Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
- Thread starter
-
- #4,081
Filamu ya Mateka wa Kiroho yaiva
Imeandikwa na Oscar Job; Tarehe: 28th January 2011 @ 23:45
MTAYARISHAJI na muongozaji wa filamu nchini Elias Magessa, amekamilisha filamu mpya inayojulikana kama Mateka wa Kiroho, ambayo tayari imeingia sokoni.
Akizungumza na gazeti hili, msambazaji wa filamu hiyo Severinus Mwijage, alisema filamu hiyo iliyoandaliwa katika Jiji la Arusha, ni mapinduzi ya filamu za hapa nchini hasa nje ya
Jiji la Dar es Salaam.
Alisema baada ya kuiandaa filamu hiyo kwa muda mrefu kwa lengo la kuifanya iwe nzuri na yenye kutoa ujumbe kwa Watanzania mapema mwaka huu wameamua kuisambaza mitaani wakianzia na Jiji la Arusha, ikiwa zawadi kwao ya kuanza kwa mwaka mpya.
Alisema filamu hiyo ilianza kutengenezwa mwaka 2009 na Kampuni ya Emags Video Entertainments ya jijini Arusha na kuwashirikisha wasanii wa kikundi cha Sanaa cha Arusha kiitwacho Agesta ambao kwa kiasi kikubwa ndiyo wamefanikiwa kuifanya filamu hiyo kuwa ya kuvutia.
"Kwa kipindi kirefu tulikuwa na kiu kubwa ya kutengeneza filamu yenye ubora kama hii iliyotengezwa nje ya Jiji la Dar es Salaam, ni furaha yetu kuona kuwa hatimaye filamu imekamilika na pia imeanza kufanya vizuri sokoni, ni imani pia wapenzi na mashabiki wa filamu nchini wataifurahia watakapoitazama," alisema Magessa.
Kwa upande wake Mwijage alisema kuanza walitengeneza nakala 3500 za filamu hiyo na kufanikiwa kuuza nakala 2600 katika Mkoa wa Arusha, ambapo ndipo walipoisambaza na
kwamba matarajio ni kuanza kuisambaza filamu hiyo katika mikoa mingine.