kusoma wapinzani wao katika mechi ambayo haikuwa na mashabiki wengi.
Kipindi cha pili wageni walianza kwa kasi tena na iliwachukua dakika mbili kabla ya Jenison Jesus kuandika bao la kuongoza kwa Atletico dakika ya 47.
Lakini bao hilo liliwazindua tena Yanga na kupeleka mashambulizi ya nguvu kwa wapinzani wao wakionesha nia ya kutaka kusawazisha hivyo, kuwachanganya Wabrazil ambao dakika ya 59 Costa alijifunga na kufanya mchezo kuwa 2-2.
Alikuwa ni Jesus tena aliyeinyanyua timu yake baada ya kupachika bao la ushindi dakika ya 80 baada ya kutokea patashika kwenye lango la Yanga.
Wabrazil hao walionesha makali yao kipindi cha pili ambapo walishambulia zaidi lango la Yanga.
Yanga ambao mwishoni mwa wiki iliyopita waliikimbia Zesco ya Zambia ambayo ilikuwa wakutane katika mechi ya kimataifa ya kirafiki kwa kisingizio cha kuwa na wachezaji wengi majeruhi na wengine kuwa Cairo, Misri na timu ya Taifa ‘Taifa Stars' walionesha mchezo mzuri pamoja na mapungufu hayo.
Timu hiyo ya Brazil ambayo inashika nafasi ya tano kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya huko kesho imepangwa kuvaana na miamba wengine wa Tanzania, Simba ambapo waandaaji wametangaza kuwa hakutakuwa na kiingilio.
Simba ambao pia wamepewa ofa ya kualikwa Brazil iwapo wataibuka na ushindi wataingia uwanjani wakiwa na kumbukumbu ya kujeruhiwa na Zesco katika mechi ya kimataifa ya kirafiki mwishoni mwa wiki iliyopita hivyo, kuwa na hasira za kutaka kulipa kisasi kwa Wabrazil.
Kocha wa Simba, Patrick Phiri alipohojiwa juzi alisema anafurahi kupata nafasi ya kujipima nguvu na Wabrazil kwa sababu soka lao lipo juu zaidi ya Tanzania.
Simba na Yanga zinajiandaa na michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho hivyo wanatumia mechi hizo za kirafiki kama moja ya njia ya kujifua.