Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
- Thread starter
-
- #361
Simba kuingia kambini Krismasi
Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 13th December 2010 @ 23:30
IKOSI cha mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba kinatarajiwa kuingia kambini Desemba 25 kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu.
Mzunguko wa pili wa Ligi Kuu unatarajiwa kuanza Januari, Simba inaongoza msimamo wa Ligi kwa kuwa na pointi 27 ikifuatiwa na Yanga yenye pointi 25 na Azam inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 20.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Makamu Mwenyekiti wa Simba Geofrey Nyange ‘Kaburu' alisema wanatarajia kufanya maandalizi ya kutosha kwa ajili ya kumaliza ngwe ya lala salama ya ligi.
Alisema siku ambayo timu itaingia kambini itacheza mechi ya kujipima nguvu na Ulinzi ya Kenya ili kujiweka sawa baada ya mapumziko ya takriban miezi miwili.
"Wachezaji wetu wote wameshapewa taarifa na kocha wetu Patrick Phiri anatarajiwa kuwasili leo mchana (jana) kutoka Zambia,"alisema.
Simba inatarajia kuanza mzunguko wa pili wa ligi Januari 15 dhidi ya Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Jamhuri Morogoro.