Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
- Thread starter
-
- #3,381
Omari adai Sh 10m
Friday, 21 January 2011 20:17
Sosthenes Nyoni
ALIYEKUWA mgombea wa kiti cha urais wa Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) Amani Makungu amemtaka mrajisi wa vyama vya michezo visiwani humo Mustapha Omari kumlipa Sh 10 milioni ikiwa ni fidia ya hasara aliyoipata baada ya awamu nyingine ya uchaguzi uliopaswa kufanyika Januari 18 kufutwa.
Uchaguzi huo wa awamu ya pili uliamuriwa kufanyika tena baada ya ule wa awali uliofanyika Disema 31 kubatilishwa baada ya kuwepo kwa kasoro kadhaa ikiwemo ya aliyeshinda kiti cha Uraisi Ally Ferej Tamim kubainika kukosa cheti cha kidato cha nne hali iliyomlazimu mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi Ally Suleiaman 'Shihata' kutaka urudiwe.
Makungu aliyeshindwa katika katika duru ya kwanza alisema kuwa kitendo cha mrahisi huyo kufuta uchaguzi huo na kumrudisha madarakani Ally Ferej Tamim ni ukiuwaji wa katiba.
"Nimeingia gharama kubwa kwa kujiandaa na uchaguzi, lakini mrajisi ameufuta sasa namtaka anilipe fidia ya Sh 10 milioni vinginevyo nimtamshtaki.
"Isitoshe yeye hana mamlaka ya kuzuia uchaguzi kazi yake ni kusajili vyama au kuvifuta sasa inashangaa pia amemrudisha Ferej huu ni ukiukwaji wa katiba.
"Kwa maana nyingine ni kwamba kama yeye ataakuwa na mamlaka ya kumrudisha mtu madarakani pia atakuwa na fursa nyingine ya kumfukuza mtu kitu ambacho si cha kweli,"alisema Mkungu