Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
- Thread starter
-
- #3,441
Yanga yaipiga AFC 6
Imeandikwa na Evance Ng'ingo; Tarehe: 22nd January 2011 @ 08:08
TIMU ya Yanga imeanza vema mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kuwashushia kipigo cha mabao 6-1 AFC ya Arusha na kupanda kileleni mwa msimamo wa ligi.
Ushindi huo kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam jana umewawezesha Yanga, kuwashusha mahasimu wao wakubwa Simba wakifikisha pointi 28 ambazo ni moja zaidi ya wapinzani wao ambao watashuka dimbani kesho kuvaana na Azam FC inayoshika nafasi ya nne ikiwa na pointi 20.
Vibonde AFC ambao wanashika mkia kwenye msimamo wa Ligi Kuu wakiwa na pointi 5 katika mechi 13 walizocheza, balaa lilianza dakika ya 24 ambapo mchezaji Iddi Mbaga alimalizia mpira uliopigwa na Davies Mwape.
Yanga waliongeza bao la pili kwa njia ya penalti iliyojazwa kimiani na nahodha Shadrack Nsajigwa dakika ya 28 baada ya Mwape kuchezewa rafu kwenye boksi.
Mwampe aliongeza bao la tatu kwa kichwa dakika ya 43 kufuatia krosi ya Nurdin Hamad na hivyo, kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa mabao 3-0.
Kipindi cha pili Yanga walianza kwa kasi ambapo mnamo dakika ya 50 Mbaga alifunga bao la nne akimalizia mpira uliotemwa na kipa wa AFC kutokana na shuti la Mwape.
Arusha FC walipata bao la kufutia machozi dakika ya 65 mchezaji wake Daudi Mgige alipopiga shuti la mbali lililokwenda moja kwa moja wavuni.
Dakika ya 84 Mwape alifunga bao la tano kwa kichwa baada ya kumalizia krosi ya Juma Seif, kabla ya Mwape kufunga bao lake la tatu na kukamilisha kikapu cha mabao baada ya kufunga la sita dakika ya 88.
Baada ya kumalizika mchezo mashabiki wa Yanga walikusanyika nje ya geti na kuwafanyia fujo baadhi ya viongozi wao na kuimba na kusisitiza kuwa hawamtaki Meneja wa timu Emmanuel Mpangala na kumfuata Mwenyekiti wa klabu hiyo, Lyod Nchunga ambaye alijisogeza kwa Polisi ambao waliwatawanya.
Katika mchezo wa kesho Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Phiri alisema baada ya sare ya bao 1-1 na Atletico Paranaense ya Brazil wamejifunza mengi na sasa kazi kwa Azam FC.